Sababu Arobaini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Kwanza ya Juma
1. Kitu cha kwanza kabisa kilichowekwa kwenye kumbukumbu za Biblia ni kazi iliyofanywa siku ya Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Mwanzo 1:1-5. Hii ilifanywa na Mwumbaji mwenyewe. Ikiwa Mungu aliumba dunia siku ya Jumapili, je itakuwa ni vibaya kwetu kufanya kazi siku ya Jumapili? 2 . Mungu anawaamuru watu kufanya kazi siku ya kwanza ya juma. Kutoka 20:8-11. Je, ni makoa kumtii Mungu? 3. Hakuna hata mzee wa zamani aliyepata kuitunza. 4. Hakuna hata manabii watakatifu waliopata kuitunza. 5. Kwa amri iliyofafanuliwa ya Mungu, watu wake watakatifu walitumia siku ya kwanza ya juma kama siku ya kawaida ya kufanya kazi kwa miaka 4,000, angalao. 6. Mungu mwenyewe huiita “siku ya” kufanya kazi. Ezekieli 46:1. 7. Mungu hakupumzika katika siku hii. 8. Hakuibariki kamwe. 9. Kristo hakupumzika katika siku hii. 10. Yesu alikuwa seremala ( Marko 6:3 ) na akafanya shughuli hiyo mpaka alipokuwa na miak...