Kwa nini kutunza siku ya Sabato? Ni nini kusudi la Sabato? Je, ilifanywa lini, nani aliifanya, na kwa ajili ya nani? Siku ipi ni Sabato ya kweli? Wengi hutunza siku ya kwanza ya juma, au Jumapili. Ni mamlaka gani ya Biblia waliyo nayo kwa kufanya hivyo? Wengine hutunza siku ya saba, au Jumamosi. Ni Maandiko gani waliyo nayo kwa kufanya hivyo? Hapa kuna ukweli kuhusiana na siku zote mbili, kama zilivyoelezwa wazi wazi katika neno la Mungu. Sababu Sitini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Saba 1. Baada ya kufanya kazi siku sita za kwanza za juma katika kuumba dunia hii, Mungu mkuu alipumzika siku ya saba. Mwanzo 2:1-3. 2. Hii iliweka muhuri [katika] siku hiyo kama siku ya Mungu kupumzika, au siku ya Sabato, kama siku ya Sabato [basi] humaanisha siku ya kupumzika. Kwa kufafanua: Wakati mtu anapozaliwa siku fulani, siku hiyo huwa siku yake ya kuzaliwa . Kwa hiyo wakati Mungu alipopumzika siku ya saba, siku hiyo ilikuw...
Comments
Post a Comment