IMANI
Imani ni mtu
kuamini Mungu. Neema ni Mungu kuamini mtu
Maisha ni kushirikiana,
barabara mbili, hali ya kupeana na kuchukua ambayo inafanya uhusiano ulio na
mazao bora. Bila ushirikiano huu vile tunajua, maisha hayawezi kuendelea. Hata
Mungu, ingawa ni Mkuu na hagharimii yeyote, amechagua kukamilisha mapenzi yake
kwa kushirikiana na binadamu. Nguvu na afya ya uhusiano wowote unategemea kila
mmoja akitenda sehemu yake kwa njia isiyo ya uchoyo
.
.
Uhusiano ulio nao na Mungu,
kinyume na imani zingine, sio kwa ajili yako. Imani ni kile unachompa Mungu
ukitumai kitabalisha dunia yako. Neema, hata hivyo, ni kile Mungu anakupa,
akitumai kitabadilsha dunia yake. Mungu ndiye tumaini lako … wewe ni wake. Kwa
hivyo, weka imani yako na uamini Mungu wakati ambapo yeye pia ataweka imani
yake kwako. Tumia neema zako za maisha ulizopewa na Mungu kufaidisha Ufalme wa
Mungu na sio wako tu.
Ombi la Leo
Mungu, nisaidie kugundua kwamba
uhusiano wetu ni njia mbili na kwamba sote tunategemeana kwa msaada
tunaohitaji. Najua ninaweza kuweka imani yangu kwako kwa siku zangu za usoni na
naomba uniamini na mipango yako. Kwa neema yako, sitakuangusha.
Maandiko ya Leo
Wakolosai 1:27 Mpango wa Mungu
ni kuwajulisha watu wake siri hii kuu na tukufu ambayo ni kwa ajili ya watu
wote. Na, siri yenyewe ndiyo hii: Kristo yuko ndani yenu, na jambo hilo
lamaanisha kwamba ninyi mtaushiriki utukufu wa Mungu.
Waefeso 2:8 Maana, kwa neema ya
Mungu mmekombolewa kwa njia ya imani. Jambo hili si matokeo ya juhudi zenu,
bali ni zawadi ya Mungu.
Warumi 5:2 Kwa imani yetu, yeye
ametuleta katika hali hii ya neema ya Mungu ambamo sasa tunaishi. Basi,
tunajivunia tumaini tulilo nalo la kushiriki utukufu wa Mungu.
Maswali yanaweza kubadilika kutoka ujira mmoja wa
maisha hadi mwingine; hata hivyo, majibu kila mara ni yale yale
Tunapokua tukupitia maisha,
mara kwa mara tunabadilika katika ujira mmoja hadi mwingine. Kutoka shule ya
watoto hadi shule ya msingi, kutoka shule ya upili hadi masomo ya juu, kutoka
kukuza watoto hadi kustaafu, majira ya maisha huja na kuenda. Kwa kila sehemu
ya maisha kunaweza kuwa na maswali mengi tunayokumbana nayo, mambo ambayo
hatujawahi kabiliana nayo hapo awali.
Ingawa
maswali hayo yanaweza kubalika kutoka ujira mmoja wa maisha hadi mwingine,
majibu hubaki yaleyale. Neno hilo hilo la Mungu, mapenzi ya Mungu, na njia ya
Mungu itakuwa mwongozo wako maishani. Heshima, tabia, unyenyekevu, uvumilivu,
upendo, msamaha, kujizuilia, na imani itakuwa nguzo yako na udhibitisho wa
uvumilivu katika maisha yako yote. Shiklilia majibu yale mepesi yatokayo katika
Neno la Mungu.
Ombi la Leo
Bwana, ninaahidi kuweka Neno
Lako karibu na mimi na kulificha ndani ya moy wangu ili nisitoke katika mapenzi
Yako. Nitalifanya la kutafakari kila wakati na furaha yangu. Niongoze kupitia
majira ya maisha na unipe amani yako kuchao.
Maandiko ya Leo
Waebrania 13:8 Yesu Kristo ni
yuleyule, jana, leo na milele.
Wagalatia 5:22 Lakini matokeo
ya kuongozwa na Roho ni mapendo, furaha, amani, uvumilivu, wema, fadhili,
uaminifu, …
Kuna uwezo kaitka chombo kilicho tupu
2 Wafalme 4 inatuambia hadithi
ya mwanamke aliyekuwa na haja kuu. Akamjia nabii Elisha na akaamuriwa kumba
vyombo vitupu kutoka kwa majirani wake. Elisha akamwambia ya kwamba Mungu
atapaka kiwango kidogo cha mafuta aliyokuwa nayo na kujumulisha kujaza kila
chombo kilichokuwa tupu. Kwanini vyombo vitupu? Vyombo vilivyojaa huenda vikawa
vishafika siku zao kuu, kulingana na ni nini vimejazwa. Vyombo vilivyojaa nusu
angalau vinaweza toa mchanganyiko wa Mungu na mwanadamu vikielekeza kumwagika
chini kwa upako.hata hivyo, vyombo vitupu vinatoa fursa kuu ya kujazwa kabisa
na upako wa kimiujiza wa Mungu. Maisha yetu ni chombo,tunakiinua kwa Mungu.
Wakati mwingi tumejaa nusu ama tumejazwa kabisa na mambo mengine ambayo sio
kuchagua kwa Mungu,ambayo huleta kung’ang’ana ama kushindana na upako ambao
Mungu angelitaka kutumwagia ndani yetu. Je, ungependa kuondolewa mambo haya
kidunia ili ujazwe na Mungu? Jimwage mwenyewe katika maombi na uruhusu upako
mpya wa Roho Mtakatifu ujaze maisha yako.
Ombi la Leo
Baba, najitoa mwenyewe katika
mambo haya ya ulimwengu na nikuuliza ujaze maisha yangu. Sitakata tamaa
ninapojikuta niko tupu nikihitaji upako wako.
Maandiko ya Leo
2
Wafalme 4:1-7 Basi, mwanamke mmoja mingoni mwa wake za wana wa manabii
alimlilia Elisha, akasema, Mtumishi wako mume wangu amekufa; nawe unajua ya
kuwa mtumishi wako alikuwa mcha Bwana; na aliyemwia amekuja iliajitwalie wana
wangu wawili kuwa watumwa. Elisha akamwambia, nikufanyie nini? Niambie; una
kitu gani nyumbani? Akasema, mimi mjakazi wako sina kitu nyumbani, ila chupa ya
mafuta. Akasema, nenda, ukatake vyombo huko nje kwa jirani zako wote, vyombo
vitupu; wal usitake vichache. Kasha uingie ndani, ukajifungie mlango wewe na
wanao, ukavimiminie mafuta vyombo vile vyote; navyo vilivyojaa ukavitenge. Basi
akamwacha, akajifungia mlango yeye na wanawe; hao wakamletea vile vyombo, na
yeye akamimina. Ikawa, vilipokwisha kujaa vile vyombo, akamwmbia mwanawe,
niletee tena chombo. Akamwambia hakuna tena chombo. Mafuta yakakoma. Ndipo
akaja akamwambia yule mtu wa Mungu. Naye akasema, nenda ukayauze mafuta haya,
uilipe deni yako; nayo yaliyosalia uyatumie wewe na watoto wako.
Maisha ni fursa
Hebu wazia kuamka asubuhi moja
bila kazi, gari, ama pengine nyumba. Hii yaweza kuonekana kama moja wapo ya
siku za huzuni maishani mwako ama yaweza kuonekana kama moja wapo ya fursa kuu
ya maisha. Hebu litafakari…ingawaje waweza kukosa ulichokuwa nacho na pengine
haungechagua kukipoteza, hata hivyo, sasa uko na fursa ya kukibadilisha na kile
unachotamani. Pengine, waweza kuijenga vyema zaidi wakati huu, ifanye tofauti
kwa njia nyingine, na uishie kuwa na kitu kinachoambatana na mahitaji yako ya
sasa ama siku za usoni. Hauwezi kila mara kuchagua kile unachopoteza lakini
waweza chagua kufanya bidii kuelekea kubalisha hasara na kile bora zaidi.
Ombi la Leo
Ewe Bwana, nipe neema ya
kuendeleza hasara zangu, na kuwacha majuto yangu mikononi Mwako na nibadilishe
imani yangu Kwako. Nipe hekima ya kutazama kila siku kama fursa ya kufikia ukuu
kwa ubora Wako.
Maandiko ya Leo
Wafilipi 3:13, 14 Ndugu,
sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu;
nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo,
niifikilie mede ya dhawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Isaya 43:18-19 Msiyakumbuke
mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Tazama, nitatenda neno
jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa? Nitafanya njia hata jangwani, na
mito ya maji nyikani.
Kwa pumzi yako ya mwisho waweza sema kwa ujasiri
kwamba siku yako kuu bado iko mbele
Bila kutilia maanani ni nini
tofauti za binadamu: mila, uzalendo, sehemu ya mtu maishani, kama mtu ni tajiri
au masikini, kama mtu amesoma ama ni mpumbavu kabisa, ama hali za kuzaliwa
kwetu, tuko na agano ambalo tutatimiza: agano na kifo.
Agano hili na kifo ndiyo sababu
ni lazima tuhubirie ulimwengu, tukishiriki upendo wa Kristo na tuwakilishe
uchaguzi wa kukubali ama kukataa upendo wa Mungu. Kwa wale wamkataao Kristo,
kifo kitawashikilia hukumu ya kifo, lakini kwa Mkristo, kifo ndiyo njia ya
amani ya milele, furaha, tumaini, na upendo. Tumaini lililo bora zaidi kwa
Mkristo upande huu wa mbingu ni uhakikisho ya kwamba hata nini kitendeke
maishani haya, bora zaidi bado yaja. Ni ya muhimu tuweke mtazamo wa umilele
tunapotazamia maisha kama tunavyoyajua sasa kwa sababu kwa kweli siku yetu kuu
bado iko mbele!
Ombi la Leo
Baba, ninashukuru sana kujua
kwamba Unaniandalia makao. Kwa wakati wa ajabu nitakuona uso kwa uso na nijazwe
na kuelewa kwa upendo wako na utukufu wa uwepo Wako. Ninapotazia maisha,
nisaidie kuweka mtazamo wa umilele - kwa vile wakati yote yamesemwa na
kutendwa, siku yangu kuu bado iko mbele.
Maandiko ya Leo
1 Wathesalonike 4:13-14 Ndugu,
twataka mjue ukweli kuhusu wale ambao wamekwisha fariki dunia, ili msipatwe na
huzuni kama watu wengine wasio na matumaini. Sisi tunaamini kwamba Yesu
alikufa, akafufuka; na hivyo sisi tunaamini kwamba Mungu atawaleta pamoja na
Yesu wale wote waliofariki wakiwa wanamwamini.
Yohana 14:1-3 Yesu aliwaambia,
"Msifadhaike mioyoni mwenu. Mwaminini Mungu, niaminini na mimi pia.
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; la sivyo ningalikwisha waambieni. Sasa
nakwenda kuwatayarishieni nafasi. Na nikienda na kuwatayarishieni nafasi,
nitarudi na kuwachukueni kwangu, ili nanyi muwe pale nilipo mimi.
Luka Mtakatifu 21:28 Wakati
mambo hayo yatakapoanza kutukia, simameni na kuinua vichwa vyenu juu, kwa maana
ukombozi wenu umekaribia."
Kuza subira kuu ya kurudia
Waweza kuwa tayari umesikia
kwamba ufanisi ni zaidi ya hatua moja na kwamba ufanisi mara kwa mara ni ya kwa
wale ambao wanaweza kuvumilia hiyo hatua.
Maisha
yamejawa na majaribu na makosa, ambayo yanahitaji uvumbuzi, tung’oe maishani
yale mambo ambayo yanaweza sababisha kuanguka na kujaribu tena.
Mwenendo wetu wa Kikristo ni
sawa na haya. Maisha ya muumini yanahitaji tuinuke tunapoanguka, tujikung’ute
na tuendelee mbele tena. Sio kwamba jambo halikutendeka inamaanisha
halitatendeka. Yaweza maanisha tu twahitaji kulitenda tena. Je, mawazo yapi ama
majaribio yapi umeyatupilia hapo awali kwa sababu hayakutenda kazi kwa mara ya
kwanza…wahitaji kujaribu tena.
Ombi la Leo
Baba wa Mbinguni, nisaidie
kukuza tunda la Roho maishani mwangu, hasa matunda ya uvumilivu na kujizuilia.
Nifunze kukabiliana na hofu zangu na kutokata tamaa kamwe nikijaribu jambo
ulilonipa kutenda.
Maandiko ya Leo
Wafilipi 3:14 nakaza mwendo,
niifikilie mede ya dhawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Mithali 24:16 Kwa maana mwenye
haki huanguka mara saba akaondoka tena; Bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
Habakuki 2:3 Maana njozi hii
bado ni kwa wakati ulioamuriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake,
wala haitasema uongo; ijapokawia, ingojee; kwa kuwa haina budi kuja, ingojee.
Unayemruhusu katika mviringo wako wa ndani anaweza
kukuzuilia
Wengi wetu ambao walilelewa na
wazazi wamakinifu tulijifunza mapema kiasi ni nani tunapaswa au hatupaswi
kumleta nyumbani kumjua mama. Mama walionekana kana kwamba wametengeneza
mashine ambayo ingewajuza kama kile kikundi tulichokuwa nacho kama watoto ni
kizuri. Walijua kuwa hata tungali watoto, siku zetu za usoni zingeweza
kuadhiriwa na ule mviringo wa marafiki na tunapokomaa, ukweli huu hubaki
vilevile.
Mviringo wetu wa kati wa
marafiki mara nyingi waweza kuwa ndio utatuadhiri sisi zaidi maishani. Wakati
mwingi tunawaamini hawa marafiki na kushiriki nao mambo mengi ya siri na ndoto
zetu. Pia tunajaribiwa kuwaruhusu kunena zaidi ndani ya maisha yetu. Tunazingatia
maoni yao. Hii ndiyo sababu ni muhimu kusikia kutoka kwa Bwana na tuchague kwa
umakini uhusiano kulingana na maagizo Yake. Je, unaaminiwa na mviringo wako wa
ndani? Wao hukutia changamoto yakutembea juu ya maji ama wanakusababisha
kuangalia gharika
kando
yako? Pengine unastahili kuwachambua tena watu walio katika mashua yako uone
jinsi kila mmoja anavyokuadhiri na utengeze husiano zako vilivyo.
Ombi la Leo
Ewe Mungu, ninakuomba leo unipe
mawazo Yako kuhusu marafiki walio maishani mwangu. Ninakuomba unizingire na
watu waliojawa imani wenye maono na nia. Ninajua pia ya kwamba mimi ni sehemu
ya mviringo wa mtu vilevile, kwa hiyo unitumie niwe adhari nzuri na
niwasukumilie karibu na hatua zako kila wakati.
Maandiko ya Leo
1 Wakorintho 15:33 Msidanganyike!
Urafiki mbaya huharibu tabia njema.
Matendo ya Mitume 4:23 Mara tu
walipoachwa huru, Petro na Yohane walirudi kwa wenzao, wakawaeleza yale
waliyoambiwa na makuhani wakuu na wazee.
Mtihani wa kweli wa kuwa mtumishi ni jinsi
utakavyofanya wakati utachukuliwa kama mmoja
Watu wengi wangependa kutumika
na Mungu lakini sio kila mtu angependa kuandaliwa kwa matumizi. Pia, mara kwa
mara, fursa za huduma ambazo Mungu anatupatia zinahitaji ya kwamba tunyenyekee
na tuwe watumishi kwa wengine. Yesu alitupa mfano wa kuwa mtumishi wakati
alipoyaosha miguu ya wanafunzi Wake. Hii inatuonyesha ya kwamba hakuna aliyee
mkuu zaidi hata asifanyike mtumishi na hakuna nafasi iliyo ya juu zaidi ambayo
mtu hawezi kuiacha na kutumikia wengine. Ukweli ni kwamba, ukitaka kufanyika
mkuu katika Ufalme wa Mungu, ni lazime ufanyike mtumishi kwa wote. Kwahivyo,
tutajuaje kama tumemiliki roho ya unyenyekevu na hatujajawa na kiburi na mambo
ya kujiona wa muhimu zaidi? Jaribio la kweli la kuwa mtumishi ni vile
utakavyofanya ukifanyika kama mmoja. Unajisikiaje unapofanywa kuwatumikia
wengine? Ishughulikie.
Ombi la Leo
Baba, ninatamani kuwa na moyo
wa utumishi. Unapochagua kunitumia, nitakuwa mtumishi asiyelalamika, nikijua
kwamba lolote nifanyalo nitalifanya kama kukufanyia Wewe.
Maandiko ya Leo
Mathayo Mtakatifu 23:11-12 Naye
aliye mkubwa wenu atakuwa mtumishi wenu; na yeyeote atakayejikweza, atadhiliwa;
na yeyote atakayejidhili, atakwezwa.
Marko
Mtakatifu 10:43-45 Lakini kwenu isiwe hivyo, ila anayetaka kuwa mkuu kati yenu,
sharti awe mtumishi wenu. Anayetaka kuwa wa kwanza, sharti awe mtumishi wa
wote. Maana Mwana wa Mtu hakuja kutumikiwa, ila alikuja kutumikia, na kutoa
maisha yake kuwa fidia ya watu wengi."
Kuweza kuwajibika
Huenda ikawa uwezo wetu mkuu ni
jinsi tunavyoweza kupatikana, ambapo bila, uwezo wetu wote huenda usitumike.
Neno la Mungu linasema ya kwamba tukimwona ndugu anahitaji na tuna suluhisho la
kukutana na hilo hitaji, lakini, hatuguswi na huruma ya kusaidia, je, ni vipi
upendo wa Mungu unaweza kukaa ndani yetu? Ukiweka kwa njia rahisi, maandiko
yanasema ya kwamba kama tuna fursa na uwezo wa kushughulikia hitaji, na bado
tunakosa kushughulika, basi uwezo wetu umepotea kwa kukosa kuwajibika.
Wakati watu wengi wanaangalia
mamlaka, Mungu anawatafuta watu ambao wanawajibika. Mungu akimpata mtu ambaye
anawajibika, ambaye atakayejibu na uweza wake wa kukutana na mahitaji,
anawapatia mamlaka yote yanayohitajika kumaliza huduma hiyo. Ni jukumu la Mungu
kufungua milango na ni jukumu la mwanadamu kupita kwenye milango hiyo. Jibu
wakati unaweza.
Ombi la Leo
Baba, asante kwa kunifanya mimi
kuwa zaidi ya kuweza kukumbana na kila changamoto ya maisha na pia uwezo wa
kwenda sambamba na kuwasidia wengine katika mahitaji yao pia. Nitajifunza
kuegemea mkuu aliye ndani yangu na kukuza hali ya kuwajibika kuhusu kila kitu
maishani.
Maandiko ya Leo
Wafilipi 4:13 Nayaweza mambo
yote katika Yeye anitiaye nguvu.
1 Wakorintho 10:13 Majaribu
mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye
hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni
pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
Ufunuo wa Yohana 3:7 Kwa
malaika wa kanisa la Filadelfia andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka kwake
yeye aliye mtakatifu na wa kweli, ambaye anao ule ufunguo wa Daudi, na ambaye
hufungua na hakuna mtu awezaye kufungua.
Usipime kufaulu kwako kwa kila siku
Maisha
yamejaa fursa za kufurahisha kupita kiwango na tena fursa za kuhuzunisha kila
siku. Wakati mwingine tunajaribiwa kufanya uamuzi kulingana na hisia za wakati
huo. Niamini mimi, haijalishi ni nzuri ama mbaya kiasi gani, bado unaweza
kuichanganya ama kuiharibu kabisa unapoitenda wakati huo.
Ili uweze kuepuka hali zisizo
za kudumu na kutengeneza shida za kudumu, tunahitaji kukataa kuingiliana na
tabia za ketenda haraka. Hii inatuhitaji tupunguze mwenendo wa kujibu kulingana
na Neno la Mungu na tumpatie Mungu nafasi atusaidie katika mwenendo wa maisha.
Usipime kufaulu kwako kwa kila siku.
Ombi la Leo
Baba, nisaidie kuona maisha
kupitia macho Yako na kwa mtazamo wako, wala sio mtazamo wnagu. Ninaposhangazwa
na kile siku yangu inaleta, nitaweka huko kushangazwa miguuni pako kwa maombi.
Nionyeshe jinsi ya kujibu na uniweke salama.
Maandiko ya Leo
Yakobo 1:19 Ndugu zangu
wapenzi, kumbukeni jambo hili! Kila mtu na awe mwepesi wa kusikia lakini asiwe
mwepesi wa kusema wala mwepesi wa kukasirika.
Mhubiri 5:2 Usiseme maneno ya
ujinga kinywani mwako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu;
kwa maana, Mungu Yuko mbinguni, na wewe uko chini, kwa hiyo maneno yako yawe
machache.
Mhubiri 7:9 Usifanye haraka
kukasirika rohoni mwako, maana hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu.
Mithali 19:11 Busara ya mtu
huiahirisha hasira yake; nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
Wakolosai 3:15 Nayo amani ya
Kristo itawale mioyoni mwenu; maana kwa ajili hiyo ninyi mmeitwa katika mwili
huo mmoja. Tena muwe na shukrani!
Mungu haelekezi pale hatatwalia
Moja wapo ya majina ya Mungu
katika agano la kale ni Yehova Yire, haswa hili neno limeunganishwa na jina la
Mungu kumtambua kwa umakini kama Mtwaliwa wetu. Hata hivyo, maana yake haswa
ni, “katika mlima wa Bwana itaonekana”. Baba wetu wa imani, kwanza alimtambua
Mungu kama mmoja ambaye atafanya kutwaliwa kupatikane kwa mahali atakapochagua.
Kwa hali ya Ibrahamu, Mungu
alimuagiza
afunge safari kwa mlima fulani ambapo Ibrahamu alipata kutwaliwa kumemngojea
alipofika. Mambo haya hayakunakiliwa katika Biblia kutupasha tu safari ya
Ibrahimu, lakini kututia moyo hata nasi katika safari zetu. Wewe, kama
Ibrahamu, utapata kutwaliwa kumepeanwa na kuna kusubiri wewe katika kila hali
yako mbaya na kwenye safari yako na Mungu. Mungu haelekezi pale hatatwalia.
Mtumainie Bwana maana Yeye ni Yehova Yire.
Ombi la Leo
Nionyeshe njia Zako, Eeh Bwana
na unipe ufahamu wa barabara unayotaka nipitie. Nielekeze kwa njia yangu
iliyoteuliwa, ukinitwalia njiani. Naweka tumaini langu kwako kama chanzo
changu.
Maandiko ya Leo
Mwanzo 22:14 Ibrahimu akapaita
mahali hapo Yehova-Yire, kama watu wasmavyo hata leo, katika mlima wa Bwana
itapatikana.
Warumi 4:1 Tuseme nini basi,
juu ya Ibrahimu baba yetu?
Warumi 4:20-24 Ibrahimu
hakuionea mashaka ile ahadi ya Mungu; alipata nguvu kutokana na imani,
akamtukuza Mungu. Alijua kwamba Mungu anaweza kuyatekeleza yale aliyoahidi.
Ndiyo maana Mungu alimkubali kuwa mwadilifu. Inaposemwa,
"Alimkubali," haisemwi kwa ajili yake mwenyewe tu. Jambo hili
linatuhusu sisi pia ambao tunamwamini Mungu aliyemfufua Yesu, Bwana wetu,
kutoka wafu.
Mungu hakukusudia uhusiano wake na mwanadamu kuchukua
nafasi ya uhusiano wa mwanadamu na mwingine
Katika kitabu cha Mwanzo, Mungu
alimuumba binadamu kwa mfano wake mwenyewe na kumuweka kwenye shamba. Baadaye
Mungu akatazama yale yote aliyokuwa amefanya na akaona jambo moja ambalo halikuwa
zuri. Akasema, “Sio vizuri kwa mwanadamu kukaa peke yake.” Kwa hivyo Mungu
akamuumba mwanamke.
Ijapokuwa hakuna kina
kinachoweza kubadilishana uhusiano wako na Mungu, Mungu hakukusudia uhusiano
Wake na wewe kuchukua nafasi ya uhusiano wako na mtu mwingine. Anajua kwamba
watu wanahitaji watu. Tunahitajiana mmoja nao mwingine. Tumia wakati leo katika
uhusiano huo wa muhimu katika maisha yako…pamoja na Mungu na wapendwa wako.
Ombi la leo
Bwana,
nataka uhusiano wa kina wewe. Wewe ni wa muhimu sana maishani mwangu. Kwa
wakati huohuo, nataka kujenga na kufurahia uhusiano ulionipa na watu wengine.
Nisaidie kujua na kufuata kipaumbele katika uhusiano wangu. Asante.
Maandiko ya Leo
Mwanzo 2:18 Bwana Mungu
akasema, si vema huyu mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.
Waefeso 5:31 Kama yasemavyo
Maandiko Matakatifu: "Kwa hiyo, mwanamume atawaacha baba na mama yake,
ataungana na mkewe, nao wawili watakuwa mwili mmoja."
Mithali 18:24 Ajifanyiaye
rafiki wengi ni kwa uangamivu wake mwenyewe; lakini yuko rafiki aambatanaye na
mtu kuliko ndugu.
Mabadiliko yanakuja – upende
usipende, mabadiliko yanakuja Mabadiliko
huenda yakawa ni baadhi ya mambo yasiyotulia na wakati wa kushusha sana
maishani. Kutoka mahali pamoja hadi pengine, kazi moja hadi nyingine, ama
majira haya ya maisha hadi mengine, ni ukawaida wa maisha. Sio mabadiliko yote
ni mabaya, na wakati mwingi mabadiliko ni ya muhimu na hayaepukiki.
Imeshasemwa ya kwamba Mungu
anatupenda sana hata hawezi kutuacha jinsi tulivyo. Jambo moja ni la hakika,
mabadiliko yanakuja, upende usipende, mabadiliko yanakuja kwako. Ukikumbana na
mabadiliko maishani, kuwa mwepesi wa kubadilika, mwamini Mungu, na upate maono
ya siku kuu.
Ombi ya Leo
Mungu, nifunze kukumbatia
nyakati za mabadiliko ambayo ni muhimu na haziwezi kuepukika maishani. Niongoze
kupitia kutokuwa na uhakika kwangu na hali ya kujishuku na unipe maono Yako ya
siku bora kwa upande mwingine wa mabadiliko.
Maandiko ya Leo
Wafilipi 3:13-14 Ndugu,
sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kishika; ila natenda neneo moja tu;
nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo,
niifikilie mede ya dhawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Isaya
43:19 Tazama, nitatenda neno jipya; sasa litachipuka; je! Hamtalijua sasa?
Nitafanya njia jangwani, na mito ya maji nyikani.
Mungu anakutengenezea siku
za usoni na anatengeneza “wewe” kwa siku hizo za usoni Maandiko yanatufunilia ya kwamba Mungu
amejitoleakuendelea kufanya kazi nasi, kama vile mfinyanzi anafanya kazi na
udongo. Yeye anakumbana na kila jukumu la kila siku na kila hali ya maisha
kuleta kila mmoja wetu katika mfnao wa Mwanawe wa pekee, Bwana wetu na Mwokozi,
Yesu.
Mungu anatengeneza siku za
usoni kwako; halikadhalika anaumba uweza mkuu ndani yako wa kukumbatia siku za
usoni. Ni kwa sababu hii Mungu ameamuru mambo yote kutendeka kwa wema wetu. Na
ameunda misukumo ya maisha kutufanya kuwa bora, lakini sio watu wa machungu.
Kumbatia mfano ulio bora na uanze kujiona vile Mungu anavyokuona. Ota ndoto
zake maishani mwako na uwache akuumbe upya.
Ombi la Leo
Mungu, Baba yangu, nijenge mimi
na unipe milki…nipeleke katika siku za usoni ulizoniotea uliponiumba. Nisaidie
niwe wa kujengeka kuumbika katika mikono Yako. Fanyika kuwa mfinyanzi mkuu nami
nitakuwa udongo. Nifanye wa kufurahisha mbele zako.
Maandiko ya Leo
Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo
ndilo hili, ya kwamba Yeye aliyeanza kazi njema ndani yenu ataimaliza hata siku
ya Kristo Yesu.
Zaburi 138:8 Bwana atanitimilizia
mambo yangu; Ee Bwana, fadhili zako ni za milele; usiziache kazi za mikono
yangu.
1 Timothy 4:8 Mazoezi ya mwili
yana faida yake, lakini mazoezi ya kiroho yana faida za kila namna, maana
yanatuahidia uzima katika maisha ya sasa, na pia hayo yanayokuja.
Isaya 64:8 Lakini sasa, Ee
Bwana, wewe u Baba yetu; sisi tu udongo, nawe u mfinyanzi wetu; sisi sote tu
kazi ya mikono yako.
Jifunze kukimu makabiliano
badala ya kuyaepuka kila wakati Makabiliano
mara nyingi ni hatua ya muhimu kuelekea kuwa na umoja. Ni mara nyingi kwenye
mng’ang’ano tunauafikia uamuzi ulio bora nakufika kwenye makubaliano wakati
yaliyo bora yametambulika. Usiendelee kupitia maisha ukiogopa kukabiliana ya
kwamba utashindwa kutambua dhamana na manufaa ya
makabiliano.
Sio lazima tu tung’ang’ane na maadui zetu, lakini pia tuwatie nguvu marafiki
wetu, tupanue uhusiano wetu, na tutafute majibu ambayo hayajavumbuliwa kwa
changamoto za maisha. Tungelikuwa wapi sisi sote pamoja kama tungewachilia
mbali misukumo, ming’ang’ano, na ugumu wa kuzaa mtoto? Kumbuka, la muhimu
linapatikana wakati ambapo tunang’ang’ana tukitafuta ukweli, kando na
makabiliano. Jifunze kikimu makabiliano badala ya kuyaepuka kila wakati.
Ombi la Leo
Baba, nifunze kusimama imara,
kutokuogopa makabiliano ya maisha haya. Nipe neema ya kukimu muda wakati
mng’ang’ano ni muhimu kufikia kilele changu kwako. Usiruhusu makabiliano yalete
mgawanyiko lakini nitendeshe kazi mimi ili niwe na nguvu katika Jina la yesu.
Maandiko ya Leo
Mithali 27:17 Chuma hunoa
chuma; ndivyo mtu anunoavyo uso wa rafiki yake
1 Petro 4:12 Wapenzi wangu,
msishangae kuhusu majaribio makali mnayopata kana kwamba mnapatwa na kitu
kisicho cha kawaida.
2 Wakorintho 4:18 Hivyo
tunatazamia kwa makini si vitu vinavyoonekana, bali visivyoonekana. Maana vinavyoonekana
ni vya muda tu; lakini vile visivyoonekana ni vya milele.
Baraka zetu kuu maishani
huenda ikawa zinatungojea tuwe wa baraka kwa wengine Hadithi ya Ayubu, hata pia hadithi ya Yusufu, zote ni
mwelekeo ya kanuni hii ya kiungu maishani. Yusufu hangelipata kuachiliwa kutoka
korokoroni kama hangelichukua muda kuwa mkarimu na wa baraka kwa yule mkuu wa
kubeba kikombe cha Farao alipokuwa gerezani. Hata hivyo, Ayubu alijipata mahali
maishani ambapo alipoteza kila kitu. Katika sura ya mwisho iliyonakiliwa kwa
hesabu za Ayubu, tunasoma ya kwamba Bwana aligeuzwa utumwa wake wakati Ayubu
alwaombea marafiki wake.
Hata Mungu hakujitoa katika
kanuni ya ukweli huu. Unaona wakati Mungu alikuwa ametengwa kutokana na
maumbile yake, na mwanadamu alikuwa anaeleka kuzimu, Mungu alikuwa na njia moja
tu ya kufikia shauku Yake kuu. Ni nini ambayo ingembariki Mungu? Ilikuwa ni
kurudi kwa uhusiano sawa na mwanadamu. Hata hivyo, urejesho ulihitaji dhabihu.
Ili Mungu abarikiwe, ilimbidi kwanza awabariki wengine. Kwa hivyo Mungu
akamtuma Mwanawe wa pekee na akambariki mwanadamu kwa msamaha wa dhambi, na
baadaye Mungu
akabarikiwa
na watoto wengi. Baraka zetu kuu maishani huenda ikawa zinatungojea tuwe wa
baraka kwa wengine.
Ombi la Leo
Baba Mpendwa wa Mbinguni,
nauliza Roho Wako Mtakatifu anikumbushe katika lisaa langu kuu la hitaji ya
kwamba wengine pia wameketi kwenye mahitaji. Nisaidie nitazame tena maisha
yangu ili niwe wa baraka kwa wengine ninaposubiri baraka zako kwenye maisha
yangu na kazi.
Maandiko ya Leo
Waefeso 6:8 Kumbukeni kwamba
kila mtu mwenye kutenda mema, awe mtumwa au mtu huru, atapokea tuzo lake kutoka
kwa Bwana.
Mwanzo 12:2 Nami nitakufanya
wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka.
Wagalatia 6:7 Msidanganyike;
Mungu hafanyiwi dhihaka. Alichopanda mtu ndicho atakachovuna.
Wale hawataondoka
hawatabanduka Maisha yamejaa
mabadiliko…mambo yanaanza na mambo yanaisha. Mara nyingi tukifikia mwisho huu
tunatambua ni kuanza safari kwa hatua nyingine kuu ya shani zetu. Wakati
mwingine Mungu anatutuma kwenye barabara fulani kufika mwisho wa barabara hiyo
na wakati mwingine Mungu anatuelekeza kwenye barabara hiyo kufika kwenye njia
panda. Kwa hali zote mbili mabadiliko yanahitaji uamuzi wa ujasiri na kujitolea
rasmi.
Wakati mwingine maisha
yanatuhitaji tuachilie jambo moja kabla hatujashika lingine. Kuachilia siku
zilizopita maramara haisawazishwi na kuachilia watu wa siku zilizopita. Wakati
mwingi, inatubidi tu tuachilie siku zilizopita kwa kusamehe kuumizwa kwa roho,
kushushwa, na kuanguka. Hata hivyo, kuna nyakati ambazo zitatuhitaji kujitenga
kikamilifu kutokana na mtu binafsi ama kikundi cha watu kabla hatujakumbatia
siku mpya ambayo Mungu anataka kwa ajili yetu. Kuondoka ni nadra lakini mara
kwa mara kabla ya kubanduka, inawezekana.
Ombi la Leo
Bwana, ninaelewa ya kwamba ni
lazima niwachilie baadhi ya mambo ili niyashike mengine. Nionyeshe jinsi ya
kufanya hivyo. Ninataka kukufurahisha Wewe zaidi ya chochote ama mtu yeyote.
Nipe hekima ya kupambanua kinachohitajika katika mafikira yangu maishani
mwangu. Nitafuata hekima yako.
Maandiko
ya Leo
Waefeso 4:22-24 Basi, acheni
mwenendo wenu wa awali, yaani ule utu wenu wa kale uliokuwa unaangamizwa kwa
tamaa zake danganyifu. Jirekebisheni upya rohoni na katika fikira zenu. Vaeni
hali mpya ya utu ambayo imeumbwa kwa mfano wa Mungu na ambayo hujionyesha
katika maisha ya kweli ya uadilifu na utakatifu.
Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume
atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili
mmoja.
Mathayo 19:5 … na akasema: “Kwa
sababu hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake, ataungana na mke wake,
nao wawili watakuwa mwili mmoja”
Wakati mwingine msimu wetu wa maisha hututaka
tumtumainie Mungu katika wengine
Katika Mwanzo 22 Ibrahimu
aliambiwa amtwae mwanawe Isaka hadi mahali Mungu angemwonyesha na amtoe kama
thabihu kwa Mungu. Wakati huu isaka alikuwa na miaka kati ya 30 na 35. Ibrahimu
alimchukua isaka na kutembea kwa siku tatu kaskazini mwa Barsheba hadi mahali
ambapo hivi leo ni mji wa kale wa Yerusalemu. Ibrahimu aliweka kuni za thabihu
kwenye mabega ya Isaka na wakaushuka mlima ambao Mungu alimwonyesha Ibrahimu.
Hadithi inaendelea ambapo Ibrahimu akimfunga mwanawe kwa kamba, akiweka kuni
katika madhabahu mapya na kumweka isaka tayari kumtoa kama kama dhabihu.
Waebrania 11 inasema kuwa Ibrahimu alimtumainia Mungu… lakini Isaka
alimtumainia nani?
Isaka alimhoji babake na
akasikia jibu la babake kisha akamkubali babake amfunge na kumtayarisha ili
amtoe kama dhabihu. Katika haya yote Isaka alimtumainia Mungu katika Ibrahimu
ingawa Isaka hakusikia kwa uhalisi kutoka kwa Mungu. Wakati mwingine misimu
yetu na hali zetu za maisha hututaka tumtumainie Mungu katika wengine.
Ombi la leo.
Ewe baba wa Mbinguni, nisaidie
kupambanua nyakati na misimu ya maisha inayonitaka nikutumainie katika na
kupitia zingine. Nipe neema ya kukubali uongozi unaonitumia na nikakubali
uniongoze katika nyakati hizi kulingana na mapenzi yako.
Maandiko ya leo.
Mwanzo 22:7-9 Isaka akasema na
Ibrahimu baba yake, akinenea, Babangu! Naye akasema, Tazama! Moto upo, na kuni
zipo, lakini yuko wapi mwana-kondoo kwa sadaka ya kuteketezwa? Ibrahimu
akasema, Mungu atajipatia mwana-
kondoo
kwa hiyo sadaka,mwanangu. Basi wakaendelea wote wawili pamoja. Wakafika mahali
pale alipoambiwa na Mungu, Ibrahimu akajenga madhabahu huko, akziweka tayari
kuni, kasha akamfunga Isaka mwanawe, akamweka juu ya madhabahu, juu ya zile
kuni.
Waebrania 11:17 Kwa imani,
Ibrahamu alimtoa mwanae Isaka sadaka wakati Mungu alipomjaribu. Huyo Abrahamu
ndiye aliyekuwa amepokea ahadi ya Mungu, lakini, hata hivyo, alikubali kumtoa
dhabihu mwanae wa pekee,
Sio kila wakati kila
aliyeadhirika husikia kutoka kwa Mungu
Kama tulivyojadiliana katika
funzo la jana, Ibrahimu alisikia kutoka kwa Mungu eti amtoe mwanawe Isaka kama
dhabihu… Isaka alisikia kutoka kwa Ibrahimu tu. Hatuna njia ya kujua kama isaka
alisikia sauti kutoka mbinguni ikimwambia Ibrahimu abadilishe mipango yake na
asimtoe mwanawe Isaka kama dhabihu. Hata hivyo kuna matukio mengine mengi
ambapo si kila aliyeathirika alisikia kwa uhalisi kutoka kwa Mungu. Hivyo
ndivyo ilivyokuwa katika kisa cha Samweli ambaye akiwa mvulana mdogo alisikia
sauti ya Mungu ikiliita jina lake na kunena ujumbe ilhali Eli kuhani mzee
hakusikia.
Mungu humnenea anayetaka na
wakati mwingine si kila aliyeathirika kwa sauti hiyo huisikia sauti hiyo.
Mruhusu Mungu achague yule anayetaka kutumia, na bila shaka wakati mwingine
utasikia kutoka kwa Mungu; na wakati mwingine utasikia kutoka kwa wengine ambao
Mungu amewachagua kunena.
Ombi la leo.
Ewe Baba wa Mbinguni, nipe
neema ya kukutumainia ninaposikia ukinizungumzia na pia nikutumainie kupitia
uongozi wa wengine uliowaweka maishani mwangu. Ninajua sauti yako haiwezi
kukiuka Neno Lako. Nifunze Neno Lako Ewe Bwana.
Maandiko ya leo.
1 Samweli 3:9, 10, 11, 15 Kwa
hivyo, Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena
Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali
pake. Bwana akaja, akasimama, akaita vile vile kama kwanza, Samweli! Samweli!
Ndipo Samweli akasema, Nena, Bwana; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Bwana
akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila
atakayelisikia masikio yake yatamwasha. Naye Samweli akalala hata asubuhi,
akaifungua milango ya nyumba ya Bwana. Samweli akaogopa kumjulisha Eli maono
hayo.
Usiwahi kudunisha nguvu za maono
Mara nyingi watu huacha kuona
siku zao za usoni kwa sababu ya hali wanayopitia. Wingu la kuchanganyikiwa na
misimu ya kufadhaika hufanya kazi ya kutunyang’anya tumaini letu kwa ajili ya
siku zetu za usoni. Katika nyakati hizi za kuchanganyikiwa hakuna kitu
kitakachonyoosha maisha kama kuwa na maono kwa siku kuu. Hata kama tunakumbana
na jaribio gumu maishani au kupitia
mabadiliko
ya misimu ya maisha, tumaini kwa siku za kesho zilizo bora zaidi ndio ufunguo
wa sisi kusonga mbele kwa mwito ulio imara. Usikubali uvuli wa wakati ukufungie
katika wakati huo. Angalia mbele na umuulize Mungu akupe maono ya kesho kama
alivyokupangia.
Usiwahi kudunisha nguvu za maono.
Itakurejeshea furaha, ikupe nguvu, na ikuongoze katika mabonde ya maisha.
Usisahau, siku yako kuu zaidi ingali mbele.
Ombi la leo.
Ewe Mungu, ninaomba unipe maono
ya yale umenipangia katika siku zangu za usoni. Nitembelee wakati wangu wa
usiku na uninenee kwa kupitia maono na ndoto. Nitie nguvu na unipe furaha
unaponiongoza kwa ukuu wangu kwa roho wako mtakatifu.
Maandiko ya leo.
Zaburi 126:1 Bwana
alipowarejeza mateka wa Sayuni, tulikuwa kama waotao ndoto.
Ayubu 33:14-16 Kwa kuwa Mungu
hunena mara moja, naam, hata mara ya pili, ajapokuwa mtu hajali. Katika ndoto,
katika maono ya usiku, usingizi mzito uwajiliapo watu, katika usingizi
kitandani; ndipo huyafunua masikio ya watu, na kuyatia muhuri mafundisho yao.
Matendo ya Mitume 2:17 `Katika
siku zile za mwisho, asema Bwana, nitawamiminia binadamu wote Roho wangu.
Watoto wenu, wanaume kwa wanawake, watautangaza ujumbe wangu; vijana wenu
wataona maono, na wazee wenu wataota ndoto.
Mithali 29:18 Pasipo maono,
watu huacha kujizuia; bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.
Mungu ni Mungu wa “nitumainie, nijaribu, na
unithibitishe”
Mungu ni wa umilele, si mwenye
nguvu zote tu, bali wa umilele. Mungu hawezi kutiwa majaribuni au hawezi
kushawishiwa kujibu maswali yetu. Ilhali amejitolea kujithibitisha kwa wana
wake ili tuwe na ujasiri mkubwa katika neno lake na tuongeze imani yetu kwake.
Kupitia chaguo kuu la Mungu amesema kuwa tunaweza kumjaribu na tuone kama
hatatenda neno lake kwa niaba yetu.
Andiko moja kama hili katika
Malaki hushughulikia zaka na sadaka zetu. Amua leo kuwa utamtumainia Mungu
umjaribu na umkubali athibitishe uaminifu wake kwa niaba yako. Inaanza
unapotumia neno la Mungu katika hali zako za maisha. Mjaribu leo.
Ombi la leo.
Bwana,
wewe pekee ndiwe Mungu na hakuna mwingine kando na wewe. Asante kwa kunipenda
na kunijali. Katika mambo yote nitakutumainia kupitia kwa neno lako. Nionyeshe
unachotaka nifanye nami nitafanya. Imani yangu ikuavyo, nifunze kushiriki
shuhuda hizo na wengine.
Maandiko ya leo.
Malaki 3:10 Leteni zaka kamili
ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo,
asema Bwana wa majeshi; mjue kama sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na
kuwamwagieni baraka hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.
Zaburi 9:10 Nao wakujuao jina
lako wakutumaini Wewe, maana Wewe, Bwana, hukuwaacha wakutafutao.
Zaburi 56:11 Nimemtumaini
Mungu, sitaogopa; mwanadamu atanitenda nini?
Kama Mungu si namba moja katika siku yako, yawezekana
yeye si namba moja maishani mwako.
Maisha yana shughuli nyingi na
siku hujazwa haraka na majukumu yanayotumia muda wetu. Siku hupita na kugeuka
kuwa majuma na majuma kuwa miezi kabla tugundue. Mara nyingi inaonekana kuna
wakati mdogo wa kutulia na kufurahia mambo madogo ya maana ya maisha.
Tusipokuwa waangalifu, uhusiano
wetu na Mungu unaweza kuwa moja ya zile zitakazoumia. Ni rahisi sana kumzima,
kulegea katika tabia zetu za maombi na kupatia masomo ya Neno la Mungu mahali
pake sawa katika siku yetu. Hata hivyo, kama Mungu si namba moja katika maisha
yako yaweza kujadiliwa kuwa huenda ikawa yeye si namba moja maishani mwako.
Fanya mabadiliko sasa. Weka nadhiri ya kuanza kila siku na Mungu.
Ombi la leo.
Baba, nisamehe pale ambapo
sikukujumulisha katika wakati muhimu wa siku yangu. Nikumbushe kila asubuhi ya
kuwa unaningoja nitumie wakati wako nawe. Fungua hazina za ufalme wako kwangu
tunapoangalia neno lako pamoja. Sikia ombi langu, ewe Mungu. Ninakupenda.
Maandiko ya leo.
Mwanzo 19:27 Ibrahimu akatoka
asubuhi kwenda mahali aliposimama , mbele za Bwana.
Marko 1:35 Kesho yake, kabla ya
mapambazuko, Yesu alitoka, akaenda mahali pa faragha kusali.
Mithali
8:17 Nawapenda wale wanipendao na wale wanitafutao kwa bidii wataniona.
Msaada mara nyingi uko hatua moja tu ya uamuzi mgumu
Nimesikia inasemekana kuwa kama
pesa zinaweza kuitengeneza, wakati waweza kuitengeneza, ama kama ni uamuzi
mgumu, si shida bali ni fursa. Hata hivyo kuna hali zingine ambazo zaweza
kutatuliwa tu kwa kufanya uamuzi ambao ni mgumu kufanya. Hii ndiyo iliyokuwa
hali ya Mungu alipokumbana na hali ya kutengana milele na wanadamu. Hakuna
kiasi cha pesa ambacho kingesuluhisha na wakati bila suluhisho ungefanya hali
hiyo ngumu zaidi. Suluhisho pekee la shida ya Mungu lilikuwa kumtuma mwanawe
kama mtoto, akazaliwa katika hori la ng’ombe kule Bethlehemu, hatima yake ikiwa
kukataliwa, kuumizwa, kuchapwa, na kusulubiwa, yote hayo kwa dhambi ambazo
hakufanya. Huu ulikuwa uamuzi mgumu lakini hakukuwa na msaada na hakuna
mwingine ambaye angeufanya uamuzi huu ila Mungu. Ingawa hakuna kafara nyingine
itahitajika, tunakumbana na hali ambazo haziwezi kutatuliwa bila ya sisi
kufanya uamuzi mgumu. Kubali ukweli, msaada mara nyingi uko hatua moja tu ya
uamuzi mgumu ... na huenda ukawa ni wewe pekee unayeweza kuisuluhisha.
Ombi la leo.
Ewe Bwana, nisaidie kuchukua
jukumu langu kwa kumaanisha na nifahamu kuwa kuna vitu vingine ambavyo mimi tu
ndiye ninayeweza kusuluhisha. Nisaidie kukumbana na kufanya uamuzi ufaao hata
kama ni mgumu.
Maandiko ya leo.
Isaya 53:3-5 Alidharauliwa na
kukataliwa na watu; mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; na kama mtu ambaye
watu humficha nyuso zao, alidharauliwa na wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika
ameyachukua masikitiko yetu, amejitwika huzuni yetu; lakini tulimdhania ya kuwa
amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, alichubuliwa
kwa makos ayetu; adhabu ya amni yetu ilikuwa juu yake, na kwa kupigwa kwake
sisi tumepona.
Kumbukumbu la Torati 30:19
Nazishuhudiza mbingu na nchi juu yenu hivi leo, kuwa nimekuwekea mbele yako
uzima na mauti, baraka na laana; basi chagua uzima, ili uwe hai, wewe na uzao
wako.
Mungu huwapa watu kupitia watu
Usiku kabla ya Krismasi Mungu
alikuwa ameshajitayarisha kupeana zawadi yake kuu… zawadi ya wokovu. Mungu
alichagua vipi kuipeana zawadi yake kuu? Alichagua kuuleta wokovu kwa wanadamu
kupitia Yesu wa Nazareti. Mara nyingi Mungu anapotaka kazi ifanywe mwana huzaliwa.
Kwa nini? Kwa sababu Mungu amechagua kuwapa watu kupitia watu. Hata kama Yesu
ni Mwana wa Mungu yeye pia ni mwana wa mwanadamu na ni kupitia kwa utu wake
ndiyo Yesu alilipa deni na kuleta zawadi ya Mungu.
Kanuni
hii yaendelea kupitia maandiko na maisha. Kama Mungu anatamani kukubariki yeye
mara nyingi huchagua kutuma Baraka hizo kupitia mtu mwingine. Unaona, Mungu
mara nyingi hawezi kukupa kile hawezi kupeana kukupitia. Mungu anataka
kuwabariki wengine leo… anaweza kukutumaini? Je Mungu akikubariki utawabariki
wengine? Wacha Mungu ajue kuwa u tayari kupeleka zawadi yake kwa mtu mwenye
hitaji leo.
Ombi la leo.
Mungu, ninakushukuru kwa Mwanao
Yesu na kwa zawadi ya wokovu aliyoniletea. Nitumie, Bwana, kuwasilisha zawadi
yako kwa wengine wanaoihitaji. Nibariki na unifanye niwe baraka. Nipe na
unitumie kuwapa wengine katika jina la Yesu. Amina.
Maandiko ya leo.
Luka 6:38 Wapeni wengine
wanavyohitaji, nanyi mtapewa. Naam, mtapokea mikononi mwenu kipimo kilichojaa,
kikashindiliwa na kusukwasukwa hata kumwagika. Kwa maana kipimo kilekile
mnachotumia kwa wengine ndicho ambacho Mungu atatumia kwenu."
Mwanzo 12:2 Nami nitakufanya
wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza jina lako; nawe uwe baraka
Luka 19:8 Lakini Zakayo
akasimama akamwambia Yesu, "Sikiliza Bwana! Mimi nitawapa maskini nusu ya
mali yangu, na kama nimenyang`anya mtu yeyote kitu, nitamrudishia mara
nne."
Mapenzi ya Mungu kwako ni mazuri.
Hivi leo, Wakristo wengi
husherehekea kuzaliwa kwa Bwana wetu Yesu, Masihi wa Wayahudi na Mwokozi wa
ulimwengu. Usiku ambao Yesu alizaliwa malaika waliwatokea wachungaji katika
viwanja vya Bethlehemu wakitangaza mapenzi ya Mungu kwa ulimwengu uliopotea na
unaoumia. Juu ya haya yote usiku huo mzuri kulikuwa na ufunuo ulioletwa na
malaika kwa wanadamu. Malaika waliimba, “amani duniani na mapenzi ya Mungu kwa
wanadamu.”
Ingawaje siwezi kukuambia Mungu
amekuwekea nini au njia anayoweza kukuongoza, ninaweza kutangaza kuwa mapenzi
ya Mungu kwako ni mazuri. Hana hasira, Hamtakii yeyote mabaya au kuwa na wivu kwa
mwanadamu. Yesu, Mwana wake, aliyezaliwa na bikira katika mji wa Bethlehemu
alionyesha ulimwengu kuwa kile Mungu anatutakia ni kwa uzuri wetu. Mtumainie
huyu Mungu mzuri na mpango wake mzuri kwa maisha yako kwa kumkubali huyu Yesu
kama Bwana na Mwokozi.
Ombi la leo.
Ewe
Baba wa Mbinguni, leo ninakushukuru kwa kumtuma Mwanao Yesu duniani. Ninaamini
alizaliwa na bikira, akaishi maisha yasiyo ya dhambi, na akafa kifo cha uchungu
na aibu. Ninaamini kile malaika walitangaza na ninaweka nadhiri kuwa nitawaeleza
wengine habari hii njema.
Maandiko ya leo.
Luka 2:10-14 Malaika
akawaambia, "Msiogope! Nimewaleteeni habari njema ya furaha kuu kwa watu
wote. Kwa maana, leo hii katika mji wa Daudi, amezaliwa Mwokozi kwa ajili yenu,
ndiye Kristo Bwana. Na hiki kitakuwa kitambulisho kwenu: mtamkuta mtoto mchanga
amevikwa nguo za kitoto, amelazwa horini." Mara kundi kubwa la jeshi la
mbinguni likajiunga na huyo malaika, wakamsifu Mungu wakisema: "Utukufu
kwa Mungu juu mbinguni, na amani duniani kwa watu aliopendezwa nao!"
Msamaha wa dhambi si kibali cha dhambi
Yesu, Mwana wa Mungu, Masihi wa
Wayahudi na Mwokozi wa Ulimwengu alizaliwa na bikira katika mji wa Bethlehemu,
aliishi maisha yasiyo na dhambi na kufa kifo cha uchungu na aibu. Dhabihu yake
msalabani Kalvari ililipa milele dhambi za wanadamu. Yesu alikufa kuokoa roho
zetu kutoka kuzimu ya milele na kutokana na kuzimu ya maisha haya. Alitukomboa
kutokana na nguvu ya dhambi ya kuangamiza roho zetu milele na kutokana na nguvu
za dhambi za kutawala maisha yetu kwa muda. Msamaha wa Mungu kupitia damu ya
Yesu, ikitumika mara moja, imekamilika. Hakumbuki dhambi zilizosamehewa;
anazitupilia nyuma yake; anaziangusha katika bahari la sahau; na kuzitoa zetu
kama vile mashariki ilivyo mbali na magharibi. Mungu baba, alimwekea Yesu,
Mwana, makosa yetu yote na tumesamehewa. Hata hivyo, msamaha wa dhambi si
kibali cha kutenda dhambi.
Ombi la leo.
Baba, watu wote wamefanya
dhambi na kupungukiwa na utukufu wako na mshahara wa dhambi ni mauti bali
karama yako ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Nisamehe dhambi,
nioshe kutokana na kutokuwa mwenye haki na unipe neema yakutembea huru kutokana
na mshiko utawala wake.
Maandiko ya leo.
Warumi 6:14 Maana, dhambi
haitawatawala ninyi tena, kwani hamko chini ya Sheria, bali chini ya neema.
Warumi 10:13 Maana Maandiko
Matakatifu yasema: "Kila mtu atakayeomba kwa jina la Bwana,
ataokolewa."
Isaya
53:6 Sisi sote kama kondoo tumepotea; kila mmoja wetu amegeukia njia yake
mwenyewe; na Bwana ameweka juu yake maovu yetu sisi sote.
Zaburi 25:11 Ee Bwana, kwa
ajiliya Jina lako, unisamehe uovu wangu, maana ni mwingi.
Isaya 55:7 Mtu mbaya na aache
njia yake, na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana, naye
atamrehemu; na arejee kwa Mungu wetu, naye atamsamehe kabisa.
Ulichofanya kupata kitu ndicho unachohitaji kufanya
kwa ujumla ili ukiweke
Yohana alipoandika kitabu cha
Ufunuo, Yesu alimnenea kuhuhu Kanisa la Efeso. Hili lilikuwa kanisa zuri
lililofanya kazi, lilikuwa na mazao, lilikuwa na uvumilivu, lilichukia maovu,
na lilichunga dini. Yote haya waliyafanya bila kuchoka kwa ajili ya Yesu na
Jina Lake. Hata hivyo, Yesu alikuwa na jambo moja dhidi yao: walikuwa wameuacha
upendo wao wa kwanza. Je, Yesu alikuwa akizungumzia nini? Alikuwa akisema
kanuni ambayo misingi ya Kikristo haitabadilika na haijalishi tuna mazao kiasi
gani ama tunahusika kiasi gani kama tumeunganishwa kwa mtiririko wa maisha wa
uhusiano unaotokana na uhusiano wa ndani na yesu, kazi zetu zote ni bure. Ni
sawa na kila uhusiano, hata ndoa na/au kazi yako. Ulichofanya kupata kitu
ndicho unachohitaji kufanya kwa ujumla ili ukiweke. Rudi kwa misingi na
usiusahau upendo wako wa kwanza.
Ombi la leo.
Baba Mungu, nionyeshe makosa na
motisha ya kweli ya moyo wangu. Nisaidie nisiusahau upendo wangu wa kwanza na
nilichofanya ili nifike nilipo. Nifunze kudhamini misingi ya maisha na uhusiano
ninapoendelea kuutumikia Ufalme wako.
Maandiko ya leo.
Ufunuo wa Yohana 2:1-5
"Kwa malaika wa kanisa la Efeso andika hivi: "Huu ndio ujumbe kutoka
kwake yeye ashikaye nyota saba katika mkono wake wa kulia, na ambaye hutembea
katikati ya vinara saba vya taa vya dhahabu. Najua mambo yako yote; najua bidii
yako na uvumilivu wako. Najua kwamba huwezi kuwavumilia watu waovu, na kwamba
umewapima wale wanaojisemea kuwa mitume na kumbe sio, ukagundua kwamba ni
waongo. Wewe unayo saburi, umestahimili taabu nyingi kwa ajili ya jina langu,
wala hukuvunjika moyo. Lakini ninayo hoja moja juu yako: wewe hunipendi tena
sasa kama pale awali. Basi, pakumbuke pale ulipokuwa kabla ya kuanguka,
ukayaache madhambi yako, na kufanya kama ulivyofanya pale awali. La sivyo, naja
kwako na kukiondoa kinara chako mahali pake.
Hakuna awezaye kupewa kamili hadi avunjike kamili
Mungu
huwapinga wajikuzao bali huwapa neema wanyenyekevu. Unyenyekevu ni kujua kila
wakati kuwa tunamtegemea Mungu. Mara nyingi katika injili zote, Yesu anaonekana
akitwaa mkate, akiubariki kisha kuumega kabla ya kuupeana. Kanuni hii
inatunenea kuhusu mpangilio wa Mungu maishani mwetu. Mkono wa thamani wa Mungu
utuchukuao na kutusongeza karibu naye ndio mkono wa upendo unaotubariki. Kwa
watu wengi huu ndio umbali watakaomkubali Mungu kuhusiana nao. Hata hivyo ili
upewe kamili yafaa umruhusu Mungu huyo anayejali aingie ndeni ya kina cha
maisha yako. Anajua kilicho ndani ya mwanadamu na anajua unachoweza. Mungu
anataka kukuchukua na anataka kukubariki lakini anataka kukuvunja ili upeanwe.
Wale wawili njiani wakielekea Emau walitoa ushuhuda kwa wanafunzi wengine
wakisema, “tulimtambua katika kuumega mkate.” Usife moyo Mungu anapoanza
kushughulikia kiburi chako au dhambi zingine kuu maishani mwako. Makusudi yake
ni kukupeana.
Ombi la leo.
Ewe Bwana, kuwa mwenye rehema
kwangu na ukumbuke mimi si kitu ila vumbi tu. Usinipige kwa kutoridhika kwako,
lakini chukua maisha yangu, bariki maisha yangu, vunja maisha yangu katika
mikono Yako miepesi, unapopenda, ili unipeane kama unavyohitaji katika jina la
Yesu. Amina.
Maandiko ya leo.
Yohana 2:25 … Hakuhitaji
kuambiwa chochote juu ya watu, maana aliyajua barabara mambo yote yaliyomo mioyoni
mwao.
Luka 24:35 Basi, hao wafuasi
wawili wakawajulisha yale yaliyowapata njiani, na jinsi walivyomtambua katika
kumega mkate.
Mathayo 26:26 Walipokuwa
wanakula, Yesu akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa wanafunzi wake
akisema, "Twaeni mle; huu ni mwili wangu."
Yakobo 4:6 Lakini, neema
tunayopewa na Mungu ina nguvu zaidi; kama yasemavyo Maandiko: "Mungu
huwapinga wenye majivuno lakini huwapa neema wanyenyekevu."
Kama ni mbaya Mungu hajamaliza bado
Waweza kuwazia, kutokana na
mtazamo wa binadamu, jinsi ilivyoonekana vibaya kwa Yesu alivyotazama msalaba
kuadhibiwa kwa makosa ambayo hakutenda? Hakika, alinakiri kutoka Zaburi 22
alipoangikwa msalabani akisema, “Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha?”
Yusufu huenda alikuwa na hisia hizo wakati mwingi na hata pia Ayubu, Paulo,
Petro, Mariamu na watakatifu wengine wengi katika Biblia.
Kumbuka,
imani ni kuamini ya kuwa haijalishi tuliko au tunakabiliana na nini maishani,
Mungu yu kwenye usukani. Chukua nguvu na imani leo kutoka kwa hadithi za
watakatifu waliothihirishwa kwetu katika Maandiko na ujue kama ni mbaya Mungu
hajamaliza bado!
Ombi la leo.
Mungu, nisaidie kugundua kuwa
Hakuna lilio gumu kwako. Ninajua kuwa maisha yangu na wakati wangu u kwako na
mazuri yangali yaja!
Maandiko ya leo.
Warumi 8:28 Tunajua kwamba,
katika mambo yote, Mungu hufanya kazi na kuifanikisha pamoja na wote wampendao,
yaani wale aliowaita kufuatana na kusudi lake.
Yohana 16:33 Nimewaambieni
mambo haya ili mpate kuwa na amani katika kuungana nami. Ulimwenguni mtapata
masumbuko; lakini jipeni moyo! Mimi nimeushinda ulimwengu!"
Mungu huzungumza kupitia hatima
Mungu alipomwambia Musa
kuwakomboa wanawe kutoka bonde la Misri, alimtuma Musa na ujumbe kutoka
mbinguni. Ujumbe Musa alionena kwa niaba ya Mungu kwa wana wa Israeli ulikuwa
sambamba kabisa: “Nitawakomboa kutoka Misri na kuwapeleka katika nchi ya ahadi
ya maziwa na asali.” Mungu alipomtuma nabii Samweli kumpaka mafuta kijana mdogo
Daudi ili awe mfalme wa Israeli yote, alimnenea Daudi kupitia nabii kuhusu
hatima yake kuu ya kuwatawala wana wa Mungu. Yesu alipokutana na wanafunzi wake
wa kwanza ufuoni mwa Galilaya aliwaita kwa kuwaambia, “Njooni mnifuate nami
nitawafanya kuwa wavuvi wa watu.”
Maneno haya yote ya Mungu
yanawanenea wanadamu kuhusu hatima bila kuashiria safari ndefu, ngumu na
inayogharimu ili mtu afike hatima ile. Mungu hutunenea kuhusu hatima, kisha
hutembea nasi safarini tukielekea hatima hiyo. Maisha ni safari…na ukiwa na
Mungu safari ni rafiki yako.
Ombi la leo.
Mungu, nipe hekima ya kukubali
mapenzi yako kwa maisha yangu na nguvu za kutembea njia yako kwa mapenzi hayo.
Amina.
Maandiko ya leo.
Wagalatia 6:9 Basi, tusichoke
kutenda mema; maana tusipolegea tutavuna mavuno kwa wakati wake.
Hesabu
21:4 Wakasafiri kutoka mlima wa Hori kwa njia ya Bahari ya Shamu; ili
kuizunguka nchi ya Edomu, watu wakafa moyo kwa sababu ya ile njia.
Mathayo 4:19 Basi, akawaambia,
"Nifuateni, nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."
Siku yako kuu haitakuja hadi ushinde jaribio lako kuu
Kama ilivyo na kuzaliwa kwa
kila kitu, kuanzia wanadamu, kupitia ufalme wa wanyama, na hata mbegu
tunazopanda, maisha huanza kwa mng’ang’ano. Siku baada ya siku, mwaka baada ya
mwaka, maisha huendelea kutiwa nguvu tunaposukuma kinyume na nguvu zinazopinga
ukuaji wetu na kujaribu kutushikilia nyuma. Mng’ang’ano ni sehemu ya maisha
inayoendelea kwa maana ni kupitia kwa mng’ang’ano ndipo tunatiwa nguvu. Yakobo
aling’ang’ana na malaika, Paulo na mambo yake ya kale, na Yesu na hatima yake.
Katika kila mng’ang’ano wake kwa waume walioshinda na kunyakua ushindi katika
hali hizo ni wale ambao pia wanaenda mbele na kunyakua ushindi dhidi ya hali
hizo. Usifadhaike maisha yajapo kukujaribu na kumbuka kuanguka si kushindwa.
Kwa maana mwenye haki huanguka mara saba akaondoka tena. Pigana vita vizuri vya
imani. Jitie nguvu katika vita na ukumbuke kuwa siku yako kuu haitakuja hadi
ukabiliane na ushinde jaribu lako kuu.
Ombi la leo.
Baba, Neno lako Linasema kwamba
nikizimia katika siku ya majaribu basi nguvu zangu ni kidogo. Nakuomba
unifanyishe mazoezi, uninyooshe na unifanye kuwa sambamba kwa kunipa majaribu
ninayoweza kukabiliana nayo maishani, si magumu sana, si rahisi sana, lakini
inayotoshana na wakati na kiwango cha maisha yangu ili nikue. Nifunze njia
zako.
Maandiko ya leo.
Mithali 24:16 Kwa maana mwenye
haki huanguka mara saba akaondoka tena; bali wasio haki hukwazwa na mabaya.
1 Timotheo 6:12 Piga mbio
kadiri uwezavyo katika shindano la mbio za imani, ukajipatie tuzo la uzima wa
milele, uliloitiwa wakati ulipokiri imani yako mbele ya mashahidi wengi.
1 Wakorintho 10:13 Majaribu
mliyokwisha pata ni ya kawaida kwa binadamu. Mungu ni mwaminifu, naye
hataruhusu mjaribiwe kupita nguvu zenu, ila pamoja na majaribu, yeye atawapeni
pia nguvu ya kustahimili na njia ya kutoka humo salama.
2 Wakorintho
4:17 Taabu tunayopata ni kidogo, tena ya muda tu: lakini itatupatia utukufu
upitao matazamio yote, utukufu ambao hauna mwisho.
Comments
Post a Comment