NEEMA ITOKAYO KWA MUNGU

1
NEEMA YA MUNGU IOKOAYO
2
NEEMA YA MUNGU IOKOAYO
UTANGULIZI:
Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu
wote imefunuliwa” (Tito 2:11).

Katika dunia hii tunayoishi wanadamu wanakabiliwa na maamuzi mbalimbali ya kufanya maishani
mwao. Maisha aliyo nayo sasa, na baadaye ni mambo ambayo kila mtu anayafanyia maamuzi,
kwamba anafanya kwa kujua au kwa kutokujua. Miongoni mwa maamuzi makubwa sana ambayo
kila binadamu anayafanya ni kuhusu mambo ya imani, yaani dini.
Dunia yetu inazo imani au dini kadhaa, ambazo pia zimegawanyika katika madhehebu au vikundi
mbalimbali. Jambo hili lazima linasababisha hali ya kuchanganyikiwa kwa watu wengi, kama hali
halisi ilivyo hasa ukizingatia kuwa dini hizo zote zinadai kuwa na Mungu mmoja wanayemwabudu.
Ni lazima mtu ajiulize swali na kulipatia jibu. Na swali lenyewe ni kwamba, Inawezekana kweli kwa
Mungu aliye mmoja, aliyeumba mbingu na nchi na vyote vilivyomo atoe miongozo mbalimbali
inayotofautiana na hata kupingana, kwa watu wake anaohitaji wamwabudu yeye peke yake? Na kama
Yeye ni mkamilifu na asiyeweza kufanya makosa, kwa nini hali iwe ya kuchanganya mawazo namna
hii?
Hivyo basi, ni hakika kuwa lazima kuna udanganyifu unaofanyika katika mambo haya ya dini. Ndiyo
sababu kwa Upendo wake usio kifani, Mungu wetu kwa kutambua kuwa hali ya udanganyifu
itakuwepo, alitupatia neno lake – yaani Maandiko Matakatifu au Biblia. Maandiko haya yanasema
hivi katika Zaburi 119:105, “NENO LAKO NI TAA YA MIGUU YANGU, NA MWANGA WA
NJIA YANGU.”
Neno la Mungu ni taa ili tusitembee gizani, ni mwanga ili tusije tukaacha njia ya kweli na kufuata njia
nyingine za uongo. Hivyo msomaji, Mungu wetu hakutuacha gizani, tulitafute neno lake kwa bidii,
na kulisoma na kujitoa kumtii katika kila jambo. Katika kitabu cha 2 Timotheo 3.:15 tunasoma “Na
ya kuwa tangu utoto umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate
wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu .” Neno la Mungu linahekimisha hata kupata wokovu .
Kwamba wokovu ni nini, na unapatikanaje, ndilo somo Kuu la Kigazeti/kijitabu hiki. Hebu fungua
moyo wako ili Roho Mtakatifu akuongoze kuyatambua mapenzi yake na kuyatenda. Kumbuka
mambo ya Kiroho hutambulikana kwa jinsi ya rohoni.
Ni ombi la Mtayarishaji.
3
HISTORIA FUPI YA ANGUKO
Maandiko Matakatifu huelezea hali ya dunia na vyote vilivyomo mara baada ya uumbaji kuwa
“Mungu akaona kila kitu alichokifanya, natazama ni chema sana…..” (Mwanzo 1.31). Hivyo
mwanadamu alikuwa mkamilifu alipotoka mikononi mwa Mungu. Je ukamilifu huu ulitokana na nini?
Ulitokana na kipimo kile ambacho Mungu alikuwa akimtazama mwanadamu - Kiwango cha
ukamilifu ambacho ni sheria takatifu ya Mungu. Na kwa kadri mtu alivyodumu katika utii huo wa
sheria au kanuni za Muumba wake, aliendelea kuwa mkamilifu. Lakini jambo moja lilitokea katika
viumbe vya Mungu. Uasi dhidi ya sheria hii takatifu ya Mungu ulitokea Mbinguni, ukianzia kwa yule
malaika aliyeitwa Lusifa, na uasi huo ukafika katika dunia yetu hii, pale Adamu na Hawa
walipomwamini shetani.
Watu wengi huwa na mtazamo tofauti wanaposikia “Sheria ya Mungu” maana hufikiria juu ya
usifanye hiki au kile – “usi” na hivyo wanafikiria juu ya Kanuni ngumu ambazo Mungu amemwekea
mwanadamu ili azifuate. Lakini je, hii sheria ya Mungu hasa ni ipi? Ni ile sheria Kuu ya Upendo.
Na ieleweke kuwa upendo huu wa Mungu sio ule tunaoufikiria na kuufahamu. Upendo huu wa
kimbingu ni ule amabao umeelezwa kama “AGAPE”. Ni Upendo usio na Ubinafsi. Unaweza
kuliona na kulitambua hili katika uumbaji – yaani Mungu alipoumba viumbe alikuwa anatoa uhai
wake na mema yake yote ili yafurahiwe na wengine, hakutaka kujilimbikizia mwenyewe. 1Yohana
4:8 anasema, “Yeye asiyependa hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni Upendo.” Ndio maana
Bwana Yesu alipoulizwa kuhusu amri iliyo kuu, alijibu kwa kuonyesha kuwa Upendo Kwa Mungu na
kwa mwingine ndio msingi wa amri au sheria (Mathayo 22:36-40). Sheria iliyo ya Uhuru – yaani ya
hiari.
Shetani alipoanzisha uasi mbinguni kwa madai kuwa Mungu ameweka Kanuni ngumu kwa viumbe
vyake kuzitii, ni kuwa alikuwa anaonyesha kutoweka kwa upendo huo wa Mungu ndani yake,
ambako kwa maana halisi ni kutoamini. Upendo ukatoweka moyoni na sasa Ubinafsi ndio ukawa
mfumo bora kwake. Na kwa sababu aliona chuki dhidi ya Mungu na sheria yake ya Upendo, kusudi
lake likawa kumuua Mungu na wafuasi wake ili aanzishe himaya yake ambayo yeye atakuwa ndiye
mkuu (soma Isaya 14:13-14). Na hii ndiyo sababu akaanzisha vita mbinguni (soma Ufunuo 12:7-9).
Baada ya shetani kushindwa vita mbinguni alishuka akiwa na ghadhabu nyingi akikusudia kuharibu
hali njema ya viumbe na mpango wa Mungu kuhusu uumbaji. Ndipo alipopata nafasi katika dunia
yetu hii. Soma pia Ezekiel 28:11-15.
Jaribu Na Anguko
Shetani alimjaribu Hawa pale Bustani ya Edeni, Alijenga jaribu lake katika kumfanya Asimwamini
Mungu. Alimfanya Hawa aone kuwa Mungu hana upendo kwao, ana ubinafsi, ndio maana
amewazuia au kuwaficha mambo fulani ambayo yangewapatia furaha zaidi; tabia ambayo kwa kweli
ni ya shetani mwenyewe. Maana shetani hakuwa na upendo kwa Mungu na viumbe vyake. Angalia
alivyomwambia Hawa “Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu
anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo Mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa
kama Mungu, mkijua mema na mabaya” (Mwanzo 3:45).
Katika maneno haya tunaona Uongo ukichanganywa na ukweli kidogo na kuleta udanganyifu Mkuu
kwa Hawa. Ukweli ni kuwa shetani hakumwambia Hawa ukweli. Watu wengi wanaamini kuwa
madai ya shetani kwamba Mungu aliwaficha Adamu na Hawa mambo fulani mazuri ni ya kweli.
Lakini hebu tuchunguze kidogo ukweli wa madai haya:-
“Hakika hamtakufa.” – Katika Mwanzo 2:17b Mungu aliishamwonya Adamu kuwa kama angeasi
angekufa, “Utakufa hakika.” Kwa hiyo maneno haya ya shetani yalikuwa uongo kabisa (soma
Warumi 6:23a). “Mtafumbuliwa Macho.” – Katika maelezo haya, Shetani alikuwa akijenga wazo
kuwa, pamoja na kwamba walikuwa wanaona, lakini bado walikuwa wamefichwa mambo fulani
ambayo ni mazuri na njia pekee ya kuyafahamu na kuyaona ni kwa kumwasi Mungu. Lakini ukweli
ni kuwa hakuna jema lolote ambalo Bwana aliwaficha. Kumbuka sheria yake ni ya Upendo usio na
Ubinafsi.
4
“Mtakuwa kama Mungu” – Kufanana na Mungu. Katika Mwanzo 1:26, “Mungu akasema ‘na tufanye
mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu…..”. Kwa hiyo shetani alijifanya kumweleza Mwanadamu hali
bora zaidi ambayo angekuwa nayo kwa kuasi. Lakini hali ya kufanana na Mungu tayari mwanadamu
alikuwa nayo. Leo, tunaposema hivi, inakuwa jambo gumu kuingia akilini. Lakini Adamu na Hawa
walimwona Mungu, wakaongea naye uso kwa uso, walimjua vizuri, ndiyo maana unapotafakari
waliwezaje kufikiri hawafanani na Muumba wao, na sasa walitafuta kufanana naye kwa jinsi ipi,
inakuwa vigumu kuelewa. Hali kamili ya kufana na Muumba wetu tuliipoteza kwa kukubaliana na
maneno ya shetani. Tulipoteza utukufu wa Mungu (soma Warumi 3:23).
“Mkijua Mema na Mabaya.” Mti wa Ujuzi wa mema na mabaya uliwekwa kuwa kipimo cha upendo
wao kwa Mungu, upendo ambao ungedhihirishwa kwa Utii wao kwa Muumba wao. Sasa swali la
kujiuliza ni kuwa, je, mwanadamu hakuwa na Ujuzi wa jambo lolote kabla ya kula matunda ya mti
Huu? La, alikuwa na Ujuzi wa mema, maana haya yaliumbwa ndani yake (soma Waefeso 2:10) na
ndiyo aliyotenda tu hadi siku ile alipoanguka (soma Mwanzo 1:31; 3:2-3).
Kula matunda ya mti huo kuliongeza kitu kigeni – kulifungua mambo mabaya (maovu) ambayo
mwanadamu hakutegemea ndiyo yangekuwa matokeo ya uasi wao. Na mabaya hayo yanazidi
kuzaliana hata leo. Badala ya ujuzi huo kuleta Mema kama shetani alivyowatumainisha, umeleta
misiba na mauti, na kumtenga Mwanadamu mbali na Muumba wake. Matumaini aliyowapa yakawa
ya uongo. Kutokana na kupandikiza Ubinafsi ndani yao walitegemea kufaidika, kumbe ikawa hasara
ya milele.
Kwa njia hii shetani alifanikiwa kumfanya mwanadamu kumtazama Mungu kwa picha nyingine.
Badala ya kumuona kama Muumbaji wao anayewapenda na kupenda kuwapatia mema, walimwona
Mungu kama Mtawala aliye na ubinafsi na aliyeweka sheria ngumu kwa viumbe vyake ili kuzitii. Na
huu ndio mtazamo wa mamilioni ya wanadamu leo kumhusu Mungu. Shetani akafanya Mungu
aonekane kwa sura ambayo kwa kweli ni ya Shetani mwenyewe yaani Ubinafsi. Dini hii
ikaanzishwa. Muumbaji wetu akawa adui yetu, na shetani aliyekuwa adui akawa rafiki yetu.
Ubinafsi huu ndio msingi wa dini au imani zote zisizomkubali Yesu kama njia pekee ya wokovu.
Mara baada ya anguko mwanadamu alipoteza haki zote alizokuwa amepewa na Mungu. (Kumbuka
kuwa uumbaji lilikuwa ni tendo la Mungu la Upendo, alilolifanya kwa hiari yake mwenyewe, na
viumbe vyote ili vifurahie uumbaji wao vilipaswa kuishi kwa kanuni ambazo ziliwekwa na Muumbaji
wao). Haki ya mwanadamu saa hiyo ilikuwa ni kufa palepale, maana alikuwa amejiondoa chini yake
aliye asili ya uhai au uzima. Kwa hiyo Mungu alikuwa na haki kabisa ya kuchukua dunia yake na
viumbe wengine wote aliowaweka chini ya mamlaka ya Adamu na kuviondoa, Je mwanadamu
angeelea angani? Lakini, anga pia ni la Mungu. Kadhalika Muumbaji alikuwa na haki ya kuchukua
pumzi yake ya uhai na mwanadamu kurudia udongo tena. Ni hakika kwa tendo la Ubinafsi ambalo
mwanadamu alitegemea kujipatia zaidi, sasa alipoteza vyote.
Matokeo ya Uasi yalikuwa Nini?
Mwanadamu alipoteza utukufu wa Mungu (soma Mwanzo 2:25; 3:7; Rumi 3:23).
Alipoteza haki ya kuwa hai (uzima wa sasa na wa milele) (soma Mwanzo 2:17).
Alijifanya kuwa adui wa Mungu (soma Mwanzo 3:8).
Alipoteza uwezo wa kutii sheria za Mungu (soma Zaburi 14:23).
Katika hali hii mwanadamu alipoteza uhusiano na Mungu – Ndipo Biblia inasema “Toka Mbinguni
Bwana aliwachungulia wanadamu, Aone kama yuko mtu mwenye akili, amtafutaye Mungu. Wote
wamepotoka, wameoza wote pamoja. Hakuna atendaye mema, La! Hata mmoja,” (Zaburi 14:23).
“-------Hakuna mwenye haki hata mmoja. Hakuna afahamuye, Hakuna amtafutaye Mungu.”
(Warumi 3:10-11). Katika Isaya sura halisi ya uasi imefananishwa na mgonjwa ambaye labda,
kamwe hujawahi kukutana naye au kumwona, inasema “---------Kichwa chote ni kigonjwa, moyo
5
wote umezimia. Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na
machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala
havikulainishwa kwa mafuta,” (Isaya 1:5-6).
Je, mtu wa Mungu unajua hivi ndivyo tunavyoonekana katika hali yetu ya uasi na darubini ya
Mbinguni? Je mgonjwa wa jinsi hii atawezaje kujiokoa au kujiponya mwenyewe? Hata kama
angetaka kufanya, kumbuka neno la Mungu linasema “tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna
uzima ndani yake” – amekufa. Hakika hakuna njia ya kujinasua wenyewe katika hali hii. Hii ndiyo
hali yetu pasipo Kristo. Tafakari kwa Makini.
Mungu Aingilia Kati
Sheria takatifu ya Mungu iliyovunjwa ilidai uhai wa yule Mhalifu (soma Mwanzo 2:17). Lakini kwa
Upendo Mkuu wa ajabu, Mungu aliandaa mpango wa pekee utakaompatia mwanadamu nafasi
nyingine ili kuweza kuishi kwa kanuni hii ya Kimbingu yaani Upendo usio na Ubinafsi. Mpango
huo ndio unaoitwa Mpango wa Wokovu (soma Zaburi 111:9).
Mpango wa Wokovu
Mungu alitangaza kwa mwanadamu na nyoka juu ya kile atakachokifanya kati yao. Kumbuka baada
ya uasi mtu akawa adui wa Mungu na rafiki ya shetani. Mpango huu wa wokovu ambao ni wa
Mungu mwenyewe ulifanya kitu. Mwanzo 3:15 inasema, “Nami nitaweka uadui kati yako na huyo
mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake, huo utakuponda kichwa na wewe utamponda
kisigino.” Mungu akavunja urafiki kati ya Mwanadamu na Shetani kwa kuweka uadui – na hicho
alichofanya ndiyo “Neema.” Wengi wameelekeza zaidi mawazo yao kwa hawa nyoka wa kawaida
na kumsahau Shetani mwenyewe ambaye ndiye adui hasa (soma Ufunuo 12:7-12, 17).
Mungu wetu akijua kile ambacho kingetokea, aliandaa mpango wa wokovu tangu Mwanzo. Katika
Ufunuo 13:8b tunasoma, “------Mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia”. Soma
pia 1 Petro 1:18-20. Ni kwa sababu Bwana Yesu alikuwa amekwishajitoa kuwa “mwanakondoo wa
Mungu achukuaye dhambi za ulimwengu” ndio maana Adamu na Hawa hawakufa mara tu
walipokuwa wamekula matunda ambayo Mungu aliwakataza wasile. Lakini pia wanadamu
tumeendelea kujiuliza swali moja kubwa kuhusu jambo hili na mara nyingine majibu labda
yameonekana kutotosheleza mashaka ya mwanadamu.
Lakini kama tukitafakari kwa makini ukweli wenyewe tutaridhika. Swali lenyewe ni hili “Kama
Mungu alijua yote yatakayotokea, kwa nini hakuyazuia? Na kwa nini hakumwangamiza shetani mara
tu alipoasi ili asiambukize uasi wake kwa viumbe wengine?
Jibu ni kuwa Mungu ni Upendo, na upendo unaandamana daima na haki (yaani kutenda haki). Je,
hatua za kuzuia uasi zilifanyika? Ndiyo. Kwanza kwa kufundisha viumbe vyote juu ya kanuni hii kuu
ya kimbingu yaani Upendo. Hivyo viumbe vilipaswa kuishi kwa kanuni hiyo tu ili kudumisha furaha
ya ulimwengu. Lakini pia shetani alipoanzisha uasi rasmi, Mungu alimwonyesha wazi matokeo yake,
na kumsihi aachane na mipango yake iliyokuwa kinyume, lakini hakukubali. PP - Chapter isemayo
‘why was Sin permitted’?
Kwa nini asimharibu shetani mara moja? Tafakari kwa makini unajua Mungu wetu alishitakiwa na
shetani kwa viumbe wake kuwa - Yeye si mwenye haki. Hakutoa uhuru ili wao (viumbe) waishi kama
wapendavyo. Yaani ni mtawala asiyewapenda na asiyependa furaha yao. Kama Mungu
angemwangamiza shetani palepale. Hakika shetani angeonekana kuwa mkweli, na ile kanuni ya
Upendo usio na Ubinafsi ingekuwa imevunjwa na Mungu mwenyewe. Lakini kwa kuwa Mungu ni
upendo na yeye habadiliki ndio maana ilibidi ushahidi udhihirike wazi kwa viumbe wote kuwa ni nani
hasa aliye mwema - Mungu au shetani? Kumbuka daima haki ina gharama.
6
Kwa hiyo ili Mungu audhihirishe upendo wake na haki yake - dhambi imemgharimu sana kuliko
tunavyoweza kufikiri. Ili hatimaye viumbe wenyewe waamue na kukiri kuwa - Hakika Mungu wetu
ndiye mwenye haki. Kumbuka mashitaka yoyote yanahitaji ushahidi, hivyo mshitaki aeleze
mashitaka yake yasikilizwe na kupimwa. Na mshitakiwa naye aeleze ukweli usikilizwe na kupimwa.
Sasa tafakari maelezo machache yafuatayo:-
1. Malaika waliishafanya uamuzi juu ya ukweli kuhusiana na mashitaka haya.
Theluthi ya malaika waliamua kuungana na Shetani (soma Ufunuo 12:3-4). Theluthi
mbili walidumisha utii kwa Mungu.
2. Sayari nyingine ambazo hazikuasi zilikwisha fanya uamuzi, na kudumu kuwa upande
wa Muumba wetu (soma Ufunuo 12:10-12)a.
3. Dunia yetu ilimkubali shetani na kanuni zake za Ubinafsi, lakini Mungu
wetu kwa Upendo aliingilia kati ili kutuokoa. Unajua kwa nini hadi leo vita hii
haijafikia mwisho wake? Ni kwa sababu wanadamu tumeendelea kudumu katika njia
panda kwa mda mrefu. Wapo waliokwisha kuchagua kuwa upande wa Mungu
(wachache), wapo wameamua kuwa upande wa Shetani, na wengi sana hawajajua la
kufanya. Ukweli ni kwamba, ijapokuwa wanadamu wengi wanadai kuwa na imani
kwa Mungu kwa madai kwamba wana dini, lakini imani ya kweli haiko wazi kwa
mamilioni ya watu. Yawezekana ukawa mmoja wao!! Kwa hiyo ndiyo maana
Mungu anatusubiri tufanye uamuzi huo. Lakini ni lazima watu waamue kwa
kufahamu wazi ni nini wanachofanya. Ndiyo maana Bwana Yesu, baada ya kueleza
dalili nyingine zitakazoonyesha mwisho wa dunia, akasema “Tena habari njema ya
Ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote, hapo
ndipo ule mwisho utakapokuja” (Mathayo 24:14)
Je, mpendwa unajua kuwa mahubiri mengi sana ambayo yamekuwa yakifanyika hayajahubiri hii
“habari njema ya Ufalme” kwa nuru yake halisi? Na je, wewe binafsi unafahamu hiyo habari njema
ni ipi? Napenda kukujulisha kuwa hili ndilo somo kuu la maandiko haya. Unapokuwa ukiendelea
kujifunza, hebu uwe mwenye maombi ya kweli na makini ili kujifunza, kuelewa, kuupokea na kuuishi
ukweli huu wa pekee, Mungu akubariki, anakusubiri ufanye uchaguzi sasa na si baadaye - ili vita kuu
ifike mwisho (soma 2 Kor. 6:2).
KRISTO HAKI YETU
Mungu ashukuriwe kwa kumtoa Bwana Yesu kwa ajili yetu. Unapoendelea kujifunza mpango huu
wa ukombozi daima zingatia maneno haya “Kristo haki yetu.” Kile ambacho Wanadamu tulipoteza
katika Adamu, Mungu wetu amekirudisha katika Kristo Yesu. Ndiyo maana mpango huu kwa hakika
ni wa kumrudisha mwanadumu katika hali ile aliyokuwa nayo kabla ya kuanguka dhambini. Sasa
swali - Kristo anakuwaje haki yetu? Kumbuka kuwa mara baada ya uasi, mwanadamu alikuwa
amejitenga kabisa na Mungu, lakini Mungu ndiye asili ya vyote, kwa hiyo mtu hakuwa tena na haki
ya kutumia chochote kilicho cha Mungu - tangu pumzi ya uhai, chakula, mwanga wa jua, dunia
yenyewe, maji na kila kitu unachoweza kukifikiria. Mwisho wake ulikuwa ni kifo tu, tena cha milele,
maana angewezaje kuupata tena uhai na yeye alipewa tu na Mungu? Ndiyo maana katika Biblia Yesu
anasema, “---- Mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele” (Yohana 10:10). Ni kwa
sababu ya kafara ya Kristo ndio maana tuna uzima huu wa sasa (uzima) na kisha kuna ahadi ya uzima
tele (wa milele) katika ufalme wake ujao. Kwa hiyo vyote tunavyopata ili kutusaidia sasa kwa maisha
haya vimenunuliwa kwa damu ya Yesu ya thamani - yaani hewa tunayovuta, nuru ya jua, mvua, maji,
chakula na vingine vyote. Unapolitambua hilo, ndipo hutakuwa mharibifu au mtumiaji mbaya
asiyejali vitu hivyo. Kwa hiyo kama isingekuwa Kristo Yesu, wanadamu wote tusingekuwepo.
Tunaishi leo kwa kuwa yeye - Yesu - ametununulia haki hiyo. Na kwa vile mauti ilikuwa ya milele,
pia kwa kafara yake ametu-nunulia uzima wa milele. Kwa hiyo utaona kuwa mwanadamu hana
chochote anachoweza kukidai kuwa kingempatia haki ya kuishi, isipokuwa tu-kile alichofanya
Mungu wetu kupitia kwa Yesu Kristo Bwana na Mwokozi wetu. Ni haki ya Kristo tu inayotupatia
vitu vyote. Ndio maana yeye ni haki yetu. Je, ulifahamu hayo? Au ni kitu kipya? Na je, watu
wengine wanafahamu hivyo? Je, unajua kuwa katika Kristo Yesu, tuna haki ya kuishi sasa, na
7
hatimaye milele siku ile ajapo? Hii ndiyo habari njema. Je umeielewa vizuri na kuipokea? Kwa
sababu habari hii ndiyo “Injili” yenyewe, hakika tunahitaji kuifahamu vizuri ili kuipokea au kuikataa.
Na kwa kuwa hakuna ukweli mwingine zaidi ya huo, kumbe ni ujumbe muhimu sana kwa maisha
yetu. Hebu tafakari fungu lifuatalo:-
“Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda Ulimwengu, hata akamtoa mwanawe pekee, ili kila
mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele”. Yohana 3:16.
Mungu wetu alipenda na kutoa. Sisi tunachotakiwa kufanya ni kuamini tu. Kama ujumbe ndiyo huu,
mbona inaonekana kuwa Wakristo, ambao ni wengi duniani, wamekuwa wakidai wanauamini na
kuuhubiri, na bado inaelekea mwisho hauji? Endelea kujifunza na nuru zaidi itakuangazia.
Jambo la muhimu ni kwamba, kama “habari njema ya ufalme” itaeleweka vizuri na kupokelewa, au
kama watu wote wataamua kuhukumu kesi hii ambayo Mungu ameshitakiwa, kwa kujiweka upande
wa Mungu au Shetani - dunia hii itashuhudia mabadiliko makubwa ambayo hayajawahi kuwepo tangu
dunia kuwepo, na ndipo mwisho utakapokuja. Sasa swali jingine ni hili - Je, tunawezaje kuupokea
ukweli huu ili uwe halisi maishani? Neno la Mungu linasema ni kwa njia ya Imani - Yohana 3:16.
Ndipo tunapoingia katika hatua nyingine ya somo hili. Unajua kwa nini maisha ya kumcha Mungu
yanaonekana kuwa ni maisha magumu (yaani ni mzigo) kwa watu wengi? Ni kwa sababu
hatujamfahamu Yesu na kumpokea kama haki yetu - Habari njema. Watu wengi sana wanajaribu
kumfanya Mungu awapende kwa kujitahidi kutenda mema. Lakini neno la Mungu linasema yeye
hajawahi kutuchukia hata wakati mmoja - yaani siku zote anatupenda. Wengi tunajaribu kumpenda
Mungu ili atusamehe dhambi na halafu atupatie uzima wa milele, asitutupe jehenamu. Lakini unajua
haya yote Mungu amekwishayafanya kwa ajili ya watu wote katika Kristo? Yaani, Kwa njia ya
Kristo Yesu, wanadamu wote tumesamehewa dhambi (Kupatanishwa na Mungu) na hivyo
uzima wa milele ni matokeo ambayo hayana budi kutokea kwa kila atakayekubali kuamini ukweli
huu. Na ndipo maisha ya kumfuata Kristo yatakuwa furaha tupu - iwe ni katika raha au shida. Biblia
itadhihirisha ukweli huu. Ndiyo maana injili ni habari njema. Haiwezi kuwa njema halafu hapo hapo
iwe mbaya au mzigo. Kumbuka: Ukiona dalili ya uumini kuwa mzigo au adhabu maishani, basi
umeanza mahali pasipo sahihi. Tafuta uanze upya, maana vinginevyo hutafika pale ulipokusudia.
Lakini kwa bahati mbaya sana, wengi tunaosema ni Wakristo, hiyo ndiyo hali yetu. Endelea
kujifunza ili uwe na amani ya Yesu moyoni. Ni heri kwetu kama tutaanza upya kwa usahihi kuliko
kuendelea na kile tunachodhani pia ni sawa tu - kisitufae.
INJILI KATIKA AGANO LA KALE:
Watu wengi sana huamini kuwa kipindi cha agano la kale watu walikubalika mbele za Mungu kwa
kuzishika sheria, na kipindi baada ya kuja Kristo sasa tunakubaliwa kwa neema. Lakini, je, umewahi
kujiuliza kuwa kama watu waliokolewa kwa kuzishika sheria, wale wanyama waliotolewa kafara
walikuwa wa kazi gani? Je, Mungu alikuwa anajaribu mpango ambao anajua wazi hauwezekani? Je,
ni kweli huu ulikuwa ndio mpango wa Mungu? La, hasha. Kwa sababu Shetani anafahamu vizuri
nguvu ya watu kuipokea injili, yaani habari njema, basi tangu mwanzo alianzisha mfumo ulio tofauti
kabisa na mpango wa Mungu, lakini ulioigizwa na kuonekana kama ndio mpango wa Mungu. Hebu
sasa tuingie kwa undani zaidi kuona ukweli huu.
ADAMU: Kumbuka, Mungu aliweka uadui kati ya mtu na Shetani (soma Mwanzo 3:15). Baada
ya kutangaza mpango huo ambao kwa kweli bila Yeye (Mungu) Adamu hakuwa na
mpango wowote wa kumrudia, Bwana alimfundisha Adamu somo la kwanza kabisa
jinsi atakavyoonyesha Imani yake kwa kile ambacho Mungu alikifanya kwa ajili
yake. Mungu alimfundisha ibada ya kutoa kafara.
Adamu alitetemeka kwa hofu kuu kuona akitoa uhai wa mnyama asiye na hatia
badala yake, uhai ambao ni Mungu pekee awezaye kuutoa, aliona ubaya wa dhambi
kwa sura tofauti kabisa kuliko kabla ya hapo, kama ambavyo dhambi itaonekana kwa
yeyote anayemtazama mwanakondoo wa Mungu pale Msalabani. Adamu alipoelezwa
kwa upana mpango wa kumwokoa, jinsi ambavyo kwa dhambi yake inabidi mwana
pekee wa Mungu ashuke, atwae ubinadamu, azaliwe, ateswe na mwisho kufa
8
msalabani, alisikitika kwa huzuni ya ajabu. Ndipo akaomba kuwa yeye (Adamu)
pamoja na uzao wake walipe gharama hiyo badala ya Mwana wa Mungu. Lakini
alielezwa kuwa asingeweza kulipia gharama hiyo, Malaika nao walipoelezwa
mpango huo, wakajitoa ili kufa kwa ajili ya mwanadamu badala ya Bwana wao
wanayempenda sana, lakini nao pia waliambiwa hawawezi kulipa gharama ya
ukombozi. Kwa nini wasiweze?
1 Ni kwa sababu sheria ya Mungu iliyovunjwa ni takatifu sana
kuliko kiumbe chochote, maana ndiyo tabia ya Mungu mwenyewe. Hivyo ni
yule aliye sawa na Baba, ambaye pia alishiriki katika uumbaji, ndiye tu
angeweza kutosheleza matakwa ya sheria ya Mungu iliyo takatifu sana, soma
- PP - Chapter - the Plan of Redemption.
2 Mwanadamu alikuwa amepoteza utukufu wa Mungu - hivyo
lazima aupate kutoka kwa yule aliye asili ya utukufu - yaani Mungu
Mwenyezi.
3 Mwanadumu alipoteza uzima na kiumbe yoyote hana asili ya
uhai, isipokuwa Mungu Mwenyewe, yeye ndiye mtoaji (mpaji). Ndiyo
maana ilibidi Bwana Yesu aliye sawa na Baba alipe gharama ya ukombozi
wetu. Adamu na Hawa waliipokea injili hii iliyohubiriwa kwao, na
walionyesha imani yao katika Kristo kwa ibada ya kafara ya wanyama kama
Mungu alivyowafundisha. Nao pia wakawafundisha watoto wao mpango
huo wa wokovu na ibada kuhusu mpango huo.
Kaini na Habili
Watoto hawa wawili wa Adamu walifundishwa kumwabudu Mungu na pia ibada hiyo ifanyikeje, na
maana ya ibada hiyo. Biblia inaonyesha ibada za hawa vijana wawili katika Mwanzo 4:3-5: “Ikawa
hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana, Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa
wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama, Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake, bali
Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake, Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana”. Biblia
haisemi hili lilikuwa tukio la ngapi la ibada, lakini inaonyesha tofauti ya pekee iliyojitokeza na
matokeo yake. Pia ieleweke kuwa tukio hili ni tofauti kabisa na utoaji wetu wa sadaka leo ambapo
mtu hutoa kile alichonacho. Ili ionekane kwa nini sadaka ya Kaini isikubaliwe wakati yeye kama
mkulima alitoa kile alichokuwa nacho, zingatia kuwa hii ilikuwa ibada maalum ya kutoa kafara
ambayo kwa hiyo walionyesha imani kwa mwanakondoo wa Mungu achukuaye dhambi za
ulimwengu. Kwa hiyo ilikuwa lazima kiwakilishi halisi kitumike bila kubadilisha. Na ieleweke
kuwa hata leo tutakuwa tunafanya ibada kama ya Kaini, kama katika mahali mbingu zilipoweka kitu
maalum kutumika kwa ibada, Tutaweka kitu kingine tofauti. Hakitawakilisha kile kilichokusudiwa
na Mungu na hivyo tutakuwa tunaonyesha kukosa imani kwa Mungu - kutoamini.
Sasa katika ibada hii ya Kaini ndiyo tunapoanza kuona hasa kanuni za Babeli zikitenda kazi. Shetani
akaweka injili nyingine (bandia) badala ya ile ya kweli, Injili ya kweli inasimama katika msingi huuwokovu
ni katika Kristo Yesu kwa njia ya imani; wakati ile injili bandia ina msingi huu - wokovu
unapatikana kwa imani na matendo - yaani ni kitu mtu anachopata kutokana na juhudi zake
mwenyewe na pale anaposhindwa, basi Mungu anafanya. Na injili hii bandia imeshika mateka
wanadamu wengi sana - tangu wale wanaojiita wakristo wa madhehebu yote na dini zote nyingine
duniani - Uislamu, Hinduism, Buddha, n.k. Ndiyo maana injili ya kweli ya milele, ile iliyotangazwa
na Mungu mwenyewe pale Edeni inahitajika ifahamike katika nuru yake halisi - halafu kila mtu
aamue kumpokea Yesu kama tumaini lake pekee la wokovu au kumkataa; na ndipo kila mtu
atakapokuwa amekwishafanya uamuzi, Yesu aendelee kusubiri nini? Hapo ndipo ule mwisho
utakapokuja. Nuru hii imefunuliwa kwa namna ya peke katika Kanisa la Mungu la Masalio. Lakini
wengi sana miongoni mwetu hatujaifahamu na kuipokea, halafu kuipeleke kwa ulimwengu. Je,
tutaendelea kuipuuzia hata lini? Mauaji yanayoendelea kuikumba dunia, vita, magonjwa na misiba
9
mingine mingi inatusonda kidole watu wa Mungu kuwa tunaendelea kuchelewesha ule mwisho.
Unapotafakari mambo haya mazito hebu liwe ombi letu kuwa Bwana atusaidie kuufahamu ukweli
huu, kuuamini na kuuishi ili kazi yake imalizike na aje kukomesha mateso ya watu na ya viumbe
wengine yaliyosababishwa na dhambi.
Kumbuka Habili alikwenda mbele ya Mungu akionyesha imani kwa kile Mungu alichofanya kwa ajili
yake, na Kaini alionyesha kutoamini mpango wa Mungu na akaenda na mpango wake mwenyewe wa
kazi za mikono yake - yaani matendo, kumbuka mpango huu wa wokovu ni wa Mungu mwenyewe
hivyo ili tuokolewe, inatupasa kufuata kile alichosema Mungu kwa usahihi.
Ibrahimu:
Anajulikana kama “Baba wa imani”. Mara Bwana Mungu alipomwita atoke katika nchi ya kwao
aende katika nchi ambayo yeye Bwana atamwonyesha, Ibrahimu aliondoka bila swali kuwa nchi
anayoiendea ikoje, watu wake wakoje, ina rutuba, au ni jangwa, bali alimwamini yeye
aliyemwita(soma Mwanzo 12:1-7). Bwana akampa Ibrahimu ahadi nyingine, “Akamleta nje,
akasema, tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu, Akamwambia, ndivyo
utakavyokuwa uzao wako. Akamwamini Bwana, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki” (Mwanzo
15:5-6). Mungu akaendelea kufanya agano na kumpa Abrahamu ahadi zaidi (soma Mwanzo 15:8-21).
Zingatia: Kitu alichotakiwa akifanye ni “kulishika agano la Bwana” (Mwanzo 17:9), yaani katika
maelezo yote utagundua kuwa Mungu anaahidi atakachomfanyia Abrahamu na wala si Abrahamu
atamfanyia Mungu nini. Ibrahimu hakutoa ahadi yoyote, isipokuwa alipokea daima kile Mungu
alichokuwa akimfanyia, na ndiyo maana alifikia uhusiano wa juu sana na Mungu, kiasi cha kuwa
tayari kumtoa mwanawe pekee - Isaka - kuwa sadaka ya kuteketeza kwa Bwana. Unajua wengi sana
tunakosea tunapotafuta uhusiano na Mungu kwa kujaribu kushika sheria fulani, kwa kweli hilo
haliwezekani. Uhusiano wa kweli kati yetu na Mungu, utatokana na kupokea kwa imani kile
ambacho Mungu ametufanyia. Kumbuka Adamu na Hawa walijificha walipomsikia Bwana bustanini,
je wewe na mimi tunaweza kufanya zaidi ya hayo? Soma Warumi 4:1-22 na utafakari kwa makini
jinsi Mungu alivyomhesabia haki Ibrahimu. Ni kwa imani tu, wala si kwa imani na matendo. Je
unaona mashaka kuhusu ukweli huo? Endelea kujifunza kwa makini. Imani kwa Mungu hongoza
kwenye utii. Imani ni sawa na mtu na matendo (utii) ni matokeo ya imani.
Ismaili na Isaka (Maagano Mawili)
Hawa walikuwa ni watoto wa Ibrahimu. Mmoja alizaliwa kwa mjakazi na mwingine kwa mke halali.
Wa mjakazi alizaliwa kwa mwili - yaani ni kwa mpango wa Ibrahimu mwenyewe na wa pili alizaliwa
kwa ahadi. Katika wana hawa wa Ibrahimu, kuna somo kubwa sana la imani. Ismaili, aliyekuwa
mtoto wa mjakazi, alizaliwa kutokana na kutoamini. Kumbuka, Mungu aliishamwahidi Ibrahimu
kuwa atampatia uzao mwingi (soma Mwanzo 12:2-7; 15:4-6, 13-16, 18). Lakini mashaka yao kwa
Mungu yalifanya atafute njia yake mwenyewe ya kupata mtoto. Kama ilivyokuwa kwa Adamu,
ndivyo ilivyokuwa kwa Ibrahimu. Sara mkewe, akamshawishi atende kinyume na mpango wa
Mungu. Kwa hiyo Ismaili ni mfano wa kazi ya mtu mwenyewe - yaani imani na matendo. Na Isaka
ni kielelezo cha haki ipatikanayo kwa imani - haki ile itakayo kwa Mungu. Ismaili ni mfano wa
agano la kale (haki kwa matendo) na Isaka ni mfano wa agano jipya au agano la milele (haki kwa
imani) (soma Wagalatia 4:21-31). Sasa shida ilitokea baada ya kuzaliwa mtoto wa ahadi, maana sasa
wako wawili, je ni yupi mrithi? Mwanzo 21:8-12 inasema, “Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya,
Ibrahimu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya. Sara akamwona yule mwana
wa Hajiri Mmisri (Ismaili) ambaye alimzalia Ibrahimu, anafanya dhihaka. Kwa hiyo Sara
akamwambia Ibrahimu, mfukuze mjakazi huyu na mwanawe, maana mwana wa mjakazi hatarithi
pamoja na mwanangu, Isaka. Na neno hilo lilikuwa baya sana machoni pa Ibrahimu, kwa ajili ya
mwanawe. Mungu akamwambia Ibrahimu, Neno hili lisiwe baya machoni pako, kwa ajili ya huyo
mwana, na huyo mjakazi wako. Kila akuambiacho Sara, sikiza sauti yake, kwa maana katika Isaka
uzao wako utaitwa”. Katika kisa hiki kuna mambo kadhaa ya kujifunza:
10
1. “Mtoto kukua na kufanyiwa dhihaka.” - Unajua, daima katika maisha yetu ya kiroho, ile haki
binafsi yaani ya matendo, siku zote hudhihaki ile haki ipatikanayo kwa imani. Yaani tunajisifia
haki yetu wenyewe badala ya haki ya Mungu iliyo katika Kristo Yesu kwa njia ya imani (soma
Luka 18:9-14). Ndani yetu kila mmoja, haki hizi mbili hushindana daima, na mtu binafsi ndiye
ataamua ni haki ipi ishinde. Ndiyo, maana Nafsi ndiye adui mkubwa tuliye naye wa kwanza
tunayepaswa kumshinda (soma Mathayo 10:38-39; 16:24-25, Luka 9:23).
2. “Sara akamwambia Ibrahimu, mfukuzemjakazi huyu na mwanawe.” - Hapa tunapata somo
jingine tena. Kama neno la Mungu linavyosema, Sara ndiye aliyemshawishi Ibrahimu ili apate
mtoto kwa Hajiri. Kwa hiyo, yeye mwenyewe (Sara) lazima afanye toba kwa kosa alilofanya.
Ndiyo maana ilibidi yeye ndiye aanzishe mpango huo kati yake na mumewe. Katika maisha yetu
leo, kila mtu anayo haki yake binafsi aliyojifanyia, na hakuna mtu mwingine atakayefanya toba
kwa ajili ya mwingine ili kuiondoa hiyo haki bandia. Lazima kila mtu afanye kazi hiyo yeye
mwenyewe (soma Luka 9:23).
3. “Hatarithi pamoja na mwanangu.” - Kumbuka Ismaili na Isaka ni mfano wa haki mbili tofauti - ile
ya Mungu na nyingine ya mwanadamu. Sasa, Katika kurithi ufalme wa Mungu, kwa kweli ni haki ya
Mungu tu, itakayotupatia urithi, na wala si haki yetu binafsi. Wala sio haki ya Mungu pamoja na haki ya
mwanadamu. Zingatia sana maneno haya usije ukajuta baadaye (soma Warumi 8:28-30, Mathayo 25:34,
37, 46). Kristo ndiye haki yetu pekee ya kuokolewa.
4. “Neno hilo likawa baya sana machoni pa Ibrahimu.” - Kila mmoja wetu anaweza kulishuhudia
jambo hili maishani mwake. Yaani matendo yetu yote mema tunayotenda hayawezi kutupatia
urithi!! Hakuna lolote la kujisifia! Jambo hilo daima katika utu wetu wa asili ni baya sana
machoni petu. Nafsi, nafsi, nafsi, hutafuta kujiinua. Ndiyo maana hata kuiamini “habari njema
ya ufalme” huwa ni shida sana. Nafsi hairidhiki kumpatia mwingine sifa zote. Hivyo lazima kitu
kifanyike dhidi ya nafsi (haki binafsi), na hicho ndicho neno lifuatalo (soma Mathayo 16:24, Luka
14:26) - KUJIKANA NAFSI.
5. “Mfukuze mjakazi na mwanawe,” (Wagalatia 4:30). - Lazima haki binafsi ifukuzwe, vinginevyo
hakuna kurithi. Itafukuzwa kwa njia gani? Kwa kuisulubisha nafsi daima (soma Marko 8:34), maana nafsi
daima hushindana na haki ya Mungu (roho) (soma Wagalatia 5:16.17).
Maagano Mawili: Isaka na Ismaili ni mfano wa Maagano Mawili - moja la Sinai na jingine la
Yerusalemu wa juu. Ieleweke kuwa maagano haya si yale ya vitabu vya Biblia - yaani kipindi kabla
na baada ya kuzaliwa Kristo, Maagano haya ni:
ß Agano la Mungu kwa Wanadamu, yaani kile Mungu alichoahidi kutufanyia. Na agano hili ndilo
linaitwa “Agano la Milele” au “Agano jipya” (soma Waebrania 8:8.10). Katika Kristo Yesu (soma Zaburi
111:9).
ß Agano la mwanadamu kuahidi kile atakachomfanyia Mungu. Nalo huitwa “Agano la Kale”
(soma Waebrania 8:9). Agano hili limeelezwa katika ahadi ambayo Waisraeli waliahidi kufanya
yote Mungu aliyosema (soma Kutoka 19:8). Lakini unaposoma Biblia, utaona wazi kuwa Israeli
hawakuweza kufanya kile walichoahidi. Na pia ieleweke kuwa ni hapa katika ahadi hii ambapo
torati inasema “Ayatendaye hayo ataishi kwa hayo,” (Wagalatia 3:12, soma pia Walawi 18:5).
ß Kama tulivyokwisha kuona, kutokana na matokeo ya uasi, kwa kweli hakuna mwanadamu
anayeweza kutosheleza madai au matakwa ya sheria ya Mungu (soma Waefeso 2:8-9).
Wanadamu wengi sana tunasumbuka katika utumwa huu ambao kwa kweli tunamhitaji Kristo ili
atuokoe nao. Hebu kumbuka ni mara ngapi umahidi kumfanyia Bwana mambo fulani, iwe ni kwa
siri moyoni mwako, kwa kuinua mkono kanisani, kwa kusimama wito unapotolewa au katika
nyimbo nyingi tunazoimba kanisani, halafu angalia umeyatimiza kwa uaminifu kiasi gani. Ni
hakika, mengi kabisa hatujayatimiza kulingana na ahadi zetu kwa Bwana. Matokeo yake
unayajua? Ni yale kuona kuwa Ukristo ni mgumu sana, ni mzigo mzito Mungu aliotupatia
kuubeba, na matokeo yake ni kumwona Mungu kama mkandamizaji anayetaka tufanye mambo
magumu tusiyoyaweza (soma Wagalatia 4:24). Na hivyo wengi hatuna amani na Mungu,
11
Mwisho wake ni kukata tamaa na kusema, “Bwana anawajua walio wake, na kama mimi ni wake
ataniokoa tu kwa njia yoyote ile, na kama mimi si wake basi hata nikijitahidi vipi bado siwezi
kuokolewa”. Na kwa jinsi hii wengi tunamchukia sana Mungu kiasi kuwa kama tungepata nafasi,
na sisi tutamsulubisha msalabani. Njia pekee itakayotupatia amani ni kuikubali haki ya Mungu,
agano lake kwetu (soma Warumi 5:1).
KUHESABIWA HAKI (HAKI KWA IMANI)
Haki ni nini? Ni kutenda haki (mema) au utakatifu. Je, mtu yeyote anaweza kuitenda iliyo haki? La,
hasha maana ndani yetu sisi, hakuna lililo jema (soma Warumi 7:14-19). Mti mbaya unawezaje kuzaa
matunda mazuri, (Mathayo 12:34)?
Nini maana ya kuhesabiwa? Kuhesabiwa ni kupewa kitu bila kukifanyia kazi au bila kustahili. Hivyo,
kuhesabiwa haki au utakatifu ni kupewa haki hiyo sisi tulio wadhambi. Yaani badala ya kuhesabiwa
kuwa wadhambi tunahesabiwa kuwa watakatifu. Je, jambo hili linawezekana kabla ya sisi kushika
amri za Mungu? Ndiyo na ndivyo ilivyo maana ndani yetu hakuna jema. Haki hii tunayopewa bure
ni ya nani? (soma Isaya 52:3). Isaya 45:24.25 inasema, “---- kwa Bwana peke yake, iko haki na
nguvu-----. Katika Bwana wazao wote wa Israeli watapewa haki, na kutukuka”. Tulitangulia kuona
kuwa Kristo ndiyo haki yetu. Sasa swali kubwa ni kuwa ni kwa jinsi gani haki (utakatifu) ya Kristo
unakuwa wetu? Neno la Mungu linasema ni pale tunapomwamini Yesu kama Bwana na mwokozi
wetu (soma Warumi 3:23-24). Ni wakati gani Mbingu zinapomhesabu mtu kuwa amemwamini
Yesu? Ni pale mtu anapoona utakatifu wa sheria ya Mungu kwa kuona na kutambua gharama
iliyolipwa msalabani; akaona na kutambua ubaya wa dhambi zake, akaichukia dhambi na kukusudia
kuicha kabisa moyoni, akatamani na kukubali kupokea kwa njia ya imani maisha matakatifu ya
Kristo. Hapo ndipo haki ya Kristo inapowekwa badala ya dhambi za mtu, na anahesabiwa kuwa
mtakatifu. Yaani, ni lazima tukubali kubadilishana na Bwana Yesu - sisi tumpe dhambi zetu zote, na
yeye anatupatia maisha yake matakatifu. Huku ndiko kutubu kwa kweli kutakakomfaa mdhambi. Je,
mwanadamu anaweza kulifanya hili yeye mwenyewe? La. Mungu pekee ndiye anayelianzisha ndani
ya mdhambi (soma Mathayo 5:30-31; 4:12, Waefeso 2:8-9). Kumbuka Mwanzo 3:15 na Waebrania
12:2-3. Ndipo tutakapoona upendo huu mkuu wa Mungu kwetu unatupatia amani na Mungu. Na ni
amani hii ya Kristo moyoni inaweza kutupatia furaha ya kumtii Mungu maishani. Mtu anapokuwa
amehesabiwa haki (amesamehewa dhambi) (soma Warumi 4:6-8), Mungu anafanya kitu kingine zaidi
kwa mtu huyo (soma Ezekieli 36:25-27, Yohana 3:7-8, 2 Kor. 5:17, Waebrania 8:10). Mtu anazaliwa
mara ya pili (upya) na anakuwa kiumbe kipya. Na mtu anapokuwa kiumbe kipya, ataishi maisha
mapya, siyo yale ya zamani. Maana si yeye atendaye, bali ni Kristo atendaye kazi ndani yake kwa
njia ya Roho Mtakatifu (soma Wagalatia 2:20, Yohana 15:1-5, Wafilipi 2:13, Warumi 6:17-18, 22).
Kwa hiyo mtu anaendelea kukaa katika utakaso, na Mungu mwenyewe akiwa ndiye mtendaji,
mwanadumu anadumu kuwa mpokeaji kwa njia ya imani, maana Mungu ndiye mwanzilishi na
mkamilishaji wa imani yetu (soma Waebrania 12:2). Hadi hapo bado mwanadumu hana la kujisifia,
maana matendo hayo si yake mwenyewe (soma Warumi 3:27), bali ni Roho wa Kristo aliye ndani
yake (soma Wagalatia 5:22-25).
Wengi wanaweza kufikiri kuwa tayari wamempokea Yesu kwa maana halisi inayoelezwa na
maandiko. Lakini unajua watu wa Mungu wa Kanisa la Mitume waliupindua Ulimwengu wa wakati
ule kwa injili ya milele? Je, kile kilichofanyika wakati ule, unakiona leo? Unajua kwa nini hali ile
ilikuwa tofauti na hii ya sasa? Hebu soma na kutafakari mafungu haya kwa makini. 2 Kor.5:14-15
inasema, “Maana, upendo wa Kristo watubidisha, maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja
alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; tena alikufa kwa ajili ya wote; ili walio hai wasiwe hai
tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao”.
Unakumbuka ile sheria kuu ya mbinguni? Ni Upendo usio na ubinafsi.
12
Kanisa la nyakati za mitume walipotambua upendo wa Mungu kwa ajili yao katika Kristo Yesu,
walijitoa, Walijisalimisha kwa Mungu, wao na vyote walivyokuwa navyo (soma Warumi 12:1).
Ndipo mbingu zikawamwagia roho Mtakatifu siku ya Pentekoste, ambayo matokeo yake yaliupindua
ulimwengu (soma Matendo 17:6). Waumini walipokuwa wakitoa nyumba zao, wakiuza viwanja na
vitu vingine wakavileta miguuni pa mitume, walikuwa wakionyesha upendo wa Yesu ndani yao
ulivyokuwa ukibubujika. Waliishi si kwa ajili yao wenyewe, bali kwa ajili ya yeye aliyekufa
akafufuka kwa ajili yao, yaani Yesu.
Ubinafsi ulitoka. Wakajazwa upendo wa mbinguni usio na ubinafsi. WAKAISHI KWA AJILI YA
YESU. Je, unaweza kuthibitisha kuwa pale ulipoamini, ulijitoa kwa ajili ya hilo? Yaani ulijitoa kabisa
uishi kwa ajili ya Yesu tu, si kwa faida yako mwenyewe? Je tumekuwa tayari kiasi gani kutoa mali
zetu kwa ajili ya Yesu? Vipi kuhusu muda wetu – je, unatumika kwa ajili ya Yesu, iwe kwa
kuhudhuria vipindi mbalimbali vya ibada nyumbani, kanisani au mahali pengine? Vipi kuhusu siku
yake takatifu ya Sabato? Je, saa inapofika kati ya kumtukuza Bwana Yesu na nafsi yako, humsaliti
Yesu ukamwacha na kusema utarudiana naye baadaye ukiisha timiza matakwa ya nafsi yako? Kuishi
kwa ajili ya Yesu, ni kumruhusu daima katika mambo yote atimize kusudi lake jema ndani yako(soma
Warumi 8:28). Unajua mtu anaweza kuingia kanisani, akabatizwa, akatunza Sabato pamoja na amri
nyingine zote, akatoa zaka na sadaka, akahubiri injili na kufanya mambo mengine mengi, lakini,
msukumo wa kufanya yote haya ukawa ni ubinafsi. Mara nyingi watu wa jinsi hii huhesabu yale
waliyofanya na kujilinganisha na wengine, lakini hebu jipime na Yesu Kristo peke yake ndipo
utayaona mambo kwa nuru ya mbinguni - nuru halisi. Isaya 64:6 inasema, “Kwa maana sisi sote
tumekuwa kama mtu aliye mchafu, na matendo yetu yote ya haki yamekuwa kama nguo iliyotiwa
unajisi, sisi sote twanyauka kama jani, na maovu yetu yatuondoa, kama upepo uondoavyo”. Yaani
mwanadamu anaweza kutenda matendo yanayoonekana kuwa ni ya haki lakini bado ni mwovu tu.
Dhambi imetuchafua kiasi kwamba pasipo damu ya yesu kamwe hatuwezi kuwa safi (soma
Waebrania 9:22). Dhambi imo ndani yetu na haiwezi kuondolewa kwa namna yoyote tunayoweza
kufanya (soma Warumi 7:7-10, 18). Sheria ya Mungu ya upendo, iletayo uzima, ndani yetu inaleta
mauti. Asili ya dhambi ndiyo tuliyorithi kwa baba yetu Adamu, na katika hali hiyo kamwe hatuwezi
kuwa wana wa Mungu, isipokuwa tunakubali kuingia na kuzaliwa kwa Adamu wa pili, yaani Kristo
(soma Warumi 5:17, 1 Korintho 15:45-49). Hebu fikiria, kama leo ungeamua kuacha matendo yote
maovu uliyokuwa unafanya na kuanza kutenda mema, je maovu yako yaliyopita ungeyaondoaje? Au
ukisema matendo yako mema ya sasa yatafidia yale maovu, je ungefuta kumbukumbu lake? Soma
Yeremia 2:22. Ni kwa kumpokea mwanakondoo wa Mungu tu, ndipo dhambi zetu zinaondolewa.
Kufanya vinginevyo ni sawa na kukiosha kikombe kwa nje na ndani kikabakia ni kichafu. Ni pale
kikombe kinapooshwa ndani, ndipo na nje huwa safi (soma Mathayo 23:25-26). Kutafuta kuhesabiwa
haki kwa matendo ya sheria ni unafiki na ndio maana ni machukizo kwa Bwana. Mtume Paulo
anasema, alipotambua kuwa hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele za Mungu kwa
matendo ya sheria, wao waliokuwa Wayahudi walimwamini Yesu (soma Wagalatia 2:15-16). Je,
Paulo alipomwamini Yesu hakuwa na dini au matendo mema? Hebu soma Wafilipi 3:4-7, anasema,
“Walakini mimi ningeweza kuutumaini mwili, mtu yeyote akijiona kuwa anayo sababu ya
kuutumainia mwili (yaani matendo) mimi zaidi. Nalitahiriwa siku ya nane, ni mtu wa taifa la Israeli,
wa kabila ya Benyamini, Mwebrainia wa Waebrainia, kwa habari ya kuishika torati, ni farisayo, kwa
habari ya juhudi, mwenye kuliudhi kanisa, kwa habari ya haki ipatikanayo kwa sheria sikuwa na
hatia. Lakini mambo yale yaliyokuwa faida kwangu, naliyahesabu kuwa hasara kwa ajili ya Kristo.”
Paulo anatuonyesha matendo yake mema ya kidini aliyokuwa nayo, na haya ndiyo aliona si kitu, ni
hasara tu. Fungu la 8 anasema, “Naam, zaidi ya hayo, nayahesabu mambo yote kuwa hasara kwa ajili
ya uzuri usio na kiasi kwa kumjua Kristo Yesu, Bwana wangu, ambaye kwa ajili yake nimepata
hasara ya mambo yote nikiyahesabu kuwa kama mavi ili nipate Kristo”. Mpendwa! Unaweza
kuhesabu matendo yako mema yote uliyotenda nje ya Kristo (haki kwa imani), kuwa kama mavi?
Tafakari kwa makini sana jambo hili, je utakuwa tayari kuachana na haki yako binafsi?
Unajua, wanadamu wote kwa asili tunajaribu kutenda mema ili, kwanza, Mungu atupatie nafasi
mbinguni, tukayapate mema ya huko. Pili ni ili asije akatutupa motoni siku ya mwisho HUU NDIO
UBINAFSI UNAOSEMWA. Yaani tunaamini kwa kumpokea au kumkiri Yesu kule tunakofanya ni
kama kuingia shindano la bahati nasibu. Kwa hiyo Bwana Yesu ni kama tiketi ya kuingilia shindano,
halafu kila mmoja sasa akazane mwenyewe kuepuka jehenamu na kupata mbingu kwa matendo yake.
Ndiyo maana maneno kama “imani na matendo yako ndiyo yatakuokoa” husikika miongoni mwetu.
Lakini kumbuka ndani yetu hakuna lolote jema. Na kwa sababu kujipatia haki ya Mungu kwa bidii
13
zetu wenyewe haiwezekani, (lakini ndicho wanadamu tunachojaribu kufanya, maisha ya kutaka
kumfuata Yesu yamekuwa magumu na mzigo kwetu, mwisho ni kukata tamaa, lakini kumbuka
mpendwa, “Injili ni habari njema,” yaani - KATIKA KRISTO YESU, MUNGU
AMETUPATANISHA NAYE, YAANI AMETUPATIA TOBA, AMETUSAMEHE KABISA
DHAMBI ZETU NA KUIONDOA HATIA YETU, AMETUHESABIA HAKI NA KUTUPATIA
UZIMA WA MILELE (soma Yohana 3:16-17; 2 Kor. 5:18-19). Katika Kristo Yesu mbingu zimetoa
vyote na kutupatia vyote tunavyohitaji, hakuna upungufu (soma 2 Petro 1:3-4). Tusipoamini na
kuupokea ukweli huu, kamwe hatutakuwa na amani ya Kristo mioyoni (soma Yohana 14:27; Mathayo
11:28-30. Tukiupokea ukweli huu ndipo tutamtumikia Mungu kwa furaha, kwani tunafurahia
wokovu wetu. Na kwa vile tunapomwamini yesu, ni kuwa anaingia ndani yetu nasi ndani yake, basi
matendo hayo mema hayawi yetu sisi, bali ya Kristo aliyemo ndani yetu, ndipo sifa zote na utukufu
vitamrudia Mungu, naye atatukuzwa (soma Mathayo 5:16; Yohana 15:1-8). KUMBUKA, KUSUDI
LA MAISHA LIWE KUMTUKUZA MUNGU DAIMA.
Tofauti ya Haki Hizi:
Ili kutambua tofauti kati ya Haki kwa imani na Haki kwa matendo ya sheria, mtu hana budi kutambua
asili ya jambo lenyewe. Lakini kwa maelezo machache yanayoweza kutoa mwanga kuelewa jambo
lenyewe ni kuwa:
1. Haki kwa Imani - ni kitendo cha mwadanamu kukubali kupokea kwa njia ya imani kile
ambacho Mungu amemfanyia katika Kristo Yesu, kwa ajili ya wokovu wake. Na hii
huhusisha kuhesabiwa haki (Msamaha wa dhambi), haki ya Kristo kuwa maishani
(utakaso) (au kuiishi haki ya Kristo) na mwisho kuurithi uzima wa milele (kutukuzwa
pamoja na Kristo). Yaani tangu mwanzo hadi mwisho Mungu ndiye mtendaji kupitia
kwa Kristo na mwanadamu ni mpokeaji tu (kuamini).
2. Haki kwa Matendo ya sheria - hapa ni kitendo cha mwandamu kutumainia kile
alichotenda, anachotenda sasa na atakachotenda baadaye kulingana na sheria inavyotaka
atende, ili kujiokoa. Kwa hiyo mtu mwenyewe (nafsi) ndiyo mtendaji mkuu. Ndiyo
sababu ya dhana kuwa “Mungu anasaidia wanaojisaidia”. Lakini kama unakumbuka kile
Isaya 1:6 inachosema, utagundua kuwa kwa kweli mtu hana chochote anachoweza
kujisaidia mwenyewe maana amekufa (soma Waefeso 2:5). Sasa ni maiti gani inaweza
kufanya chochote? Hakika hakuna. Ndiyo maana kamwe haki hii binafsi haiwezi
kumpatia mwanadamu wokovu, yaani atoke dhambini na kuitimiza haki ya Mungu.
Haiwezekani kwani chochote anachofanya mtu hapo ni kwa sababu ya nafsi yake na wala
si kwa ajili ya utukufu wa Mungu aliye asili ya vyote tulivyo navyo.
IMANI:
Maandiko matakatifu yanasema “Imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya
mambo yasiyoonekana,” (Waebrania 11:1). “Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza, kwa
maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu
wale wamtafutao,” (Waebrania 11:6).
Lakini imani ni nini pia. Ni mkono (Kiroho) wa mwanadamu wa kupokelea ahadi za Mungu. Yaani
ni kwa njia ya imani tu mwanadamu anaweza kupokea ahadi za Mungu kwake. Hivyo isieleweke
kuwa imani ndiyo mwokozi. La, bali ni njia yetu kuupokea. Na pia hiyo(imani) haitokani na sisi
wenyewe, bali ni kipawa cha Mungu (soma Waefeso 2:8-9, Waebrania 12:2). Imani ni msingi wa
maisha ya kumcha Mungu, maana amesema pasipo hiyo haiwezekani kumpendeza. Ndiyo maana
matendo ya haki tunayoweza kutenda, pasipo imani, bado ni machukizo tu. Yatakuwa hayajatimiza
ile kanuni ya mbinguni ya “Upendo usio na Ubinafsi:” Imani ni kumwamini Mungu kabisa kwa kila
jambo na kumtegemea yeye tu. Tunaweza kusema kuamini ni KUJISALIMISHA KWA MUNGU.
Mtu unapojisalimisha, huwa hakuna unachobakiza. Unajitoa kabisa kwa yule unayejisalimisha kwake
ili akutendee apendavyo. Ni hakika tunahitaji kujisalimisha kwa Mungu ili atutendee kama
apendavyo. Na tunafanya hivyo kwa kujua wazi kile anachotaka kutufanyia kwa kuwa yeye ni
14
mwaminifu, tofauti na ambavyo unaweza kufanya kwa mwanadamu anayebadilika-badilika. Imani
kwa Mungu ni jambo la hakika (soma Waebrania 11:1), sio bahati nasibu. Kwa kweli wanadamu
wengi sana tuna kitu kama bahati nasibu katika Ukristo wetu, wala hatuna hakika (imani) na Mungu.
Yaani tunafanya majaribio. Tukipata, bahati nzuri, tukipoteza au kukosa, bahati mbaya. Ukitaka
kuhakikisha ukweli huu, hebu jaribu kutafakari maombi yako mwenyewe na kile moyo wako ulicho
na uhakika nacho. Kwa mfano, unapoomba, ukaungama dhambi zako zote, na kueleza mengine
unayoyahitaji kwa Mungu, halafu unasema kwa jina la Yesu, Amina. Je moyoni mwako unaamini
(una hakika) kuwa ndivyo Mungu alivyofanya au atakavyofanya? Yaani Je, unaamini kuwa Mungu
amekusamehe kabisa dhambi zako na sasa anakuhesabu kuwa mwenye haki (mtakatifu) na kuwa sasa
hivi au saa hiyo hiyo tayari amekupatia uzima wa milele? Je, tunafanya maombi ili Bwana atutendee
mambo fulani, halafu mengine tutakamilisha wenyewe? Sasa kwa sababu hatuna hakika kuwa kwa
upande wetu tutafanya bila kukosea, basi hata Mungu tuna mashaka naye kama kweli atatenda kama
alivyoahidi. Ndiyo maana, kwa kweli, wengi wetu hatuna imani kwa Mungu wetu kwa kipimo cha
mbinguni. Tafakari swali la Bwana Yesu “---- Walakini, atakapokuja mwana wa Adamu, je! Ataiona
imani duniani,” ( Luka 18:8)? Bwana Yesu hakuwa anazungumzia dhana ya imani ambayo ndiyo
tuliyonayo watu wengi, lakini alikuwa akisema juu ya imani ya kweli ya Mungu (Haki kwa imani);
imani ya Yesu (soma Ufunuo 14:12). Hii humpatia mpokeaji imani ya kweli moyoni - amani na
Mungu.
Wapendwa, Shetani anachocheza nacho maishani mwetu ni imani zetu. Maana hutuletea udhaifu
wetu na dhambi zetu tulizozitenda mbele yetu na kutushawishi kuwa Mungu hawezi kabisa
kumkubali mtu mwovu. Hivyo unafuata ushauri wake mwingine kuwa, bora uendelee tu na maisha
hayo ya dhambi, na hivyo Mungu anadumu kuwa adui yetu. Na kama Shetani atashindwa kutufanya
tusimwamini kuwa Mungu atatupokea wadhambi, ataleta fundisho jingine, nalo ni la kujitahidi
kuokolewa kwa matendo ya sheria. Anasema Mungu hafanyi kila kitu, sasa kazana kwa matendo
matakatifu ili Mungu akupe maksi na uwe mshindi. Sasa tahadhari ni hii, katika hili la pili anafaulu
sana, maana inaonekana kana kwamba ni ukweli, naye anakuja kama malaika wa nuru (soma 2
Korintho 11:13-15). Lakini kumbuka neno la Mungu linasema, “kwa sababu hakuna mwenye mwili
atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria ----” (Warumi 3:20. Soma pia Wagalatia
2:16). Shetani akiishafaulu kuyumbisha imani yetu, matunda tutakayozaa daima yatakuwa najisi,
yasiyokubalika mbele za Mungu, yamechafuliwa na ubinafsi.
Lakini jambo tunalopaswa kufahamu ni kuwa imani sio swala lililo na mpaka kwamba watu wa kundi
fulani au dhehebu fulani ndio wenye imani ya kweli au imani bandia, hili ni swala la moyo wa mtu
kuhusu kile anachoruhusu akipokee.
Nataka niweke neno hili wazi kwamba msingi wa mafundisho ya imani zote duniani - zile za
madhehebu mengine na dini nyingine ni haki kwa matendo ya sheria. Ni msingi wa mafundisho ya
neno la Mungu kama lilivyofunuliwa kwa kanisa lake la Masalio (soma Ufunuo 12:17) ndiyo
unaofunua ukweli wa haki kwa imani. Lakini jambo moja la kusikitisha ni kuwa, mafundisho au
ukweli huu umechafuliwa na Shetani, na sasa wengi sana tunafahamu kuwa wokovu wetu
unategemea matendo yetu ya sheria. Mafundisho mengi tunayotoa yemejengwa katika mtazamo huo,
na ndio maana tumekuwa watumwa wa haki hii – binafsi - ambayo tunagundua kwamba ni mzigo
mkubwa, tusioweza kubeba. Kumbuka maneno ya Bwana Yesu katika Mathayo 23:4, “Wao hufunga
mizigo mizito na kuwatwika watu mabegaani mwao; wasitake wenyewe kuigusa kwa kidole chao.”
Sasa kwa sababu ya kuwa na mafundisho hayo bandia, wengi sana wamejitenga na Mungu mioyoni.
Lakini, kwa upendo, anataka kuondoa mafundisho hayo potofu, na njia pekee anayoitumia ni haki ya
Kristo ambayo ni haki ya Mungu ipatikanayo kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Kila mmoja
wetu na afanye uamuzi kuchagua ni upande gani atakayosimama.
Wako wengi ambao hawatakubali kuifukuza haki yao binafsi iliyo ya sheria ili kuipokea haki ya
Kristo kwa imani; watajitenga na Kanisa la Mungu kabisa na kuwa maadui wakuu wa ile kweli ya
Kristo Yesu.
15
Tunapohitimisha sehemu hii inayohusu imani, hebu tukumbuke na kufahamu kwamba “Imani ni
kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Kuamini ni
kujisalimisha kwa Mungu kulingana na alivyojifunua katika neno lake (Upendo). Maana roho
Mtakatifu huanzisha imani ndani yetu kwa njia ya neno la Mungu - Injili - (soma Warumi 10:17).
Mpendwa mwombaji, hebu tutafakari kwa makini ujumbe huu tunaoendelea kujifunza. Hebu
tutathmini imani zetu kwa nuru ya neno la Mungu ili isije kuwa tunapiga mbio bure (soma 1 Korintho
9:26, 2 Kor. 13:5).
IMANI NI ITIKIO LA SHUKRANI LA MOYO WA UPENDO KWA MUNGU KWA
UPENDO WAKE ALIOUONYESHA KWETU PALE MSALABANI. NI KUMPENDA
MUNGU KWA VYOTE BILA KUBAKIZA CHOCHOTE
KAFARA YA YESU:
Mara nyingi ni rahisi kwetu kuiangalia kafara ya Kristo kwa tukio la msalabani tu, yaani Kalvari.
Lakini hebu tutafakari maneno ya Wafilipi 2:5-8, “kuweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo
ilikuwemo pia ndani ya Kristo Yesu; ambaye yeye mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, naye
hakuona kule kuwa sawa na Mungu kuwa ni kitu cha kushikamana nacho; bali alijifanya kuwa hana
utukufu, akatwaa namna ya mtumwa, akawa ana mfano wa wanadamu; tena alipoonekana anaumbo
kama mwanadamu, alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti, naam, mauti ya msalaba” Maneno haya
yanatupatia sura halisi ya kile ambacho dhambi ilikisababisha kwa Uungu.
Bwana Yesu, ambaye neno la Mungu linasema ni Mungu, yaani ni mmoja wa nafsi za Uungu,
alifanyika mwili, yaani alitwaa ubinadamu (soma Yohana 1:14,18). Jambo hili kwa kweli ni zaidi ya
akili zetu kulipima na kulielewa jinsi lilivyofanyika. Mungu kutwaa ubinadamu, akazaliwa kama
mtoto mchanga wa kibinadamu! Ajabu kwa akili zetu za kibinadamu. Soma Mathayo 1:18-23, Luka
1:26-37; 2:4-14. Kwa hiyo tunaweza kuona ukuu wa kafara ya Bwana Yesu kwa kutambua kuwa
yeye ni Mungu, lakini “hakuona kule kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho” (Wafilipi
2:6b). Isije ikafikiriwa kuwa kwa kufanya hivyo Yesu aliudharau Uungu wake. La, bali inaonyesha
ni kwa kiasi gani mwanadamu ni wa thamani mbele za Mungu. Na kama mwanadamu yeyote
atafanya dharau kwa Bwana kwa kufikiria hivyo atakuwa anafanya kosa kubwa sana. Kwa hiyo
muumbaji aliyemuumba mwanadamu, akajishusha ili kutuokoa. Kwa hiyo tangu nia ilipokuwamo
ndani yake na akajitoa ili atuokoe, tayari kile kilichofanyika msalabani kilikuwa kimeanza - Yaani
Mateso.
Ubinadamu wa Yesu:
Unajua, tatizo letu kuu wanadamu ni kutoamini, yaani kutomwamini Mungu. Na unajua hili ndilo
lilikuwa hasa jaribu la shetani kwa Hawa, na ndio msingi wa majaribu yake yote kwetu. Sasa kwa
sababu hiyo, hata kile ambacho Mungu amesema katika neno lake, ni vigumu sana kukiamini; na
mojawapo ni kuhusu Ubinadamu wa Yesu. Wengi wetu tumeendelea kuamini kuwa Bwana Yesu
hakutwaa mwili hasa, yaani hakuwa mwanadamu kama sisi, na kwa jinsi hiyo hata kile alichofanya
katika hali yake ya ubinadamu hakina uzito sana maana inaonekana kana kwamba ni kiini macho tu.
Hebu tuone neno la Mungu linavyosema. Labda, kwa kuanzia, tuone kile Isaya anachosema (Isaya
9:6). “Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto mwanamume: Na uwezo wa kifalme
utakuwa begani mwake; naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa
Milele, Mfalme wa amani”. Kama nilivyotangulia kusema, mtu yeyote anayefanya dharau juu ya
ubinadamu wa Bwana Yesu anafanya dhambi kubwa. Unapotafakari maneno ya fungu hilo
yanaonyesha wazi kuwa, ijapokuwa mtoto huyu anayezaliwa ni mwanadamu, tena mwanamume,
lakini bado anaitwa, Mshauri, Mungu, Baba na Mfalme! Cheo chake cha uungu kiko palepale. Sasa,
kuna watu ambao wanamchukulia Bwana Yesu kama wao wenyewe, (sisemi kama mwanadamu, bali
kama wao wenyewe) yaani, kile wanachofikiri, kusema au kutenda, ndivyo wanavyomfanya Kristo
awe. Lakini hili ni kosa. Ijapokuwa alitwaa ubinadamu, lakini aliishi maisha tofauti na sisi katika
16
kufikiri kwake, kusema kwake na kutenda kwake. Je, hii haionyeshi kuwa lazima angeishi tofauti na
sisi maana yeye ni Mungu? La, yeye mwenyewe alisema “Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe
ila lile ambalo amwona Baba analitenda ----” (Yohana 5:19). “Mimi siwezi kufanya neno mwenyewe
----” (Yohana 5:30), “kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali
mapenzi yake aliyenipeleka” (Yohana 6:38). Ndio maana, kama mwanadamu yeyote, alihitaji
msaada wa Mungu. Ndio maana alijazwa Roho Mtakatifu, na Roho ndiye akawa kiongozi wake
(soma Mathayo 3:16, 4:1). Tofauti ya ubinadamu wake iliyo wazi ni kuwa - daima siku zote, Yesu
alitii uongozi wa roho Mtakatifu - alifanya mapezi ya Mungu (soma Yohana 8:28-29). Hakutenda
dhambi (soma Waebrania 4:15) na hakuwa na uadui na Mungu. Ndani yake asili mbili ziliunganika.
Jambo la msingi kufahamu ni kuwa ili ukombozi wetu ufanyike, ilikuwa lazima Yesu kutwaa
ubinadamu. Kwani, kama vile Mungu alivyoumba wanadamu wote katika au ndani ya Adamu (soma
Matendo 17:26), Vivyo hivyo katika mpango wa ukombozi alituunganisha sote (ubinadamu wote)
ndani ya Kristo (soma Waefeso 2:16). Kwa hiyo tendo la Bwana Yesu kufanyika mwili, ni
kuunganisha wanadamu wote ndani ya uungu, na ndio “Imanueli” yaani “Mungu pamoja nasi”
(Mathayo 1:23). Ni kwa kutambua na kulipokea neno moyoni, ndipo kafara ya Kristo inapoleta sura
halisi katika ufahamu wetu, maana kufanyika kwake mwanadamu kumetufungamanisha naye kama
ndugu yetu (soma Waebrania 2:11). Kristo hakufanya badala yetu, bali kwa ajili yetu. Ndiyo maana
hakuna chochote tunachoweza kufanya nje ya Kristo kwa ajili ya wokovu wetu, maana nje yake,
tunakuwa katika utu wetu wa kale ambao hauwezi kumtii Mungu (soma Waruni 7:14, 1 Kor. 2:14).
Lazima Kristo awe ndani yetu nasi ndani yake kwa imani.
Muhimu: Kwa sababu haikuwezekana kabisa katika hali yetu ya dhambi kuitenda na kuitimiza
haki ya Mungu, ndiyo maana kristo alitwaa mwili ili katika Yesu yote yawezekane.
Warumi 8:3-4 inasema, “Maana yale yasiyowezekana kwa sheria, kwa vile
ilivyokuwa dhaifu kwa sababu ya mwili, Mungu , kwa kumtuma Mwanawe
mwenyewe katika mfano wa mwili ulio wa dhambi, na kwa sababu ya dhambi,
aliihukumu dhambi katika mwili, ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi,
tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho.” Kwa hiyo
ubinadamu wa Yesu umefanya iwezekane kwetu wanadamu kutimiza mapenzi ya
Mungu katika Kristo. Hapo nyuma tuliona kuwa kristo Yesu amefanya yote
yaliyopaswa kwa ajili yetu na si badala yetu. Ndiyo maana, kumpokea au
kumwamini yeye, ni kujisalimisha kwake ili atimize kusudi lake ndani yetu (soma
Wafilipi 2:13). Kwa hiyo yale tunayoweza kutenda tunapoamini, hayatakuwa yetu
sisi, bali ni Kristo atakayekuwa akitenda ndani yetu (soma Yohana 15:1-5). Hivyo
kujisifia matendo hayo ni kutwaa utukufu wa Mungu, maana pasipo yeye sisi
hatuwezi kufanya neno lolote. Kumpokea Yesu moyoni ni kufanya awe Mungu
(mtawala) wa maisha badala ya nafsi kuwa Mungu.
Kuzaliwa: Malaika akasema “maana leo katika mji wa Daudi, amezaliwa, kwa ajili
yenu, Mwokozi, ndiye kristo Bwana” (Luka 2:11). Ni kwa ajili yetu, Kristo alitwaa
mwili au ubinadamu, hivyo akazaliwa. Hivyo kuukubali ubinadamu wa Yesu ni
kuonyesha imani kwake kuwa - Uungu uliungana na ubinadamu,na hivyo kupokea
yote aliyofanya kwa ajili yetu. Kutoamini jambo hili ni kumkataa Kristo, na yote
aliyofanya hayatakuwa na faida yoyote kwa mhusika (soma 1 Yohana 4:2.3. Hapa,
katika kuzaliwa kwake ni mwanzo wa maisha yake hapa Duniani. Kupokea kwa
imani mwanzo huu ni kufungua moyo kupokea huduma yake ya maisha yake yote
yaliokuwa kwa ajili yetu.
Ubatizo: Kabla ya Bwana yesu kuanza kazi rasmi hapa duniani alibatizwa. Biblia inatuonyesha
kuwa Yesu hakuwa na dhambi (soma 1 Petro 2:22). Lakini Yohana mbatizaji
alikuwa akifanya ubatizo wa toba (soma Mathayo 3:6). Sasa kwa nini Yesu
alibatizwa kama hakutenda dhambi? Jibu alilolitoa yeye mwenyewe kwa Yohana ni
kuwa “kubali hivi sasa, kwa kuwa ndiyo itupasavyo kuitimiza haki yote” (Mathayo
3:15). Kwa kuliweka wazi jambo hili ni kuwa, kwa sababu Mungu aliwahesabu watu
kuwa ndani ya Kristo, hivyo dhambi zetu zilikuwa ndani yake. Hivyo alifanya toba
na kubatizwa kwa ajili ya dhambi zetu zilizokuwa ndani yake, yaani alizozibeba
(alitubeba ndani yake) (soma 2 Kor. 5:21, Isaya 53:6). Kwa jinsi hiyo ubatizo
tunaobatizwa una maana sana kuonyesha imani yetu kwa Yesu. Ndiyo maana,
17
kufanya kitu kingine kinyume na kile alichofanya Bwana, ni kumkataa yeye kama
haki yetu na tunajipatia haki yetu wenyewe, isiyo ya Mungu. Maandiko Matakatifu
yanasema hakuna wokovu katika mwingine awaye yote isipokuwa Kristo tu (soma
Matendo 4:12). Na kama tumeamini, ambako ni kujisalimisha kwake ili yeye atende
ndani yetu apendavyo, hakika atatuongoza kubatizwa kama yeye alivyofanya ili ile
haki ikamilike ndani yetu. Kufanya kitu kinyume, kama ubatizo, tofauti na ule wa
Yesu, ni sawa na sadaka aliyotoa Kaini ambayo haikuonyesha imani kwa Masihi
ajaye. Ni kutoamini. Ni kwa njia ya ubatizo (kuzamishwa majini) tunapoonyesha pia
kukubali mauti ya Kristo kwa ajili yetu, maana ubatizo ni kama ishara ya kuzikwa
naye, na kukubali kuifia dhambi pamoja naye; na mtu hazikwi kabla hajafa. Ni wazi
kuwa hii ni ishara ya kuonyesha imani yetu katika mauti yake (soma Warumi 6:2-5).
Ni haki kwa imani.
Maisha Aliyoishi:
Kama mwanadamu neno la Mungu linasema hivi kumhusu Kristo “---- bali yeye alijaribiwa
sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi” (Waebrania 4:15). Majaribu yote
yanayotupata, Bwana Yesu aliyapitia na akayashinda. Warumi 8.3 linasema, “---- na kwa sababu ya
dhambi aliihukumu dhambi katika mwili”. Yaani katika mwili ulio kama wako na wangu, Kristo
aliihukumu dhambi - maana yake aliishinda dhambi.
Yohana 8:29, “----kwa sababu nafanya siku zote yale yampendezayo”.
Yohana 15:10, “Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu, kama vile mimi
nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake”
Yohana 8:45, “Ni nani miongoni mwenu anishuhudiaye kuwa nina dhambi”?
Kwa hiyo, maisha Kristo Yesu aliyoishi ya mwanadamu hapa duniani yalikuwa maisha ya utii kamili
kwa sheria za Mungu, ndiyo maana hakutenda dhambi. Na kwa sababu aliitii sheria kwa ukamilifu,
maandiko yanasema, “Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria ili kila aaminiye ahesabiwa haki”
(Warumi 10:4). Wengi wamelitafsiri fungu hili kumaanisha kuwa Kristo sasa ameondoa sheria na
hivyo hatupaswi kuzitii au kuzitenda. Lakini Bwana Yesu mwenyewe alisema “Msidhani ya kuwa
nalikuja kutangua torati au manabii, la, sikuja kutangua, bali kutimiliza” (Mathayo 5:17,19). Kwa
hiyo, maana ya Kristo kuwa mwisho wa sheria ni kuwa - yeye alitii sheria takatifu ya Mungu kwa
ukamilifu na hivyo sheria hiyo haimhukumu kuwa mkosaji. Sheria hiyo takatifu imeridhika kuwa
matakwa yake yametimizwa. Hivyo yeyote anayemwamini Yesu, yaani anayempokea Yesu moyoni,
hupewa uwezo wa kuzitii sheria za Mungu kwa ukamilifu - maana Kristo aliye ndani ya muumini
huyo huzitii sheria ndani yake na hivyo anasimama mbele za Mungu kama mtu mtakatifu, yaani
sheria haitamhukumu kuwa ameivunja. Kumbuka, si haki ya mtu binafsi, bali ni ya Kristo aliye ndani
yake (soma Rum. 8:1).
Mauti ya Msalaba:
Katika kitabu cha Wafilipi 2:8 tunasoma, “tena alipoonekana ana umbo kama mwadanamu,
alijinyenyekeza akawa mtii hata mauti naam, mauti ya msalaba”.
• Waebrania 2:14 inasema, “Basi kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo
hivyo alishiriki yayo hayo ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti,
yaani Ibilisi”.
• Kwa nini mauti ilikuwa lazima kwa ajili ya ukombozi wetu? Ni kwa sababu ndiyo njia ambayo
kwayo Ibilisi angeharibiwa na nguvu zake. Kumbuka mwanzo 3:15 Kumponda kichwa yule
nyoka wa zamani. Ufunuo 12:11 “ Nao wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo na kwa neno la
ushuhuda wao ----“.
18
• katika maisha yake hapa duniani, daima Yesu Kristo alikabiliwa na vita vile vilivyoanzia kule
mbinguni. Ndani yake kulikuwa na mashindano makuu - atende kama mapenzi ya Baba yake
yalivyotaka ili mwanadamu aokolewe, au atende kama nafsi yake ilivyotaka ili ajiokoe mwenyewe
na mwanadamu apotee milele. Waebrania 12:2 linasema, “tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha
na kutimiza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake, aliustahimili msalaba
na kuidharau aibu----.”
• Pale bustani ya Gethsemani Yesu aliomba kuwa “ikiwezekana kikombe hiki kiniepuke, walakini si
kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe” (Mathayo 26:39). Alipokuwa mbele ya Pilato
alisema “----Mimi nimezaliwa kwa ajili ya haya, na kwa ajili ya haya mimi nalikuja ulimwenguni
ili niishuhudie kweli----” (Yohana 18:37).
Mungu ashukuriwe. Kristo alistahimili msalaba, naam mauti ya msalaba. Pale msalabani Kristo
aliposubiliwa, Shetani alitoa matukano makuu kupitia kwa makutano waliokuwa pale ili ikiwezekana
Kristo ashuke msalabani na mwanadamu apotee milele - asiokolewe. Hebu soma jinsi ilivyokuwa
(Mathayo 27:40-44), “Ewe mwenye kulivunja hekalu na kulijenga kwa siku tatu, jiokoe nafsi yako;
ukiwa ndiwe mwana wa Mungu, shuka msalabani. Kadhalika na wale wakuu wa makuhani
wakamdhihaki pamoja na waandishi na wazee, wakisema, aliokoa wengine, hawezi kujiokoa
mwenyewe. Yeye ni mfalme wa Israeli; na ashuke sasa msalabani, nasi tutamwamini.
Amemtegemea Mungu; na amwokoe sasa, kama anamtaka, kwa maana alisema, mimi ni mwana wa
Mungu. Pia wale wanyang’anyi waliosulibiwa pamoja naye walimshutumu vile vile.” Maneno haya
makuu yakasemwa na wanadamu ambao ndio Kristo alikuja kuwaokoa!! Tusije tukawalaumu
Wayahudi hawa waliofanya hayo tukifikiri sisi ni wema kuliko wao. Kama wewe au mimi
tungekuwepo pale, yawezekana kabisa tungeshiriki kusema maneno hayo. Halafu pia, jambo la
muhimu kutambua na kukumbuka ni kuwa Bwana Yesu alikufa, si kwa ajili ya watu fulani tu, bali ni
kwa dhambi za ulimwengu wote. Dhambi zetu ndizo zilimsulibisha na kumuua (soma Isaya 53).
Maneno yaliyopigiwa msitari katika fungu hapo juu yanaonyesha vita kuu ambayo kila mwanadamu
amekuwa nayo na atakuwa nayo hadi mwisho.
Navyo ni vita dhidi ya nafsi. Unajua kama Yesu angeokoa nafsi yake, sisi sote tungepotea milele!!
Kama Mungu angemwokoa mwanawe pale msalabani asife, wewe na mimi ndio tungekufa kifo kile.
Lakini kwa Upendo mkuu usio na kifani, Mungu Baba akakaa kimya na mwana wake, Yesu, akafa
(soma Mathayo 27:46), ili wewe na mimi tuokolewe na kuurithi uzima wa milele. Kwa upendo huo
mkuu Kristo naye hakushuka msalabani kama shetani alivyotaka kupitia kwa wale makutano (soma
Warumi 5:6-8). Pamoja na yote hayo aliyofanyiwa, sikiliza alichosema Yesu; “Baba uwasamehe,
kwa kuwa hawajui watendalo----” (Luka 23:34). Upendo ulioje!!! Mwisho, Kristo alikufa msalabani
(soma Mathayo 27:50-54). Bwana Yesu hakuendelea kubaki kaburini. Siku ya tatu alifufuka (soma
Mathayo 28:1-6, Marko 16:1-6, Luka 24:1-6). Je, unajua Yesu Kristo amekufa msalabani ili tusije
tukafa mauti ya pili au ya milele katika jehanamu ya moto? Ni nini kitakuzuia usimpokee Yesu kuwa
Bwana na mwokozi wa maisha yako? Yeye alisema “aaminiye na kubatizwa ataokoka, asiyeamini,
atahukumiwa” (Marko 16:16).
Kwa nini, basi, kuna dini au imani zinazofundisha kuwa Yesu Kristo si mwokozi na pia hakufa
msalabani? Jibu ni kuwa, ni kwa sababu yule adui, yaani Shetani aliamua kuwapoteza wanadamu
kupitia jina la dini. Kumbuka alipomdanganya Hawa hakumwendea moja kwa moja kama Shetani,
alimtumia nyoka na Hawa akadanganyika. Kama angewashawishi wanadamu kumkataa Mungu
kabisa, angegundulika kwa urahisi lakini sasa yeye hujifanya malaika wa nuru ili kunasa wanadamu
(soma 2 Wakorinto 11:13-15). Bwana Yesu ndiye ambaye Shetani anamchukia, lakini pia yeye Yesu
ndiye mwokozi. Hivyo Shetani atampinga kwa njia yoyote ile ili mpango wa Mungu usitumie.
Lakini Mungu ashukuriwe - Yesu ameshinda. Mpendwa msomaji, je, utamruhusu Kristo awe Bwana
na mwokozi wako, au nafsi yako mwenyewe? Kumbuka, Mungu asipotutawala na tukafanya
mapenzi yake, nafsi ndiyo itakuwa mungu kwetu na tutatenda kulingana na nafsi itakavyotuongoza.
Lakini kumbuka kuwa daima nafsi ina uadui na Mungu ndiyo maana ili kumfuata Yesu, lazima nafsi
isulibiwe (soma Luka 9:23-25, 14;26-27.
19
HUDUMA YA PATAKATIFU
Miongoni mwa huduma ya lazima kwa wokovu wa wanadamu, lakini ambayo watu wengi, sana sana
hawaijui, ni hii ya Patakatifu. Yawezekana wewe u mmoja wao. Kwa hiyo, kabla hatujafika mwisho
wa masomo haya, napenda kukupa fursa hii ili upate kuifahamu huduma hii muhimu.
Katika kitabu cha Kutoka 25:8 tunasoma jinsi Mungu alivyomwambia Musa, “Nao na wanifanyie
Patakatifu ili nipate kukaa kati yao.” Hivyo kwa kuitikia agizo hili, mahali palijengwa yaani
Patakatifu au Hema ya kukutania au Hekalu (soma Kutoka 29:43-46, 40:1-11,7-38). Patakatifu
palikuwa na vyumba viwili kwa ndani, nje kulikuwa na madhabahu ya Sadaka ya kuteketezwa na
birika la kunawia makuhani, na ua uliovizingira vitu hivi vyote wa nguo ya kitani nzuri ya kusokotwa
(soma kutoka 38:9). Patakatifu au hema hii ilikuwa na chumba cha kwanza kilichoitwa “Patakatifu”
na chumba cha pili cha ndani kilichoitwa “Patakatifu pa Patakatifu”. Katika chumba hiki cha kwanza
cha “Patakatifu” kulikuwa na kinara cha taa, meza ya mikate ya wonyesho na madhabahu ya
kufukizia uvumba. Katika chumba cha pili yaani Patakatifu pa Patakatifu kulikuwa na Sanduku la
Agano na juu yake Kiti cha Rehema kikifunikwa na Makerubi. Kando ya sanduku kulikuwa na fimbo
ya Haruni iliyochipuka. Ndani ya Sanduku la Agano kulikuwa na mbao mbili zilizoandikwa amri
kumi za Mungu pamoja na mana. Vitu vyote hivi vilimwakilisha kristo na huduma yake ya
ukombozi. Mtu alipotenda dhambi, alikwenda na mnyama pale hemani kwa ajili ya huduma ya
upatanisho. Alipokuwa amefika kwa Kuhani (yaani mhudumu wa Patakatifu) pale madhabahuni (nje
ya hema) mdhambi aliweka mikono kichwani pa mnyama na kuungama dhambi zake. Baada ya
kuungama, yeye mwenyewe alimchinja mnyama yule na mnyama yule alitolewa pale madhabahuni
na kuteketezwa kuwa kafara kwa Bwana. Kwa imani dhambi ilihama toka kwa mdhambi na kuwa
juu ya mnyama aliyeuawa kwa ajili yake. Mtu huyu alirudi nyumbani akiwa huru. Lakini baadhi ya
damu ya mnyama ilichukuliwa na kuhani hadi chumba cha patakatifu na kunyunyizia katika pazia
lililotenga chumba cha patakatifu na kile cha Patakatifu pa Patakatifu, na kwa njia hiyo ile dhambi
ilipelekwa mbele za Mungu kwa ajili ya hukumu. Yaani dhambi ile lazima ipate kutengwa kabisa na
mtu aliyetubu. Pia kulikuwa na kafara maalum ya kutoa wanakondoo wawili mmoja asubuhi na
mmoja jioni. Huduma hizi zilifanyika kila siku isipokuwa siku moja tu kwa mwaka. Ndani ya hema
yaani katika chumba cha kwanza cha Patakatifu kulikuwa na huduma iliyofanyika kila siku, huduma
iliyokuwa ya kufukiza uvumba (soma Kutoka 29:38-42; Walawi 1:1-9, 4:1-12).
Mara moja kila mwaka, ilifanyika huduma iliyohusisha chumba cha pili cha hema yaani Patakatifu pa
Patakatifu. Huduma hii ilifanyika mara moja tu kwa mwaka ili kutakasa hema (Patakatifu) na watu
pia. Siku hiyo iliitwa siku ya upatanisho. Huduma hii ilifanywa na kuhani mkuu tu. Katika siku hiyo
kuhani alitoa ng’ombe kwa sadaka yake mwenyewe kufanya upanisho wa nafsi yake, ndipo afanye
huduma ya upatanisho kwa ajili ya watu. Huduma hii ndiyo iliyoondoa dhambi zote za wana wa
Israeli walizozitenda kwa mwaka mzima mbele za Bwana. Huduma hiyo ilihusisha mbuzi wawili –
mmoja kwa Bwana na wa pili wa Azazeli. Ni huduma ambayo kila mtu alipaswa kushiriki kwa njia
ya kujitaabisha roho yake (yaani kujihoji na kutubu dhambi yoyote aliyokuwa nayo ili apatanishwe na
Mungu). Kama mtu yeyote asingefanya hivyo, basi siku hiyo hiyo angekatiliwa mbali na watu wa
Mungu mara kuhani mkuu anapomaliza huduma ya siku ile (soma Walawi 16:1-34, 23:26-32,
Waebrania 9:1-10). Unaweza kujiuliza swali - kwani huduma hiyo inahusianaje na wokovu wetu?
Neno la Mungu linaonyesha kile kilichotokea siku ile Bwana Yesu alipokata roho pale msalabani -
“Na tazama, pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini----” (Mathayo 27:51).
Pazia hili ni lile lililokuwa linatenganisha vile vyumba viwili vya hekalu, yaani Patakatifu na
Patakatifu pa Patakatifu, na hii ilikuwa ishara kuwa huduma yote iliyofanyika hekaluni ili
kumpatanisha mdhambi ilikuwa imekoma hapa dunuani. Hakuna tena mwanadamu yeyote
anayeweza kufanya huduma hiyo na ikakubalika maana atakuwa anapingana na Mungu, na mtu
yeyote anayekwenda kwa kiongozi wa dini ili akaungame dhambi zake, pia atakuwa anapingana na
Mungu na huduma hiyo inakuwa ya bure tu (soma Mathayo 15:8-9). Sasa kama huduma ile ilikoma,
je mdhambi afanyeje sasa? Endelea kujifunza.
20
Biblia inasema, “---tunaye Kuhani Mkuu wa namna hii, aliyeketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi
cha ukuu mbinguni, mhudumu wa patakatifu, na wa ile hema ya kweli, ambayo Bwana aliiweka wala
si mwanadamu. “-----watumikao mfano na kivuli cha mambo ya mbinguni, kama Musa alivyoagizwa
na Mungu, alipokuwa tayari kuifanya ile hema; maana asema, Angalia ukavifanye vitu vyote kwa
mfano ule ulioonyeshwa katika mlima” (Waebrania 8:1-5). “Basi ilikuwa sharti nakala za mambo
yaliyo mbinguni zisafishwe kwa hizo, lakini mambo ya mbinguni yenyewe yasafishwe kwa dhabihu
zilizo bora kuliko hizo” (Waebrania 9:23).
Ni wazi kuwa Patakatifu pa duniani na huduma zake ilikuwa ni nakala au mfano wa Patakatifu na
huduma za mbinguni. Sasa elewa nakala hizi kwa ukaribu au uwazi zaidi:
• Mnyama kwa sadaka ya kuteketezwa ya dhambi ilimwakilisha kristo kama kafara kwa
dhambi zetu (soma Yohana 1:29, Waebrania 9:13-14)
• Kuhani (mhudumu wa Patakatifu) alimwakilisha Yesu kama Kuhani wetu mkuu (soma
Waebrania 8:1-2, 4:14-15).
• Kinara cha taa kilimwakilisha Yesu kama nuru halisi (soma Yohana 1:9-14, 3:19, 9:5).
• Mikate ya wonyesho iliwakilisha jinsi mwanadamu anavyopata chakula chake kwa
Mungu (cha kimwili na cha Kiroho) kwanjia ya Kristo (soma Yohana 6:31-33).
• Madhabahu ya kufukizia uvumba iliwakilisha huduma ya Yesu ya kutuombea (soma
Waebrania 7:25, 1Yohana 2:1).
• Sanduku la agano (Amri Kumi) iliwakilisha tabia takatifu ya Mungu na kanuni pekee
ambazo wanadamu wanapaswa kuzitii. Utakatifu huo ndiyo “haki ya Kristo” (soma
Kutoka 19:5-6, Ezekieli 20:11-12).
• Kiti cha Rehema ni mahali ambapo utukufu wa Mungu (Shekina) ulionekana juu ya
lile Sanduku la Agano. Hii inaonyesha kuwa enzi yake Mungu wetu imejengwa katika
sheria zake ambazo ndio tabia yake (soma Lawi. 11:44, Zaburi 45:6-7). Ni mfano wa
kiti cha enzi cha mbinguni.
• Mbuzi wa Sadaka ya dhambi kwa ajili ya bwana (siku ya upatanisho) alimwakilisha
Kristo kama kafara ya Bwana kwa dhambi.
Mbuziw a Azazeli (siku ya upatinisho) alimwakilishNa i Skhuewtaan i. k uhani
mkuu alipokuwa amekwishamtoa ng’ombe wa sadaka ya dhambi kwa ajili ya nafsi
yake na kufanya huduma zilizofuata, alikuwa akitoa pia mbuzi aliyekuwa sadaka ya
dhambi kwa ajili ya upatanisho wa Patakatifu, kwa sababu ya makosa ya Walsraeli,
na mambo yao machafu, na kwa ajili ya hema ya kukutania. Na baada ya huduma hii
ambayo ilihusisha kunyunyiza baadhi ya damu ya yule ngombe na mbuzi; juu ya kiti
cha rehema machafu yote ya wana wa Israeli yaliitoka madhabahu na Patakatifu
(hema) (soma Walawi 16:14-19). Baada ya huduma hiyo, alifanya huduma nyingine
kwa mbuzi wa pili (wa Azazeli), ambayo ilikuwa ni kuweka mikono yake juu ya
mbuzi huyo na kuungama uovu wote, makosa yote na dhambi zote za Israeli
(zilizotoka Patakatifu) juu ya mbuzi huyu, kisha alichukuliwa mbali jangwani na
kuachwa huko. Hivyo dhambi zote zilikuwa sasa zimetengwa mbali na mkutano wa
watu na Mungu (soma Walawi 16:20-28).
• Mnyama katika madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa iliwakilisha kafara ya Kristo
msalabani.
21
• Huduma ya kila siku iliyohusisha pia chumba cha kwanza cha Patakatifu ikiwakilisha
sehemu ya kwanza ya huduma ya Yesu katika Patakatifu pa mbinguni (soma Waebrania
7:26-28, 9:11-22).
Huduma ya siku ya upatanisho (siku ya Hukumu – soma Dan.7:9-10) iliwakilisha
huduma ya mwisho ya Yesu katika chumba cha Patakatifu pa Patakatifu mbinguni.
Huduma hii ndiyo inayoendelea sasa. Wote wanaomwamini Yesu na kutubu dhambi
zao watasamehewa na dhambi zao Yesu amezibeba, lakini atakapomaliza huduma hiyo,
dhambi zote zilizoungamwa zitawekwa juu ya Shetani (mbuzi wa Azazeli) aliye
mwanzilishi wa dhambi na ndiye atabeba hukumu ya dhambi hizo katika jehanamu.
Wale watakaokataa kumpa Yesu dhambi zao (kutubu) watapaswa kubeba hukumu au
mzigo wao wenyewe (soma Waebrania 9:23-28). Je, utachagua kundi gani?
Kwa hiyo sasa hivi hatuna haja ya kutoa wanyama kuwa kafara kwa dhambi maana Kristo tayari
amejitoa kwa ajili yetu. Hatuna haja kwenda kwa mtu yeyote ili kuungama mbele zake, bali
tunakwenda moja kwa moja kwa kuhani wetu wa mbinguni - Bwana Yesu - ili tuungame kwake.
Hakuna mwakilishi. Wakati wa Patakatifu pa duniani, mdhambi alikwenda yeye binafsi kwa kuhani.
Hakupitia kwa mtu mwingine ili amwombee, na hii ilikuwa nakala ya mambo ya mbinguni. Kwa
hiyo tumwendee Yesu moja kwa moja kwa njia ya maombi na kuungama dhambi zetu kwake, ili yeye
atuombee kwa Baba.
Jambo jingine muhimu ni kuwa ijapokuwa mdhambi aliondolewa dhambi alipopeleka mnyama wa
kafara, lakini ilimpasa kushirikiana na kuhani mkuu kwa huduma ya siku ya upatanisho na utakaso
kwa njia ya kujitaabisha roho yake, asije akakataliwa mbali na watu wa Mungu. Sasa wengi
wanaodai kumwamini Yesu kama mwokozi, wameishia tu pale katika huduma ya kafara katika
madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa (msalabani) na hawajui kuwa baada ya kutoa kafara, Kuhani
wetu mkuu - Yesu - ameingia Patakatifu pa mbinguni ili kukamilisha huduma yake ya Upatanisho -
ambayo ni kukomesha dhambi kabisa moyoni mwa muumini. Na kwa sababu hiyo, anasubiri kila
mtu atambue ukweli huu na kufanya uamuzi - halafu atatupa chini chetezo na kumaliza kazi ya
upatanisho na kupatakasa Patakatifu (soma Ufunuo 15:5-8). Mara tu Kristo atakapomaliza huduma
yake katika Patakatifu pa Patakatifu pa mbinguni, atakuja mara ya pili kwa wale wamtazamiao kwa
wokovu (soma Waebrania 9:28). Kwa hiyo, sasa hivi tuko katika siku kuu ya upatanisho. Kristo
yuko mbinguni mbele za Baba kwa ajili yetu. Huu ni wakati wetu kujitaabisha roho zetu kwa
kufanya toba kamili kwa Mungu wetu na kuwa na imani katika Kristo Yesu ili dhambi zetu
zisamehewe na kufutwa na Kristo awezekurudi na kutuchukua mbinguni. Kumbuka, mioyo yetu ni
hekalu ambalo Mungu anataka akae na kutawala. Je, tutamruhusu aingie na kutawala (soma Ufunuo
3:20-21)?
DHAMBI:
Katika masomo haya ambayo umeendelea kujifunza, naamini umeona wazi kuwa kilichosababisha
mpango huu wa wokovu ni dhambi. Nafasi hii tena ni ya kuiangalia dhambi kwa uwazi zaidi.
• Je, Dhambi ni nini? Neno la Mungu (Biblia) linasema “Kila atendaye dhambi afanya uasi,
kwa kuwa dhambi ni uasi” (1 Yohana 3:4).
• Uasi huu ni wa nini? Uasi huu ni wa torati au sheria ya Mungu (soma Warumi 7:7-8).
• Je, torati ina asili gani? “Ni takatifu, na ya haki na njema” na pia asili yake ni ya rohoni
(soma Warumi 7:12-14).
22
Unaposoma Warumi 7:15-24, neno la Mungu limeonyesha wazi hali yetu ya dhambi.
Imeelezwa kuwa imo ndani yetu na ndiyo sheria inayotawala viungo vyetu kiasi kwamba
hata tukitaka kutenda lililo jema, hatupati, maana hamna jema lolote ndani yetu isipokuwa
dhambi tu. Hii ni sawa na kusema nia ya miili yetu daima ni kutenda dhambi.
• Je maandiko yanasema nini kuhusu hii nia ya miili yetu? Warumi 8:6-7 inasema, “Kwa
kuwa nia ya mwili ni mauti, bali nia ya roho ni uzima na amani. Kwa kuwa ile nia ya
mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu. Wala haiwezi kuitii”.
Hali hii ya uadui juu ya Mungu ndiyo kila mwanadamu aliyo nayo. Ndiyo asili tunayorithi toka kwa
Adamu (soma Warumi 5:12, 3:10-18, Zaburi 14:2-3). Kumbuka lilitokea pale Edeni bustanini mara
Adamu na Hawa walipoasi walijikuta wamekuwa maadui wa Mungu na marafiki wa Shetani (soma
Yohana 8:44, 1 Yohana 3:8). Hivyo hakuna mtu yeyote anayeweza kukanusha kuwa kwa asili yake
hana uadui na Mungu. Si swala la uchaguzi ni la kurithi (soma 1 Petro 1:18). Kumbuka daima kuwa,
dhambi ni ile nia ya mwili ambayo ni uasi wa sheria za Mungu, ni uadui juu ya Mungu. Ndiyo maana
tunapaswa kutafakari upya juu ya maisha yetu na yote tuyawazayo, tusemayo na kuyatenda. Je, ni nia
ya miili (Nafsi) yetu au ni mapenzi ya Mungu. Na ili kujua kama ni mapenzi ya Mungu au la, njia ni
kuyapima kwa nuru ya neno la Mungu. Ikiwa ni sawa sawa na neno hilo, basi jambo hilo si dhambi
(soma Isaya 8:20).
Siku hizi yapo mambo mengi sana yanayofanyika kinyume kabisa na neno la Mungu, na tena
mengine kwa jina la dini, na watu wengi wanafikiri ni sawa tu. Wengine hujaribu kupima na kusema
dhambi hii ni ndogo tu na haiwezi kumzuia mtu kuingia mbinguni. Yote haya ni hila za Shetani
kuwadanganya wanadamu ili hatimaye wapotee. Usidanganyike mpendwa, Biblia inasema ,“Mungu
hadhihakiwi, kwa kuwa chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna, maana yeye apandaye kwa
mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu,; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho
atavuna uzima wa milele” (Wagalatia 6:7-8). Dhambi ndogo au moja ni nia ya mwili ambayo ni
uadui juu ya Mungu. Dhambi kiasi au nyingi ni nia ya mwili ambayo ni uadui juu ya Mungu. Hivyo
wote ni maadui wa Mungu na ndiyo maana hukumu yao ni moja tu - ziwa la moto. Yakobo 2:10.12
inasema, “Maana mtu awaye yote atakayeishika sheria yote, ila akajikwaa katika neno moja, amekosa
juu ya yote. Maana yeye aliyesema usizini, pia alisema usiue. Basi ijapokuwa hukuzini, lakini
umeua, umekuwa mvunja sheria ----.” Jipime katika sheria takatifu (amri kumi) za Mungu ili ujue
uko kwa Mungu au kwa shetani aliye mwenye dhambi.
Kristo Yesu pekee ndiye tumaini letu la wokovu. Hebu tufungue mioyo yetu ili aingie na kutushindia
dhambi. Kumbuka torati au sheria ya Mungu asili yake ni ya rohoni.
Hivyo uasi wa sheria hii pia unaanzia moyoni (soma Isaya 14:13-14, Ezekieli 28:17). Uasi ulianzia
moyoni mwa Lusifa na akawa Shetani. Adamu na Hawa walitenda dhambi (kula tunda) wakati
walipopoteza uhusiano na Mungu mioyoni mwao. Hivyo kula tunda ilikuwa ishara ya nje ya uasi
moyoni. Badala ya kumwamini Mungu, walimwamini Shetani. Ndivyo ilivyo leo, wale wote
wanaomwamini Yesu, wanapewa uwezo kufanyika wana wa Mungu. Hili si swala la kinywani tu,
bali ni la moyoni pia (soma Warumi 10:9-10). Wale wanaomwasi Mungu na kumwamini Shetani
wanaendelea kutenda dhambi na mwisho ni kuangamia milele (soma Ufunuo 21:8).
KRISTO AKIPOKELEWA MOYONI:
1. Atakupatanisha na Mungu kwa kuondoa ile nia ya mwili ambayo ni uadui juu ya Mungu. Nia ya
mwili ndiyo dhambi (soma Waefeso 2:13-17, 1 yohana 2:2, 3:8, 1Timotheo 2:5). TOBA!
2. Utasamehewa dhambi (soma Warumi 3:25-26, Mathayo 2:37-38, 3:19, 1 Yohana 1:8-9).
3. Anakupa uwezo kufanyika mwana wa Mungu, yaani uwezo wa kutii sheria za Mungu kikamilifu
(soma Yohana 1:12-13, 14:15, 15:1-8).
4. Anakupatia uzima wa milele (soma Yohana 3:16, 5:24-29, 6:39,48-58).
23
5. Anakupatia ushindi juu ya dhambi (soma 1 Kor. 15:57, Warumi 7:25, 1 yohana 5:3-5, Ufunuo
12:11).
Yote haya Mungu wetu ametupatia kutokana na upendo ulio mkuu kwetu wanadamu. Neno lake
linasema, “mmeokolewa kwa neema” (Waefeso 2:8-9). Neema hii imefunuliwa katika Kristo Yesu.
Na yeyote anayempokea Yesu kuwa Bwana na mwokozi wa maisha yake anakuwa ni adui wa Shetani
maana ndani yake kuna adui ya Shetani, na vita vile vilivyoanza mbinguni vinajitokeza kwa sura ya
juu zaidi. Lakini Bwana asifiwe, Kristo Yesu ameshinda.
WITO WA MWISHO WA WOKOVU KWA ULIMWENGU
Katika kitabu cha Warumi 13:12 tunasoma, “Usiku umeendelea sana, mchana umekaribia -----.”
1 Petro 4:7 inasema, “lakini mwisho wa mambo yote umekaribia, basi iweni na akili, mkeshe katika
sala”. Mwisho wa mambo yote! Mwisho wa biashara, elimu, kazi, vyeo, kilimo, anasa, mwisho wa
dunia na vyote vilivyomo. Lakini mbona mwisho huu haujafika?
2 Petro3:9 inasema, “Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake---- bali huvumilia kwenu, maana hapendi
mtu yeyote apotee bali wote wafikilie toba.”
Kwa hiyo mpendwa, Mungu wetu anayetupenda upeo. Hapendi tupotee, ndio maana ameendelea
kutusubiri ili tuujue ukweli halisi, yaani ile injili ya milele au habari njema ya ufalme, halafu tufanye
uchaguzi, ama kuamini au kutoamini, ndipo ule mwisho uje. Hivyo kabla ya ule mwisho, Mungu
ametuletea ujumbe wa mwisho wa onyo. Ujumbe huo ndio sehemu ya mwisho ya kijitabu hiki.
Ujumbe huu wa mwisho unajulikana kama Ujumbe wa Malaika Watatu. Hebu jifunza ujumbe huu
kwa makini maana ni ujumbe kwa watu wote waishio duniani.
Malaika wa Kwanza
Ufunuo 14:6-7, “kisha nikaona malaika mwingine akiruka katikati ya mbingu, mwenye injili ya
milele, awahubiri hao wakaao juu ya nchi, na kila taifa na kabila na lugha na jamaa,
akasema kwa sauti kuu, mcheni Mungu na kumtukuza, kwa maana saa ya hukumu
yake imekuja, msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi
za maji”.
ß Malaika ni nani? Ni watumishi wa Mungu (soma Waebrania 1:7, Ufunuo 19:10). Hivyo malaika
hawa huwakilisha watumishi wa Mungu (wanadamu) wanaotangaza ujumbe huo. Sasa hebu tutafakari
ujumbe au wito wa Mungu kwa njia ya malaika huyu wa kwanza. Malaika anasema:
• “Mcheni Mungu.” - Kumcha ni kumpa mhusika heshima iliyo ya juu sana. Hivyo Mungu
anatuita tumpe yeye heshima iliyo kuu sana na kumpa nafasi ya kwanza katika maisha yetu
badala ya kutanguliza nafsi ambazo hutufanya tuwe na Miungu mingine (soma Kutoka 20:3).
Tutii amri zake.
• “Na Kumtukuza.” - Tumpe Mungu utukufu wake. Njia ambayo kwayo tutampa utukufu ni kwa
kuishi maisha matakatifu ya utii kamili kwa amri za Mungu. Ni kuacha dhambi na kuishi maisha
ya ushindi katika Kristo Yesu (soma Mathayo 5:16, Waefeso 5:8-10, Yohana 15:8). Haki kwa
imani.
24
• “Kwa maana saa ya hukumu yake imekuja.” - Saa ya hukumu ni ule wakati au kipindi cha
huduma ya Yesu katika chumba cha Patakatifu pa Patakatifu mbinguni; huduma ambayo
iliwakilishwa na huduma ya siku ya upatanisho katika nyakati za huduma ya Patakatifu pa
duniani kama tulivyojifunza katika somo lililohusu Patakatifu. Hukumu ni kuamua kuwa mtu
huyu hana hatia hivyo yuko huru au kuwa ana hatia hivyo aadhibiwe. Kama tulivyoona, sasa
tunaishi katika saa hiyo ya hukumu, katika siku kuu ya upatanisho (soma Danieli 8:14, 7:9,10,13,
1 Petro 4:17). Wale wanaomuamini Yesu wanahesabiwa haki na kukubaliwa kwa ufalme wa
Mungu - Majina yao yameandikwa katika kitabu cha uzima. Wale wasioamini wanaandikwa
katika kitabu cha hukumu (soma Ufunuo 3:5, 20:12). Saa hiyo ni sasa.
• “Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji.” Hapa neno la
Mungu linatukumbusha kuhusu ibada (msujudieni) na pia linatueleza ni kwa nini tumsujudie,
linasema kwa kuwa ni Muumbaji. Unajua jambo pekee linalomtofautisha Mungu wa kweli na
miungu mingine ya uongo ni uwezo wake wa uumbaji. Katika ibada ya dini nyingi duniani, watu
wamekuwa wakiabudu vitu vingine badala ya Mungu wa kweli, huku wakidhani wanamwabudu
Mungu Muumbaji. Je, unawezaje kujua kama unamwabudu Mungu wa kweli aliyeumba mbingu
na nchi na bahari na vyote vilivyomo? Je, kuna ishara yoyote inayotajwa katika Biblia kuonyesha
jambo hilo? Ndiyo, hebu tusome. Kutoka 31.13, “Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni
ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi
Bwana niwatakasaye ninyi.” Ezekieli 20:12, “Tena naliwapa Sabato zangu, ziwe ishara kati ya
mimi na wao, wapate kujua ya kuwa mimi, Bwana, ndiye niwatakasaye.” Ezekieli 20:20,
“Zitakaseni Sabato zangu, nazo zitakuwa ishara kati ya mimi na ninyi, mpate kujua ya kuwa mimi
ndimi Bwana, Mungu wenu.”
Ishara hii inatuelekeza moja kwa moja katika amri ya nne kati ya zile amri kumi za Mungu. Hii
ni amri ambayo watu wengi sana duniani hawaishiki, tena watu wa dini zote, wakati hiyo ndiyo
ishara pekee ya kumwabudu Mungu wa kweli. Hii inaonyesha jinsi watu wengi wamekuwa
wanaabudu miungu mingine badala ya Muumbaji. Lakini je amri hiyo ya nne inasemaje? Kutoka
20:8-11 inasema, “Ikumbuke siku ya sabato uitakase, siku sita fanya kazi, utende mambo yako
yote, lakini siku ya Saba ni Sabato ya Bwana, Mungu wako, siku hiyo usifanye kazi yoyote,
wewe, wala mwana wako, wala binti yao. Wala mtumwa wako, wala mjakazi wako, wala
mnyama wako wa kufuga. Wala mgeni aliye ndani ya malango yako. Maana, kwa siku sita
Bwana alifanya mbingu, na nchi, na bahari, na vyote vilivyomo, akastarehe siku ya saba, kwa
hiyo Bwana akaibarikia siku ya Sabato, akaitakasa.” Soma pia Mwanzo 2:1-3.
• Neno la Mungu halituambii kuwa tuchague siku yoyote katika wiki ili iwe Sabato. Linasema si
yetu, ni ya Bwana. Siku aliyostarehe akaibariki na kuitakasa. Siku nyingine sita hazina utakaso
wala mibaraka ya Sabato, hivyo haziwezi kuwa siku ya Sabato. Siku ya saba ya juma (wiki)
ndiyo Sababo, na siku hiyo ni Jumamosi. Kumbuka msomaji, jambo lolote lililo kinyume na
neno la Mungu ni nia ya mwili (nafsi), ambayo ni uadui juu ya Mungu, ambao ndio dhambi.
Angalia ibada yako isiwe ya bure (somo Mathayo 15:8-9). Hivyo wote wanaotaka Mungu
muumbaji awe Mungu wao wanapaswa kuonyesha ibada yao ya kweli kwa kuitunza Sabato na
wala si vinginevyo. Wote watakaokataa ishara hii ya Sabato watakuwa wanasujudia kitu
kingine. Sabato inamtofautisha na kumtangaza Mungu kama muumbaji.
• Lakini malaika huyu, pia ana injili ya milele. Injili ya milele ndizo habari njema za wokovu
katika Kristo Yesu ambazo umekuwa ukizisoma katika maelezo yaliyopita. “Wala hakuna
wokovu katika mwingine awaye yote, maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa
wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo” isipokuwa la Yesu (Matendo 4:12).
• Huu ndio ujumbe ambao unatakiwa uhubiriwe kwa watu wa mataifa yote kuwa Yesu ni
mwokozi pekee wa ulimwengu na wale wanaomwamini wataonyesha imani yao kwa kuzishika
amri zake ikiwemo na Sabato ya siku ya saba ya juma, yaani Jumamosi.
25
Malaika wa Pili
Ufunuo 14:8, “Kisha mwingine, malaika wa pili, akafuata, akisema, umeanguka, umeanguka
Babeli, mji ule ulio mkubwa, maana ndio uliowanywesha mataifa yote mvinyo ya ghadhabu ya
uasherati wake.”
• “Umeanguka.” - Neno hili limetumika kuonyesha hali ya kuuacha ukweli wa neno la Mungu
kama msingi pekee wa imani na kugeukia mafundisho mengine yasiyo na msingi katika
maandiko (soma Mathayo 7:24-27). Hili ni anguko la Kiroho. Anguko hili limeelezwa katika
ujumbe huu wa malaika wa pili kama matokeo halisi na yasiyoepukika kwa mtu yeyote au dini
yoyote isiyokubali kuupokea ujumbe wa malaika wa kwanza. Kumbuka malaika wa kwanza
anahubiri injili ya milele (yaani wokovu katika Kristo Yesu pekee). Anatuita tumtukuze Mungu
kwa kuzishika amri zake. Anatuita tumpe Mungu heshima ya juu sana na nafasi ya kwanza katika
maisha yetu, kumsujudia (kumwabudu) na kuonyesha ibada hiyo ya kweli kwa kuitunza na
kuitakasa Sabato ya siku ya saba ya juma kumtukuza Mungu kama muumbaji wa mbingu na nchi
na bahari na vyote vilivyomo. Huu ndio mpango wa Mungu.
Kwa hiyo kuukataa (kutokuupokea) ujumbe huo wa malaika wa kwanza, ni kuukataa mpango
halisi wa Mungu na kuanguka kiroho. Na popote neno la Mungu linapokataliwa, Shetani
huingiza mafundisho ya uongo ili kuchukua nafasi hiyo. Ndiyo maana mafundisho ya dini zote
tulizo nazo leo, yako kinyume kabisa na Mungu. Na ndio sababu ya kuwa na dini mbalimbali na
madhehebu mengi sana tofauti, huku tukidai tunamwamini na kumwabudu Mungu mmoja. Huu
ni uongo wa shetani ili kuwapoteza wanadamu (soma Mathayo 15:8-9, 2 Kor. 11:13-15).
Usalama wetu ni kukubali wito wa Mungu kwetu kama unavyoelezwa katika ujumbe wa malaika
wa kwanza.
• “Babeli, mji ule ulio Mkubwa.” - Kwa mara ya kwanza katika Biblia mji ulioitwa Babeli
ulijengwa na mtu aliyeitwa Nimrodi, ambaye alifanya vita kubwa sana dhidi ya Mungu kwa
kuwafundisha watu kwenda kinyume na neno la Mungu. Alianzisha ufalme wa kwanza kabisa
duniani uliokuwa kinyume na Mungu (soma Mwanzo 10:8-14). Miji hii mikubwa aliyoijenga
ndiko kulikuwa chimbuko la ibada nyingi za uongo tunazoziona leo. Hebu angalia jinsi Nimrodi
alivyopingana na Mungu. Katika kitabu cha Mwanzo 1:28 tunasoma, “Mungu akawabarikia,
Mungu akawaambia, zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi ----.” Na katika mwanzo 9:11 tunasoma,
“na agano langu nitalithibitisha nanyi, wala kila chenye mwili hakitafutwa tena kwa maji ya
gharika, wala hakutakuwa tena gharika, baada ya hayo kuiharibu nchi.” Huo ndio ulikuwa
mpango wa Mungu. Lakini chini ya Nimrodi watu walifanya mpango ulio kinyume,
“Wakasema, haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbunguni; tujifanyie jina,
ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote” (Mwanzo 11:14). Kwa hiyo wao hawakutaka
kutawanyika usono pa nchi, na pia hawakumwamini Mungu kuwa hataleta tena gharika, hivyo
wakaamua kujenga mnara na kilele kifike mbinguni, ili gharika ikija tena, wapande juu ya mnara
na kujiponya. Jambo jingine muhimu kulitambua ni ile kanuni iliyowasukuma kufanya hivyo.
Nafsi, nafsi, nafsi, ndiyo waliyoitii, badala ya kumtii Mungu, maana walisema tujijengee,
tujifanyie jina, tusipate…, - binafsi. Hii ndiyo iliyokuwa kanuni iliyomwongoza Shetani kuasi
(soma Isaya 14:13-14). “Nita” “mimi”; ndiyo msingi wa anguko la mwanadamu katika dhambi,
na ndio msingi wa imani au dini zote zisizojengwa katika neno la Mungu. Hiyo, ndiyo kanuni ya
Babeli. Sasa, mji ule uliojengwa na Nimrodi uliharibiwa lakini mji huo wa Babeli ukajengwa
tena na mfalme aliyeitwa Nabukadreza kwa kanuni ile ile ya kujitukuza nafsi kuliko Mungu
(soma Danieli 4:29-32). Mji huu ulikuwa mkubwa. Ukaitwa “mji wa dhahabu,” “utukufu wa
dunia nzima” na ufalme huo wa Babeli ulitukuka sana. Lakini kwa sababu ya kumwasi Mungu
na kutompa utukufu, mji huu nao uliharibiwa (soma Isaya 21:9, Yeramia 51:52-64). Hivyo mji
huu ya Babeli unawakilisha mifumo yote ya dini za uongo zilizomwasi Mungu. Na kama mji huu
halisi ulivyoanguka na kuangamia na hata leo haupo, inasimama kuwa ishara kwamba imani au
dini zote zisizojengwa katika Biblia mwisho wake ni kuanguka na kuangamia milele (soma
Ufunuo 18:5-24).
Ndugu msomaji, umesimama upande gani? Katika imani inayowakilishwa na Babeli, ambazo ni
imani zilizoanguka; au upande wa Bwana? Hii ni nafasi yako ya pekee sana kuchagua wokovu
kama unavyofunuliwa na neno la Mungu.
26
• “Maana --- uliwanywesha mataifa yote mvinyo--- ya uasherati wake.”
ß Kunywesha ni kufundisha (soma Yohana 4:14, 7:37-38).
ß Mvinyo ni mfano wa mafundisho ya uongo. Kama tunavyofahamu kuwa mvinyo ni
pombe au kileo, na mtu anapokunywa analewa na matokeo ya kulewa tunayafahamu.
Hivyo mfumo huu wa imani au dini au mafundisho ya uongo, ambayo yana
chimbuko lake katika mji wa Babeli, yameenea kwa mataifa yote na kusababisha
watu kulewa na mafundisho hayo hata wasitambue kweli ya neno la Mungu.
Yeremia 51:7 inasema, “Babeli umekuwa kikombe cha dhahabu mkononi mwa
Bwana. Kilicholevya dunia yote; mataifa wamekunywa mvinyo wake; kwa sababu
hiyo mataifa wameingiwa wazimu.” Mambo ya kutisha ajabu. Kama mataifa
wamekuwa na wazimu kwa sababu ya mafundisho hayo ya uongo ya kidini, je,
tunaweza kushangaa ni kwa nini dunia yetu imejaa magomvi, mauaji, zinaa, ubakaji,
vita, dhuluma na kuharibika kwa maadili mengine mengi? Na katika hali hiyo
ukweli wa neno la Mungu unaposemwa wazi, watu hawa walio na wazimu
watawatesa na kuwaua watu wa Mungu.
ß Uasherati wake - huwakilisha uhusiano usio halali nje ya ndoa. Neno la Mungu
huelezea uhusiano kati yake na watu wake kwa mfano wa uhusiano wa ndoa -
Mungu kama mume na watu wake kama mke wake. Mambo haya ni ya kiroho na
tunatakiwa kuyatambua kwa jinsi ya rohoni (soma 1Kor. 2:13-15). Uhusiano huo
umeelezwa katika Yeremia 3:14, Isaya 54:5-6 na Waefeso 5:25-32. Kwa hiyo
tunapomwacha Mungu wetu kwa kutolishika neno lake, ijapokuwa tuwe na dini na
kuabudu, lakini tutakuwa tunaabudu Mungu mwingine asiye wa kweli, na hivyo
tutakuwa tunafanya uzinzi kiroho. Kwa hiyo Babeli ilimwasi Mungu na kufundisha
uongo ambao leo umeenea katika mataifa yote. Mafundisho mengi yaliyomo katika
baadhi ya madhehebu ya kikristo, Uislamu, Buddha, Hindu, dini za kimila nk. ni ya
uongo, na hivyo yanawakilisha Babeli (mke aliyemwasi mumewe) kiroho.
ß Sasa, kama miji ile ya Babeli iliishaanguka, je, leo bado tunaweza kusema kuna mji
wa Babeli? Ndiyo. Leo pia bado kuna Babeli ya sasa ambayo siyo mji bali ni
mamlaka ya dini ambayo ndani yake yamejaa mafundisho ya kipagani, na
mafundisho hayo yameenea katika dini mbali-mbali duniani. Hivyo badala ya
mamlaka hiyo ya kidini kuwa mke wa kristo, sasa inaitwa, “Babeli Mkuu, mama wa
makahaba na machukizo ya nchi” (soma Ufunuo 17:1-6). Lakini jina hili ni la siri,
unaweza tu kulitambua kutokana na nuru ya neno la Mungu. Na hiyo ndiyo mamlaka
ya kanisa la Rumi (Roman Catholic) kama mama, na makanisa mengine yote
yanayofuata mafundisho yake kama watoto wake ambao pia ni makahaba (soma
Ufunuo 17:18).
Baadhi ya Mafundisho ya Babeli ni:
1. Imani kwamba mtu ana roho ambayo haifi - huishim milele.
2. Waovu kuungua milele na milele katika jehenamu ya moto.
3. kuabudu jua, mwezi na nyota.
4. Ibada ya siku ya kwanza ya juma, yaani Jumapili.
5. Kuombea na kuomba wafu.
6. Kusujudia na kuabudu sanamu nk.
27
Ujumbe wa Malaika wa Tatu
Ufunuo 14:9-12, “Na mwingine, malaika wa tatu, akafuata, akisema kwa sauti kuu, mtu awaye yote
akimsujudu huyo mnyama na sanamu yake, na kuipokea chapa katika kipaji cha uso wake au katika
mkono wake, yeye naye atakunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu iliyotengenezwa, pasipo
kuchanganywa na maji, katika kikombe cha hasira yake, naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya
malaika watakatifu, na mbele za mwanakondoo. Na moshi wa maumivu yao hupanda juu hata milele
na milele, wala hawana raha mchana wala usiku, hao wamsujuduo huyo mnyama na sanamu yake, na
kila aipokeaye chapa ya jina lake. Hapa ndipo penye subira ya watakatifu, hao wazishikao amri za
Mungu na imani ya Yesu”.
Malaika huyu wa tatu anauonya ulimwengu juu ya kumsujudia mnyama na sanamu yake na kuipokea
chapa yake. Hukumu ya kutisha inatangazwa dhidi ya wote watakaomsujudia mnyama huyu -
kutupwa katika ziwa la moto - ni hukumu ya kutisha. Kwa nini usijiepushe na mnyama huyu? Je,
unamfahamu? Hebu tunapoelekea mwishoni, jifunze kumfahamu mnyama huyu.
- “Mnyama” – Biblia inatafsiri mnyama kuwa ni mfalme au ufalme (soma Danieli 7:15-17, 23-
25.) Katika Ufunuo 13:11-18 inaelezea kuhusu mnyama (ufalme) utakaoilazimisha dunia na
wote wakaao ndani yake wamsujudie mnyama anayeitwa wa kwanza na sanamu yake.
Mnyama huyu wa kwanza ni yule anayetajwa katika Ufunuo 13:1-8. Huyu ni yule aliyepokea
au kurithi mamlaka ya dola ya Kirumi (soma Ufunuo 13:1-2.) Joka ni tafsiri ya mamlaka
aliyotumia Shetani ili kumwangamiza Bwana Yesu (soma Ufunuo 12:1-5) na maandiko
yanaonyesha wazi kuwa mfalme wa Kirumi (Herode) alianzisha mauaji makuu ya watoto ili
ikiwezekana amwangamize Yesu, lakini Mungu alimwokoa na mauaji hayo (soma Mathayo
2:13-23.) Mnyama huyu, ambaye watu wote watalazimishwa kumsujudu na ambaye ni mrithi
wa kiti ch enzi cha dola ya Kirumi, si mwingine isipokuwa ni MAMLAKA YA KANISA LA
RUMI au UPAPA. Hivyo neno la Mungu linafunua jambo muhimu sana kwa kila mtu
aishiye duniani kwamba usalama wetu pekee, ili kuokoa roho zetu, ni kutomsujudia Mnyama
na sanamu yake. Jambo hili liko mbele yetu na kila mtu atatakiwa kufanya uchaguzi,
kwamba amsujudie Mungu aliyeziumba mbingu na nchi na bahari na vyote vilivyomo kwa
kuzishika amri zake (soma Ufunuo 14:6-7) au amsujudie mnyama na sanamu yake, ambako
kwa kweli ni kumsujudia Shetani mwenyewe (soma Ufunuo 13:2.) Katika Ufunuo 13:11-18
inaongezea juu ya ufalme (utawala) utakaolazimisha dunia na wote waliomo kumsujudia
Rumi lakini Ufunuo 17:12-18 inaongezea kufunua jambo hilo zaidi kwa kuonyesha kuwa
licha ya ufalme au utawala mmoja utakaolazimisha ibada hii iliyo kinyume na Mungu, tawala
zingine pia duniani (wafalme kumi) wataungana katika kutekeleza jambo hilo. Hivyo
tunachojifunza hapa ni kuwa tawala zote za dunia zitaungana kulazimisha ibada kwa kufuata
mwongozo wa Kanisa la Rumi (soma Ufunuo 16:13-14.) Wafalme hawa watapokea
mamlaka pamoja na yule mnyama, yaani kutakuwa na muungano maalum kati ya Kanisa la
Rumi na mataifa ya dunia hii kutimiza jambo hili. Kumbuka kuwa Rumi inamafundisho yake
yaliyo kinyume kabisa na neno la Mungu.
- “Sanamu ya Mnyama” – Sanamu ni mfano wa kitu halisi. Kama Mnyama ni mamlaka ya
Kanisa la Rumi (RC), sanamu yake ni mamlaka ipi? Mamlaka nyingine ya Kikristo iliyofuata
baadhi ya mafundisho ya Rumi na hivyo kuchanganya neno la Mungu na mapokeo, ni
Uprotestanti. Hivyo sanamu ya Mnyama ni UPROTESTANTI ULIOASI, ambao ijapokuwa
unadai umejitenga na Kanisa la Rumi, lakini mafundisho yao makuu ni yaleyale ya Rumi, na
leo makanisa hayo yako mbioni kurudi kwa mama yao – KUUNGANA (soma Ufunuo 17:5.)
- “Chapa Katika Kipaji cha Uso” – Akili ndiyo sehemu muhimu inayohusika katika ufahamu
na uamuzi mtu unaoweza kuufanya (soma 2 Wakorinto 5:13, Waefeso 5:15-17.) Hivyo,
kukubaliana na mafundisho na mfumo utakaowekwa na serikali za dunia zikishirikiana na
Kanisa la Rumi, ndiko kupokea chapa katika kipaji cha uso. Jambo la muhimu kukumbuka ni
kuwa kimsingi imani ya Kirumi inayakubali mambo yote ya msingi yaliyomo katika dini
nyingine, na hivyo kwa msingi huo, hata dini nyingine zitakubaliana na mpango huu. (Je, hii
ni kweli?)
28
- “Chapa Mkononi” – Mikono yetu ndiyo viungo vikuu vya utendaji, kwa maana ya kutekeleza
kazi. Ijapokuwa mwili mzima unahusishwa katika kazi, lakini mikono yetu ndio hasa hufanya
sehemu kubwa kivitendo. Hivyo kupokea chapa ya Mnyama katika mkono ni kutekeleza
kivitendo maamuzi au maelekezo yatakayotutaka tumsujudie Mnyama kwa kuiheshimu
Jumapili kama siku ya Bwana.
Katika Ufunuo 13:8 inasema, “Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake
halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya
dunia.” Maandiko yako wazi kuwa wale ambao hawatamsujudu Mnyama ni wale ambao majina yao
yameandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwanakondoo. Lakini je, ishara ya kuonyesha kuwa mtu
anamsujudu Mnyama (Rumi) itakuwa nini? Ishara ya alama hiyo ni kuiheshimu Jumapili kama siku
ya Bwana. Tulitangulia kujifunza kuwa Mungu Muumbaji anasema Sabato ndiyo ishara kati yake na
watu wake ya kuwa yeye ndiye Mungu wao (soma Ezekieli 20:12,20) na Sabato ni Jumamosi.
Lakini kwa sababu yule Mnyama alipokea mamlaka toka kwa joka ambaye ni Shetani na ambaye
ameendelea kupingana na Mungu tangu alipoasi, yeye naye aliweka siku inayoonyesha kuwa na yeye
(Shetani) anaabudiwa au kusujudiwa, na siku hiyo ndiyo Jumapili (soma Mathayo 15:8-9 na Ufunuo
13:3-4.) Kwa nini, ndugu, usichague kusimama upande wa Bwana kwa kuzitunza amri zake na
kuishika Sabato yake? Je, jina lako linawezaje kuandikwa katika kitabu cha uzima cha
Mwanakondoo? Tafakari kisa hiki. Wakati Waisraeli walipozidi kumwasi Bwana jwangwani,
Mungu alimwambia Musa kuwa atawaangamiza Waisraeli halafu atamfanya yeye (Musa) kuwa taifa
kuu (soma Kutoka 32:9-11.) Lakini Musa akamsihi Bwana na kusema, “Walakini sasa ikiwa
utawasamehe dhambi yao na kama sivyo unifute, nakusihi, katika kitabu chako ulichokiandika”
(Kutoka 32:32.) Lakini “Bwana akamwambia Musa, mtu yeyote aliyenitenda dhambi ndiye
nitakayemfuta katika kitabu changu….” (fungu la 33.) Kwa hiyo mtu anayeandikwa katika kitabu
cha uzima cha Mungu ni yule aliyesamehewa dhambi (amekiri, ameungama na kuziacha) na
amehesabiwa haki. Na kama tulivyotangulia kujifunza, mdhambi anasamehewa au anahesabiwa haki
pale anapomkiri na kumwamini Bwana Yesu na hapo ndipo jina lake huandikwa katika kitabu cha
uzima (soma Matendo 2:38-39 na Warumi 3:21-26.) Kwa kuwa Kristo anapopokelewa moyoni
anatupatia uwazo wa kumtii Mungu kwa kuzishika amri zake, basi yeyote atakayempokea Yesu
ataonyesha utii kwa amri hizo. Hivyo utii mkamilifu kwa amri za Mungu utakuwa ngao dhidi ya
hatari ya kumsujudia Mnyama na sanamu yake.
Mungu wetu wa upendo ametufunulia mambo haya wazi. Kwa nini tupotee? Hebu mchague Yesu
leo na uamue kuishi sawasawa na amri zake ili jina lako liwe katika kitabu cha uzima, usije
ukamsujudu Mnyama badala ya kumsujudia Mungu.
- “Kunywa katika mvinyo ya ghadhabu ya Mungu” - Ni hukumu ya kutisha, au adhabu kali
watakayopata wale wote watakaomsujudu yule mnyama (Roma). Ufunuo 15:1;16:1-21.
Wote watakaokataa kuupokea ukweli, watakuwa wamechagua adhabu hiyo.
- “Isiyochanganywa na maji” - Maana yake isiyo na huruma (soma Yakobo 2:13).
- “Kuteswa kwa moto na kiberíti” - Adhabu katika ziwa la moto (soma Ufunuo 20:10-15).
Wakati tunaelezwa juu ya wale watakaomsujudu mnyama na sanamu yake, tunaelezwa pia juu ya
watakatifu wa Mungu katika saa hii ya mwisho ambao neno la Mungu linasema watatambulikana kwa
kuzishika amri za Mungu na kuwa na imani ya Yesu, ishara kuu itakayowatambulisha ni kuitakasa na
kuitunza Sabato ya siku ya saba ya juma, yaani Jumamosi. Kumbuka Sabato ndiyo ishara ya Mungu
wa kweli aliye muumbaji.
Mpendwa msomaji, sasa tunasimama ukingoni kabisa mwa wakati wa kufungwa kwa rehema na
historia ya dunia hii. Ukweli wa neno la Mungu umefunuliwa wazi kwetu, kwa nini tusichague
kuokolewa sasa kabla hatujachelewa milele (soma 2 Kor. 6:2)? Usije ukadharau maneno haya kama
jambo dogo tu. Pima kila kitu kwa nuru ya neno la Mungu. Kabla ya kufika mwisho, napenda
nikukumbushe visa viwili vya pekee ili kukusaidia - Kisa cha kwanza ni uasi wa Adamu na Hawa.
Unajua kwa akili yetu, kula tunda ni jambo dogo sana, lakini je, matokeo haya mabaya na ya kutisha
yaliyoenea duniani leo unajua ni kutokana na hili lililoonekana dogo tu? Kisa cha pili ni wakati
Sodoma na Gomora ilipoangamizwa kwa moto. Baada ya Lutu na mkewe na binti zao wawili
29
kutolewa nje ya mji, walipewa sharti la kutotazama nyuma na kuwa yeyote ambaye angetazama
nyuma angeangamizwa pamoja na miji ile. Mke wa Lutu aligeuka nyuma na akawa nguzo ya chumvi
(soma Mwanzo 19:17,23-26). Kugeuka nyuma tu!! Hivyo mpendwa, hebu kwa neema ya Mungu,
iliyofunuliwa kweli kwa njia ya Kristo Yesu Bwana wetu, tuzingatie ujumbe huu, tutubu, tufungue
mioyo yetu na kuupokea ukweli wa neno la Mungu na kumpokea Yesu mioyoni ili awe Bwana na
mwokozi wa maisha yetu binafsi, ili tupate kuokolewa tusipotee na dunia. Wito wa Mungu wa
mwisho unasema “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo
yake” (Ufunuo 18:4). Tokeni Babeli.
Mungu anakuita utoke Babeli ili upone. Je, utaitikia wito huo wa rehema? Yesu yu karibu mlangoni
kuja kuchukua wateule wake (soma Yohana 14:1-3).
Huu utakuwa ndio mwisho wa pambano au vita vile vilivyoanzia kule mbinguni kati ya Mikaeli
(Yesu) na malaika zake na Ibilisi na malaika zake, kwa hiyo, kumbuka kuwa uamuzi wowote
utakaoufanya utakuwa unakuweka upande wa mmoja kati ya hao majemedari wawili - Yesu au
Shetani.
Lakini maandiko matakatifu yanasema kwamba Yesu aliishashinda vita kwa ajili yetu, na wote
watakaomwamini atawapatia ushindi. Mungu akubariki ili umchague Yesu leo. Injili hii (habari
njema ya ufalme) inapohubiriwa sasa, kila mtu anafanya uamuzi, kwa uzima (Yesu) au mauti
(Shetani), na kila mtu atakapokuwa amekwishachagua ni upande gani atakayosimama, Bwana Yesu
atarudi mara ya pili, na sasa hayuko mbali (soma Ufunuo 22:12). Anakuja upesi.
M W I S H O

Comments

Popular posts from this blog

SABABU 100 ZA UKWELI WA SUALA LA SABATO

JINSI YA KUINUA VIZAZI VINGI