Sababu Arobaini za Biblia Kuhusiana na Siku ya Kwanza ya Juma

1. Kitu cha kwanza kabisa kilichowekwa kwenye kumbukumbu za Biblia ni kazi iliyofanywa siku ya Jumapili, siku ya kwanza ya juma. Mwanzo 1:1-5. Hii ilifanywa na Mwumbaji mwenyewe. Ikiwa Mungu aliumba dunia siku ya Jumapili, je itakuwa ni vibaya kwetu kufanya kazi siku ya Jumapili?
2. Mungu anawaamuru watu kufanya kazi siku ya kwanza ya juma. Kutoka 20:8-11. Je, ni makoa kumtii Mungu?
3. Hakuna hata mzee wa zamani aliyepata kuitunza.
4. Hakuna hata manabii watakatifu waliopata kuitunza.
5. Kwa amri iliyofafanuliwa ya Mungu, watu wake watakatifu walitumia siku ya kwanza ya juma kama siku ya kawaida ya kufanya kazi kwa miaka 4,000, angalao.
6. Mungu mwenyewe huiita “siku ya” kufanya kazi. Ezekieli 46:1.
7. Mungu hakupumzika katika siku hii.
8. Hakuibariki kamwe.
9. Kristo hakupumzika katika siku hii.
10. Yesu alikuwa seremala (Marko 6:3) na akafanya shughuli hiyo mpaka alipokuwa na miaka 30. Aliitunza Sabato na kufanya kazi kwa siku sita katika juma, kama wote wanavyokiri. Hivyo basi alifanya kazi nyingi ngumu za siku ya Jumapili.
11. Mitume walifanya kazi katika siku hii wakati wa kipindi hiki hiki.
12. Mitume kamwe hawakupumzika katika siku hiyo.
13. Kristo kamwe hakuibariki.
14. Haijapata kubarikiwa kwa mamlaka yoyote ya Mungu.
15. Haijapata kutakaswa kamwe.
16. Hakuna sheria iliyopata kutolewa kulazimisha kuitunza [Jumapili], hivyo basi hakuna dhambi kufanya kazi katika siku hiyo. “Maana pasipokuwapo sheria, hapana kosa.” Warumi 4:15; (1 Yohana 3:4).
17. Hakuna mahali popote ambapo Agano Jipya hukataza kazi kufanyika siku ya Jumapili.
18. Hakuna adhabu inayotolewa kwa kuivunja.
19. Hakuna mbaraka unaoahidiwa kwa kuitunza.
20. Hakuna maelekezo yaliyotolewa juu ya namna inavyopaswa kutunzwa. Je, hii ingekuwa hivyo kama Bwana alitutaka kuitunza?
21. Haiitwi kamwe Sabato ya Kikristo.
22. Haiitwi kamwe siku ya Sabato kabisa.
23. Haiitwi kamwe siku ya Bwana.
24. Haiitwi kamwe hata siku ya mapumziko.
25. Hakuna heshma yoyote takatifu inatumika juu yake. Ikiwa ni hivyo basi ni kwa nini tuiite takatifu?
26. Inaitwa tu kirahisi “siku ya kwanza ya juma.”
27. Yesu kamwe hajataja katika njia yoyote--hakuweka jina lake kinywani mwake kulingana na kumbukumbu zinavyoonyesha.
28. Neno Jumapili kamwe halionekani katika Biblia kabisa.
29. Wala Mungu, Kristo, hata watu waliovuviwa, waliopata kusema neno moja kuipendelea Jumapili kama siku takatifu.
30. Siku ya kwanza ya juma imetajwa mara nane tu katika Agano Jipya lote. Mathayo 28:1; Marko 16:2, 9; Luka 24:1; Yohana 20:1, 19; Mdo 20:7; 1 Wakorintho 16:2.
31. Kati ya haya, ni mafungu sita yanayorejea katika siku ile ile ya kwanza ya juma.
32. Paulo aliwaelekeza watakatifu kuangalia mambo yao ya kidunia katika siku hiyo. Wakorintho 16:2.
33. Katika Agano Jipya lote tuna kumbukumbu ya mkutano mmoja tu wa kidini ulioendeshwa katika siku hiyo. Mdo 20:5-12.
34. Hakuna siri kwamba walikuwa na mkutano siku hiyo kabla au baada yake.
35. Haikuwa desturi yao kukutana katika siku hiyo.
36. Hakukuwa na umuhimu wa kumega mkate katika siku hiyo.
37. Tuna kumbukumbu tu ya tukio moja ambamo ulifanyika. Mdo 20:7.
38. Huo ulifanyka usiku--baada ya usiku wa manane. Mistari ya 7-11. Yesu aliisherehekea siku ya Alhamisi jioni (Luka 22), na mitume mara nyingine walifanya hilo kila siku. Mdo 2:42-46.
39. Biblia kamwe haisemi popote kwamba siku ya kwanza ya juma huadhimisha ufufuo wa Kristo. Haya ni mapokeo ya wanadamu, ambayo huifanya sheria ya Mungu kuwa bure. Mathayo 15:1-9. Ubatizo huadhimisha mazishi na ufufuo wa Yesu. Warumi 6:3-5.
40. Mwishoi, agano Jipya liko kimya kwa ujumla kuhusiana na badiliko lolote la siku ya saba kama siku ya Sabato ya Mungu au utakatifu wowote uliotolewa kwa Jumapili – siku ya kwanza.

     Kwa hiyo baada ya kupitia sababu hizi za ukweli wa Biblia juu ya suala hili, zikionyesha kwa kuhitimisha kwamba siku ya saba ya juma, au Jumamosi, ni Sabato ya Bwana ktika Agano la Kale na Jipya, ni nini unapaswa kuwa mwitikio wetu kwa amri hii ya nne ya Mungu?
     “Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote….Basi, imesalia raha ya sabato kwa watu wa Mungu. Kwa maana yeye aliyengia katika raha yake amestarehe mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyostarehe katika kazi zake. Basi na tufanye bidii kuingia katika raha ile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.” Waebrania 4:4, 9-11.

     “Na katika hili twajua ya kuwa tumemjua yeye, ikiwa tunashika amri zake. Yeye asemaye, Nimemjua, wala hazishiki amri zake, ni mwongo, wala kweli haimo ndani yake. Lakini yeye alishikaye neno lake, katika huyo upendo wa Mungu umekamilika kweli kweli. Katika hili twajua ya kuwa tumo ndani yake....Katika hili twajua kwamba twawapenda watoto wa Mungu, tumpendapo Mungu, na kuzishika amri zake. Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.” 1 Yohana 2:3-5, 5:2-3.

     “Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake. Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya.” Ufunuo 22:14-15.

     “Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu. Kwa maana Mungu ataleta hukumuni kila kazi, pamoja na kila neno la siri likiwa jema au likiwa baya.” Mhubiri 12:13-14.

Comments

Popular posts from this blog

SABABU 100 ZA UKWELI WA SUALA LA SABATO

JINSI YA KUINUA VIZAZI VINGI